Airtel, leo kuna nini bundle zenu za internet?

Snipper

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
1,336
2,157
Sijui kama kuna tatizo kwenye simu yangu au kuna tatizo kwenye mtandao wa Airtel. Leo nimenunua vifurushi vya internet vya thamani 1GB lakini havikuchukua hata masaa matatu vikawa vimeisha.

Nikiangalia matumizi sioni kitu ambacho nimekifanya cha kuweza kumaliza GB moja nzima ndani ya masaa matatu zaidi ya kuingia Jf na kusoma meseji Whatsap. Ukiwapigia wadada wa huduma kwa wateja wala hawana majibu ya maana zaidi ya kukuambia umemaliza bundle lako.

Nikiangalia kwenye simu sioni kama kuna updates zimefanyika ambazo zinaweza kumaliza hicho kifurushi.

Airtel kama mnaanza wizi wa namna hii jiangalieni sana na tambueni hii ni January watu tuko sensitive sana na matumizi. Hapa imebidi niachane nao nihamie mtandao wa Vodacom naendelea kutiririka tu; ka bundle ka buku lakini kamekaa muda kuliko ilivyokuwa kwenye bundle ya 1GB.

Tutawakimbia tulio wengi. TCRA waangalieni sana Airtel nahisi kuna kitu hakiko sawa leo.
 
Ni
Airtel ni wezi sana wa MB. mwenyewe ni muhanga wa hilo..sa zile GB 5 kwa wiki ndo kabisa fasta zmeisha.
Nilidhani hili tatizo linanikumba mimi tu. Nimeamua kuwapa likizo maana wamevuna sana hela zangu. Bora kwenda ambako bundle lina bei kubwa lakini ukiweka linakaa nanmakato angalau yanaendana nanhali halisi kuliko kuibiwa mchana kweupe.

Hivi hili TCRA tunalipelekaje? Wana hotline ya kupiga na kupeleka malalamiko ya namna hiyo?
 
Hilo ni tatizo kubwa, juzi wamechukua GB 1 Kama masihara nimejiunga usiku, nikazima data asubuhi natumiwa msg nimetumia asilimia 100 ya bundle. Hawa ni wezi. Selikali yetu Ina kazi ya kushughulikia kina Gigi money, inaacha haya majizi.
 
Na wameshaona ni sawa kutuibia na hatuna la kufanya. Inasikitisha TCRA kutosimamia vitu kama hivi vya msingi kabisa.
 
Sijui kama kuna tatizo kwenye simu yangu au kuna tatizo kwenye mtandao wa Airtel. Leo nimenunua vifurushi vya internet vya thamani 1GB lakini havikuchukua hata masaa matatu vikawa vimeisha.

Nikiangalia matumizi sioni kitu ambacho nimekifanya cha kuweza kumaliza GB moja nzima ndani ya masaa matatu zaidi ya kuingia Jf na kusoma meseji Whatsap. Ukiwapigia wadada wa huduma kwa wateja wala hawana majibu ya maana zaidi ya kukuambia umemaliza bundle lako.

Nikiangalia kwenye simu sioni kama kuna updates zimefanyika ambazo zinaweza kumaliza hicho kifurushi.

Airtel kama mnaanza wizi wa namna hii jiangalieni sana na tambueni hii ni January watu tuko sensitive sana na matumizi. Hapa imebidi niachane nao nihamie mtandao wa Vodacom naendelea kutiririka tu; ka bundle ka buku lakini kamekaa muda kuliko ilivyokuwa kwenye bundle ya 1GB.

Tutawakimbia tulio wengi. TCRA waangalieni sana Airtel nahisi kuna kitu hakiko sawa leo.
Nilipolalamika kuhusu hili hili Wiki iliyopita tu na Uzi upo hapa hapa JF mliniona kama vile nawasingizia na naongopa. Sasa tutaelewana vyema tu.
 
Siyo leo Tuu Ni muda sasa,Nimekuwa nikijiunga nakile kifurushi Cha unlimited Gb 10 saa 6-12 asubuhi ...Ila haifiki saa name mbs zimeisha Sasa hv nimeamishia line kwenye simu ndogo ..na muda si mrefu naivunja.
 
Na wameshaona ni sawa kutuibia na hatuna la kufanya. Inasikitisha TCRA kutosimamia vitu kama hivi vya msingi kabisa.
Hao jamaa kazi yao kudukua mazungumzo ya wakosoaji tu.
maswala ya msingi wameyaweka kando
 
Last week nilikutana na ishu kama hii nikawatafuta whatsapp wananijibu kuwa simu yakao ina 4G kwa hyo bando linakwenda sana ,Ina maana hyo tecnology ya 5G ikija tu ndo watasingizia sana hyo 5G,yan majibu marahis kama yale ya kunguru kukata Umeme.
 
Hii mitandao utadhani inamilikiwa na mtu mmoja,voda,halotel na airtel wote wanalia kitu kimoja
 
Mimi situmii Airtel ila leo nimepokea simu kama tatu kutoka kwa jamaa zangu...

Wanalalamika kuhusu hili kwamba bundle limekuwa likiwaishia mapema tofauti na mwanzo (hivyo niwasaidie).

Mtu anajiunga na kifurushi cha week cha dakika 170 ambacho kwa matumiz yake ilikuwa inamfaa ndani ya week, lakini sasa hivi hatumii hata masaa 24.
 
Yaani Gb1 inaisha ndani ya saa moja na hapo haujaenda hata youtube wala haujadownload chochote zaidi ya kuingia Jf na kuchek watsap
 
Back
Top Bottom