Airtel hawazingui kwenye airtel money?

Kibishi

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,139
1,028
1: Ukiweka pesa kama akiba halafu siku za mbele ukitaka kutoa hukuti imeyeyuka kimaajabu?

2: Ukitumiwa pesa na mtu halafu ukitaka kuzitoa meseji ya kutumiwa haichelewei kufika?

3: Weka maudhi na mabaya mengine kama yapo.

Mliotumia airtel money kwa muda mrefu tuelezeni.
 
Ukikosea kutuma pesa. Kumbuka Customer Care yao Haipatikani andika maumivu. Kwa kifupi ni mtandao hovyo sana kwenye eneo la simu pesa.
 
Kwenye kupitiapitia mtandaoni jinsi wateja wa airtel money wanavyolalamika, nimegundua hasara za airtel money zifuatazo:

-Ukinunua huduma yoyote, hutoipata muda unaotaka.

-Password ikianza na 1 au tarakimu zikijirudia kuna kufungiwa laini yako siku za mbele.

-Mawakala wenyewe wanalalamika kuwa commission ni ndogo.

-Ukimtumia mtu pesa, kama hajapata meseji ya uthibitisho, hesabia pesa uliyotuma hairudi kwako na yule uliyemtumia hapati kitu.

-Kama una jambo la maana la kununua, usiweke asilimia 100 kutoa pesa airtel money ili ukanunue hiko kitu.

-Wahudumu wake mteja kwao mavi.

-Huduma kwa wateja unachajiwa sh.60 kwa kila simu unayopiga.

-Huduma kwa wateja simu itaita mpaka uchoke hamna mhudumu anayepokea.
 
Ukikosea kutuma pesa. Kumbuka Customer Care yao Haipatikani andika maumivu. Kwa kifupi ni mtandao hovyo sana kwenye eneo la simu pesa.
Kwenye smartphone laini zote ukiweka 2G yaani E, simu inadumu sana na chaji, laini yao haikubali kusoma E kwenye simu yangu, ukiweka E inaonyesha blank tu, haisomi. Tatizo lingine hilo
 
Ukiingia mtandaoni ulinganishe makato ya kutuma na kupokea pesa, airtel money ina makato kidogo kuliko wote, kasheshe inakuja ukianza kutumia hiyo airtel money yao.....
 
Mkuu,mimi nina Airtel money na Mpesa,lakini sijawahi kupata shida ya lolote na bundle zao zinakaa sana ,,,,mwezi mzima
-Hujawahi kwenda kutoa pesa halafu ukakuta mtandao unasumbua?
-Akiba yako haijapukutika wewe bila kujua?
-Ulishawahi kumtumia mtu pesa?
-Ulishawahi kutumiwa pesa?
 
-Hujawahi kwenda kutoa pesa halafu ukakuta mtandao unasumbua?
-Akiba yako haijapukutika wewe bila kujua?
-Ulishawahi kumtumia mtu pesa?
-Ulishawahi kutumiwa pesa?
Mimi ninatuma sana pesa bank,kutoa bank to airtel money na kulipa vibarua na airtel money karibu kila siku mkuu.
 
Hata miezi 6 bila tatizo, voda nilishavunja line yao kabisa sababu ya gharama kubwa na network kusumbua. Binafsi sijawahi kuona tatizo kabisa
Unawekaga salio kubwa au dogo?
Kuhusu voda, gharama za m-pesa za kutoa na kuweka pesa ni kubwa kuliko halo pesa, tiGO pesa na airtel money, hata 3G yao ni mbovu kuliko ya tiGO, voda wako vizuri kwenye 2G.
 
Sijui kuna nin eartelwapo wezi wanaoibia watu simu na kisha kusambaza ujumbe wa kukutaka uwatumie hela kutumia line za eartel sjajua kuna tatizo gani...=
 
Unawekaga salio kubwa au dogo?
Kuhusu voda, gharama za m-pesa za kutoa na kuweka pesa ni kubwa kuliko halo pesa, tiGO pesa na airtel money, hata 3G yao ni mbovu kuliko ya tiGO, voda wako vizuri kwenye 2G.
Mimi huwa naweka kiasi chochote elfu 3 mpaka m3
 
Mimi huwa naweka kiasi chochote elfu 3 mpaka m3
Una upepo na airtel money, miaka yote hiyo hamna hata tatizo!, wakala wa airtel money huwa wanalalamika commission ya airtel money ni ndogo sana, wanasema airtel money hakuna faida, ndiyo maana mtaani mawakala wa airtel money ni wachache
 
Back
Top Bottom