Airtel kwa hali hii mtafukuza wateja wengi sana

Kichochoro

JF-Expert Member
Jul 18, 2017
1,135
1,163
Helow wana jf kuna shida imetokea kwangu ilikuwa tarehe 19/1/2020 nilikuwa nafanya malipo (kulipia bill) baada yakuthibitisha muamala sms iliyofuata ombi lako linashughulikiwa.

Nilikaa masaa kama mawili bila kuona sms ya mrejesho nikaamua kuwapigia huduma kwa wateja .wakasema ni kweli kuna tatzo wanalishughulikia nikaa siku nzima bila sms.

Kesho yake napo nill nikaamua kupiga simu tena nikaambiwa tatzo langu wanalishughulikia hadi leo mrejesho sijapata
Mpka sasa bado najiuliza ni hii airtel iliyokuja imenikuta nimezaliwa au ni mpya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Ombi lako linashughulikiwa"kuwa mpole ndugu maana hawajakwambia wanashughulikia kwa siku ngapi kwahyo likishughulikiwa tu bas utapata msg...kuna swali lingine tukusaidie tafadhali ndugu mteja
 
Kuna changamoto zinahitaji uvumilivu....hali hiyo ilinikuta kwa voda, walisema wanashughulikia tangu ijumaa nilipewa majibu jumanne
 
Mwingine kule kaanzisha uzi Tigo mtakufa. Na hawafi nawaambieni mtakufa nyie!!!

Tafuta pesa. Kijana kulalama bei ya vifurushi ni matumizi mabaya ya muda .

Watu tunatafutia pesa matumizi ili tupate akili ya kutafuta zaidi, mwingine unakuja kutetea matumizi. Wanawake wasiofanya kazi, mama wajane wasio na kipato, watoto ndio walalame.

Wewe mchapa kazi tafuta pesa nunua kifurushi. Voda walipopandisha nikaweka kifurushi kikubwa cha mwezi hata niache data on I'm relaxed.

Acha utamaduni wa kununua vibaba(unga robo kibiriti kinjeriti kimoja sukari kipimo bando kipimo)lipuuaaa... weka kingi usevu.

Weka jibi zako 20 tulia hutasikia hayo machungu...sasa vifurushi vya jero unajihurumia nini? Tumiaaa pesaaa

Effective money usage brings in upright senses for more finances wanasema wayunani!!!!

N'yadikwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nililipia king'amuzi Star times kwa mtandao wa Tigo sikupewa mrejesho kutoka star times.Nikawapigia wakaniambia muamala haujawafikia hivyo niwasiliane na Tigo.Tigo wakakili kulikuwa na hitilafu hivyo wangerejesha pesa au wapeleke pesa star times.Hiyo ilikuwa tar 24/11/2019 hadi leo pesa haijarudishwa wala kupelekwa star times.Nimepiga simu Tigo zaidi ya mara ishirini majibu ni yaleyale "tatizo lako tunalishughulikia".

Nataka niwafungulie kesi ya madai kwa kunisumbua.
 
Mkuu hii kesi utashida kikubwa uwe na ushahidi wakutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom