Airtel/ Airtel Money acheni hizi dhuluma, Mamlaka husika liangalieni hili suala

EIFFEL

Member
Jul 20, 2018
34
400
Habarini za jioni wakuu,

Poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa letu.

Binafsi naomba niwasilishe malalamiko yangu kwa hawa AIRTEL TANZANIA kutokana na vitendo vyao hivi ambavyo ni viashiria wazi vya dhuluma kwa wateja wao.

Kwa kawaida hua sipendi kununua bundles kwa vocha za kukwangua kwa sababu ya kuokoa muda na kutokua na access nazo kiurahisi, instead hua ninatumia AIRTEL MONEY. Lakini leo situation imekua tofauti, nimejiunga kifurushi changu kama ilivyo ada kwangu, unfortunately nkapokea ujumbe wa huduma hio kutokuwepo hewani labda njaribu tena baadae, lakini pesa WAMEKATA. Kuangalia salio la kifurushi ni 0 MBs, nikasema ngoja njaribu tena nkapokea ujumbe huo huo kwa mara nyingine na hela yao wakakata tena bila ya kuniunga kifurushi.

Nika-opt kuwapigia customer care, nikaishia kuambiwa leo kuna tatizo katika mtandao wao na pesa yangu itarudishwa ndani ya masaa yasiyozidi 24.

Lakini hii si mara ya kwanza hii situation kutokea kwangu ni mara ya 3, ma the previous 2 times hela yangu haijawah kurudi, wanaishiaga kunipa tu calender kuwa pesa yako inarudi ilhali huwa hawarudishi.

Leo nikasema no this is not right, namuuliza mtu wa huduma kwa wateja, kama kuna hitilafu kwanini sisi wateja hatupewi notice mapema kuhusu kutonunua kifurushi kwa njia ya AIRTEL MONEY? OK fine, hamjatoa notice kwanini mnakata hela ilhali hamniungi kiufushi?

Hana majibu ya kunipa anaishia tu kusema pesa yangu itarejeshwa.

Sasa nawauliza nyie AIRTEL,

1. Kwanini mnakata pesa za wateja wenu bila kuwaunganisha kifurushi?

2. Kama kuna hitilafu ya muda mfupi kwanini hamtoi taarifakwa wateja wenu mapema ili watafute njia mbadala mapema?
 
Siku zote pesa ukinunua kifurushi huwa hairudi. Yaani hapo utazungushwa lakini pesa kurudi sahau.
 
Hata Tigo wanamchezo huo, na pesa huwa hawarudishi
Leo nilikua na dakika 80 Tigo to Tigo, nikanunua vocha nikaweka sikuunga kwakua nilitaka kumpigia mtu wa mtandao mwingine.

Kabla sijaunga mtu wa Tigo akaomba nimpigie, ebwana eeeh ile nmemaliza kuongea pesa imeliwa yote na dk80 zile hawajatumia hata1 nimebaki nimepagawa unakuaje wanakula salio wakati dakika zimejaa?
 
Ngoja tujipange kuwasongesha kwa pilato ndio watajua kuwa fidia huwa inategenea na status zetu wengine, huwezi kukwamisha mipango yangu kuanzisha kiwanda kipuuzi

Tanzania ya Viwanda 2020
 
Leo nilikua na dakika 80 Tigo to Tigo, nikanunua vocha nikaweka sikuunga kwakua nilitaka kumpigia mtu wa mtandao mwingine.

Kabla sijaunga mtu wa Tigo akaomba nimpigie, ebwana eeeh ile nmemaliza kuongea pesa imeliwa yote na dk80 zile hawajatumia hata1 nimebaki nmepagawa unakuaje wanakula salio wakati dakika zimejaa?
Ndio tabia yao wezi
 
Ebana ni wiki 3 sasa nafuatilia kwa ukaribu mambo wanayonifanyia Airtel.

1. Vifurushi vilianza kuexpire kabla ya muda, yaani nikiunga cha 24 hours saa saba mchana kufikia kesho saa tano kinakuwa hakipo.

2. Hili suala la kununua kifurushi cha MB wananipangia matumizi, nilinunua MB 500 kabla sijazitumia nikakuta salio 249 MB, nikawapigia wakadai wamezigawa 250 MB mchana na 250MB usiku.

Basi nimeunga kifurushi mchana nikatumia kidogo tu wakaniambia MB za mchana zimeisha.

Kimbembe usiku, mida yenyewe saa 5, mzee mzima nimelala saa 2 ili saa 5 niamke nitumie MB zangu.

Ebana ee nikazani PC yangu haina network, hapakuwa na MB hata 1. yaani Airtel wanaiba bila aibu.

3. Kali ni kuwa ukinunua hicho kifurushi cha MB 500 salio linaonesha MB 250 na hizo zingine kama ambavyo huzioni ndo hutazitumia pia.

Airtel mmenishinda tabia nasubiri pakuche nihame mtandao tu.
 
[QUOTE="EIFFEL,

mkuu hakuna mtu anapenda kua na hitilafu katika biashara yake: hivi vitu huwa vinatokea sana lakini kwa bahati nzuri huwa wanarekebisha, so wape muda tu hakuna mtu alieperfect:

and this doesnt mean hakuna hitilafu zitatokea tena kwa sababu matatizo huja unexpected
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom