Locked
Member
- Jun 11, 2017
- 26
- 97
Ni kweli kuwa kuna huduma nzuri mnazitoa,
Ila mnatakiwa kujua kuwa sisi ni wateja wenu na tunaweza kuwahama muda wowote,
1. Vifurushi vyenu vinasumbua ku- extend kama hamna huduma iyo ni bora mkaweka wazi ili tujue, kifurishi kinapoishi tusubiri hadi muda wa kuisha unapofika ndio tuunge tena.
2. Customer care service, sidhani kama mliweka kwa ajili ya kumsaidia mtu au kumpotezea mtu muda, ipo mbali sana kwa mtumiaji wa kawaida kuweza kuipata tofauti na mitandao mingine. Kwa mtumiaji ambae sio mvumilivu hawezi kusubiria hadi aipate.
3. Network yenu leo ni mbayaa sana. Kuanzia internet, voice call na msg. Na kwenye internet imeanza jana usiku na hakuna taarifa yoyote ya msingi.
Ombi langu:
Kwa mitandao ya simu tanzania tafadhali jitahidini kutoa huduma za kuridhisha kulingana na gharama zenu.
Toa taarifa kwa uma kama kunatazo lolote, hii itasaidia.