Airtel jirekebisheni

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
5,056
2,850
Unampigia mtu simu hajapokea simu mnaandika call ended na mnakula salio la sh 10.Hatua inayofata nikupiga simu mbele ya wakaguzi wa TCRA ili mnirudishie sh 10 mlizozikataga .Jirekebisheni.Fedha yenyewe ngumu mtaani.
 
Huu mchezo mwanzoni nilijua ni simu yangu ndio inazingua baada ya mtu mwingine tena kuniambia nikajua alaa kumbe naliwa kiboya. TCRA msiishie kutizimia simu zetu walalahoi fanyeni kazi yenu kwa uhakika na haki.
 
Mimi niliwaandikia mpaka email, wakijifanya kunipigia na kubisha. Niliambatanisha mpaka na screenshot ya sekunde kumi wanazokula badala ya moja iliyotumika lakini bado wakabisha na kujifanya kutumia lugha za uongo. Walipoona napuuzia simu zao wakatuma msg kuwa tatizo lako limerekebishwa wakati kiukweli hakuna kurekebishwa kokote. Wengi wanapuuzia kuona ni sekunde chache lakini kama kwa siku wakiwaibia wateja mil. 3 sekunde 9 unadhani wanajipatia kiasi gani kwa udanganyifu.
TCRA badala ya kufuatilia watu wanaomuita baba j majina ya kumtusi ni bora wangetetea haki zetu watumiaji wa simu. Airtel ni jipu kubwa mno linalopaswa kutumbuliwa.
 
Back
Top Bottom