Zanzibar-Nyamwezi
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 1,244
- 766
Wakuu hili jambo la Polisi lamba-lamba ovyo airport mbili ambazo mimi natumia karibu kila wiki Zanzibar na Daressalaam, Polisi wanaomba rushwa nje nje, yaani wananyoosha mkono kwa mtalii kama omba omba hivi.
La ajabu ambalo nimeshuhudia tukio la kwanza Daressalaam December 2012 mtalii kutoka Ulaya akilalamika, na bahati nzuri naelewa vizuri alichokuwa anahadisia kwa kundi la wenzake, yeye alikuwa anasubiri ndege ya transit kuelekea Zanzibar, Mama huyo alibanwa, akaomba msaada polisi, aonyeshwe choo, polisi kamkatisha kona mbili hivi halafu kamwomba Dola kumi ili amwonyeshe choo.
Mama huyo hakumpa alirudi tu, sio kuwa hana, ila hakupenda njia aliyotumia polisi huyo ya kuomba rushwa eti tu kwa sababu amebanwa.
Alidhani polisi vijibwa vyetu ni kama Maafsa wa Kwao ambao ndio kimbilio la Raia kwa kila kitu.
nimehadisia hapa Zanzibar, nikaambiwa hapa ndio mbaya zaidi kuliko Dar polisi omba omba airport.
NDUGU ZANGU AIRPORT NDIO PICHA YA KWANZA YETU SOTE KAMA WATANZANIA, TUPAMBANE NA KILA ANAEJARIBU KUTUCHAFULIA NYUSO ZETU MLANGONI.