AirTel 1/4 sh from 11pm-6am ni Uwongo na kuvunja haki za wateja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AirTel 1/4 sh from 11pm-6am ni Uwongo na kuvunja haki za wateja

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by newmzalendo, Feb 17, 2011.

 1. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,362
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kufuatana na matukio ya leo na dharula,nimetumia simu yangu ya Air tel usiku after 11pm,wamekata pesa kubwa kama kawaida
  nikaamua kwenda ktk website ya airtel.com nikakuta offer ya robo shilingi bado ipo.

  TCCRA wanasimamia huu uozo wa kudanganya wateja?
  nikitaka ku complain kwa Airtel kuna uwezekano wa kuwa refunded hiyo pesa?

  kwa waliowahi kufaidika na hii 1/4shilingi uliwahi kuitumia lini.
   
 2. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkubwa sawa kabisa hata mimi nilipiga simu jana around saa 11.15 na nikakatwa pesa kama kawaida tena tukaulizana sana na wife wangu kwanini wamekata. hivi asubuhi naammkia hapo ofisi za airtel wanieleze kulikoni.
   
 3. G

  Gabriel Jr New Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wana jamii forum,malipo ya kupiga simu za Airtel kwenda Airtel kuanzia saa tano usiku mpaka saa kumi na mbili asubuhi ni robo shilingi kwa sekunde,naomba kwa ambae anadhani alikatwa pesa zaidi anipatie namba yake na tarehe uliyopiga simu ili niweze kuangalia na kushugulikia suala lake na kumpatia feedback, I will be more than willing to assist you and provide any clarification if need be.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wewe ni Airtel?
   
 5. G

  Gabriel Jr New Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari dugu,ndio mimi ni mfanyakazi wa Airtel naomba nikusaidie tafadhali kuhusiana na hili suala lililoletwa na mwana jamii mwenzetu,viwango vya kupiga simu Airtel kwenda kuanzia saa tano usiku 11pm mpaka saa kumi na mbili asubuhi 6am ni robo (1/4) shilingi.
   
 6. G

  Gabriel Jr New Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari ndugu wana Jamii forum,
  kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu katika kituo chetu cha huduma kwa wateja namba 100, au unaweza kututumia barua pepe helpdesk@tz.aitel.com ili tuweze kukuhudumia katika suula hili la mpango wa malipo wa robo shilingi kwa kupiga simu za Airtel kwenda Airtel kunazia saa tano usiku mpaka saa kumi na mbili asubuhi (11;00pm - 06;00am) au unaweza ukanipigia simu kwenye namba 0787 500 500 ili nikuhudumie.
  Pia kama una swali lolote,au unahitaji maelezo yoyote kuhusiana na huduma zetu tafadhali wasiliana nasi na tutakuhudumia.
  Ahsante.
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii ndo TZ waungwana. Biashara zinaenda na udanganyifu perpendicular
   
 8. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Gabriel Jr. Nimekutumia PM juu ya concern yangu, kwa kifupi hata mimi nimeshakatwa hela nyingi zaidi ya hicho mnachokisema.
  Sizani kama mnakisimamia hicho manachokitangaza.Pia kwanini hizi promotion mziweke usiku wakati mnajua watu wengi wanakua wamelala kama kweli mna haja ya kusaidia watu basi fanyeni kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa tano usiku ili kila mtu afaidi.

  Kuna hizi zawadi mnazozitoa sijui za magali nk.Kuna mtu alishapewa zawadi ya gari akadai kuna mtu wa alimpatia million 8 kwa ajili ya kupata zawadi hiyo. Mtu mmoja akaniambia kua yule mtu anayekua anayebonyeza compyuta pale hana uelewa wa kutosha juu ya mambo ya IT sasa nyie makampuni ya simu mnakua mmeshategesha # ya mshindi.
   
 9. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kaka hawa jama ni waongo sana na wanaboa atakua ni mmoja wao na kaingi JF baada ya kuon hii ishu. Ngoja niweke thread nyingine ya AIR PATEL!
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Sio airtel peke yake hata tigo ndio waizi wa wazi wazi kabisaaa
   
 11. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  :A S 101: Promosheni ya mitandao yote ni wizi mtupuuuu........
   
 12. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jamani kuweni makini kutoa namba zenu kwa mtu anayedai kuwa ni mfanyakazi wa Airtel anaweza kuwa usalama wa taifa anawapepeleza hapa jukwaani.
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,362
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Airtel wanasema 1/4 shilingi kwa huo usiku, huyu Gabriel Jr anasema robo shillingi kwa sekunde,mbona tangazo halisemi robo shilingi kwa sekunde?
   
 14. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana kuona kila kampuni inapoingia nchini inakuwa na lengo la kuvuna chee bila jasho. Moja ya wizi wa waziwazi wa hii inayoitwa Airtrel (Zamani Zain) ni hii promosheni yao ya Jirushe ya dakika 15 na kwa Tsh 250 na Dakika 30 kwa 500. Jamaa hawa hutuma msgs za kukuhamasisha ujiunge na Jirushe ya Dakika 15 kwa kutuma msg kwenda 155558 na ukituma tu wanakutumia msg ya kukupongeza na kukueleza namna ya kupiga simu na kuuliza salio la msg na simu. Lakini kinyume chake hutokea. Kila upigapo wanaendelea kukukata fedha na kukutumia msgs za gharama ulizotumia kwa mazungumzo hadi inapofika muda wa mwisho wa kujirusha. Mimi nimeshajaribu zaidi ya mara kumi na zote nimeliwa hela mara ya mwisho ni leo hii. Tunaomba Tume ya mawasiliano iwabane vibaka hawa. Kwa juu juu, shilingi 250 zinaonekana ndogo; lakini inafahamika kwamba mitandao hii ina watu zaidi ya milioni tano, sasa tafakari endapo waliohamasika kama mimi na kuibiwa 250 hizo tutafikia milioni moja kwa siku. Wahuni hawa watakuwa wamekomba milioni 250 kwa mpigo kiulainiii!
  Nasisitiza tena hakuna rongorongo za kina Gabriel hapa bali uchunguzi ufanywe na wawajibishwe. Hilo la robo shilingi ni uongo mtupu kwani kila ninapopiga simu nakatwa kama kawaida.
   
Loading...