Nanoli
JF-Expert Member
- Oct 15, 2015
- 3,735
- 5,967
Hi,
Sio mara moja, ni zaidi ya mara mbili ndani ya mwezi mmoja airtel imekua ikiniweka roho juu. Nishawahi kulipia bundle la king'amuzi cha Azam kwa airtel money, ilichukua 5 days kuunganishwa na Azam. Kwa madai wao Azam hawawezi kuniunganisha mpaka wapate malipo kutoka Airtel Money. Kwa siku tano sikuweza kuangalia taarifa za habari, mpira movies n.k
Leo tena natuma pesa kwenda Vodacom (M pesa) ni shida. Aliyetumiwa hajapata, nishapiga simu kibao huduma kwa wateja, eti wananiambia pesa imerudishwa kwenye account yako wakati huku napata zero tu.
Ninachoumia zaidi kuna wahudumu wengine hawanipi matumaini ya kupata huduma kwa wakati. Sasa sielewi huu mtandao sasa ndo umeshindwa kabisa katika huduma za pesa au ni nini?
Nyie wakuu nanyi mwakutana na kero hizi......?