Airtel jirekebisheni kwenye huduma kwa kwa wateja

gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,566
2,000
Habari za muda,

Nasikitika kua mtandao mkubwa kama airtel wanaweza kua na huduma mbovu kama hii. Wiki iliyopita nilipoteza simu iliyokua na line ya airtel ndani,Simu ambayo nilienda hadi kutoa taarifa kituo cha polisi nakupata RB namba.line hiyo iliyopotea nimekua nayo toka mwaka 2007 hadi sasa na imepotea ikiwa na namba za watu zaidi ya 180 tena ikiwa ndani ya simu yenye gharama ya mifuko kadhaa ya cement.

Sasa kilichoniudhi ni nilipoenda kwa wakala wa airtel kwa ajili yaku swap iyo line ili nisikosekane hewani maana iyo namba inatumika hadi na matumizi ya ofisi nikakutana na vikwazo visivyoeleweka.

Niliwakilisha vyote nilivyoambiwa na wakala niviwasilishe ikiwemo namba 5 nilizowasiliana nazo karibuni pamoja na kitambulisho chochote kinacho nitambulisha mimi ni nani.Vyote ivyo niliwakilisha.

Yule wakala akawapigia hao huduma kwa wateja akawajulisha kua anataka kuswap line akaulizwa maswali akayajibu mwishoni akaambiwa anipe simu niongee na huyo mtoa huduma.

Swali la kwanza akaniuliza jina langu nikamwambia kisha akauliza tarehe ya kuzaliwa na sehemu nilipozaliwa yote nikajibu sawasawa kulingana na taarifa nilizoandika wakati nasajili namba yangu.

Baada ya hapo akaniuliza nina kiasi gani cha pesa kwenye akaunti yangu ya airtel money. Nikamwambia kiasi ila tarakimu za mbele nikawa sizikumbuki vizuri mana mara ya mwisho nilinunua luku sasa sikukariri ile meseji ya kiwango kilichobaki na simu yenyewe ndo iyo iliyopotea.

Shida ikaanzia hapo uyo mdada akaniambia bila kumjulisha kiasi kamili hawezi kukubali kunifungulia iyo line. Sasa kilichonikera ni hichi. Mtu hajali nimepoteza simu yenye majina kiasi gani au gharama zake alafu yuko tayari nipoteze contact za watu zaidi ya 150 bila kujali ni hasara kiasi gani ntakua nimeipata kisa salio la airtel money.

Najua kupoteza simu ni tatizo langu lakini ninachojiuliza ni hiki inakuaje hawa watoa huduma kushindwa kunitendea haki mimi kama mteja wao wa muda mrefu kisa salio la airtel money.

Sasa najiuliza waliuliza taarifa zangu za nini kama wanajua kitakachoamua mimi kurenew line yangu ni salio la airtel money.

Na kama salio nikigezo cha chakupata line nyingine sasa sehemu kwenye airtel money yakuangalia salio kazi yake ni nini kama mnajua watu watakua wanakumbuka salio kwenye akaunti zao.

Badilikeni bana maana mimi sidhani kama salio la airtel money inaweza kua sababu yamimi kukosa huduma, maana yakukosekana hewani hadi leo maana huduma ya airtel money ni huduma yakipesa wakati mimi nakosa huduma yamawasiliano ambayo kwangu nimuhim mara elfu kuliko iyo airtel money yenu. Kwanini msiwe na utaratibu mwingine utakaowapatia huduma ya mawasiliano wateja wenu badala yakucomplicate mambo.

Mimi binafsi mnaenda kunipoteza maana sidhani kama nitakumbuka hiyo balance. Badilikeni bana vinginevyo ule mtandao mwingine utaendelea kuwaburuza mwanzo mwisho.
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,186
2,000
Airtel inaongoza kwa Huduma mbovu kwa sass. Ikifuatiwa name Tigo

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
Customer Care wao kupokea simu ni Majaaliwa,
Kuna siku nilipa Airtel Customer Care, masaa mawili haipokelewi,
Na hii hutokea mara kwa mara,
Nakumbuka siku ambayo waliwahi kupokea siu yangu ilikua ni baada ya kuita kwa dakika 32 (zaidi ya nusu saa)
 

Mbwa dume

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
3,315
2,000
Customer Care wao kupokea simu ni Majaaliwa,
Kuna siku nilipa Airtel Customer Care, masaa mawili haipokelewi,
Na hii hutokea mara kwa mara,
Nakumbuka siku ambayo waliwahi kupokea siu yangu ilikua ni baada ya kuita kwa dakika 32 (zaidi ya nusu saa)
Mi kilichofanya niwahame ni hicho tu.!
Unapata tatizo unapiga huduma kwa wateja simu haipokelewi na ikibahatika kupokelewa atakuuliza jina kisha anakata simu.!
Yaani niliumia sana!!!
Na sina mpango nao tena!
 

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
464
500
Aisee kumbe huu mtandao bado upo na watu wanautumia... Poleni sana.... Sina hamu nao tena kuna siku nilikuwa naweka pesa kiasi kikubwa tu kwenye namba yangu ya airtel money wakala alikosea namba moja ikaenda kwa mtu mwingine ishu ikawa kurudisha hadi nikasamehe mara uwapigie wasipokee mara sijui subiri baada masaa 24.... Ikafika wiki baadae wiki mbili.. Hatimae nikasamehe na ukawa no mwisho wangu wa kutumia huo mtandao ilikuwa 2011...ukiachilia mbali hilo la pesa pia hata baadhi huduma zao nyingine sikuridhishwa nazo kabisa
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,186
2,000
Mi kilichofanya niwahame ni hicho tu.!
Unapata tatizo unapiga huduma kwa wateja simu haipokelewi na ikibahatika kupokelewa atakuuliza jina kisha anakata simu.!
Yaani niliumia sana!!!
Na sina mpango nao tena!
Tena wakati wanajitambulisha hua wanatajaga majina yao kwa haraka na kwa kumung'unya maneno ili hata baadae akija kukata simu usiweze kumshitaki sababu hujui hata ulikua unaongea na nani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom