Airport yetu ya Dar inanuka uozo wa rushwa!

salmar

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
799
362
Nikiwa muathirika mkuu wa jambo hili limeniuma sana tena sana na sijui watanzania wangapi washafanyiwa hili jambo. Nikiwa miongoni wa wasafiri na kusubiri mizigo yetu pale sehemu ya kukusanyika mizigo nami nilikua na ka TV kangu nimekuja nacho kumbe sikua peke angu na kulikua na wazungu nao walikua na ma music system na vifaa vya electronic vyingine.

Baada ya kupakia kwenye kitoroli changu nikasimama nyuma ya wale wazungu hapo ndo wakaja watu wawili mmoja akajitambulisha kama TRA na mwengne kama ofisa usalama nikawauliza shida yao wakanijibu hii tv ukailipie ushuru nikamwambia sawa but na wale wazungu pia wakalipie ushuru music system zao yule jamaa wa TRA akaja juu wewe usituchagulie mtu wa kulipa ushuru nikamjibu mimi ni mhasibu na najua wajibu wa kulipa kodi so waite na wale walipe otherwise nitatafuta haki mbele ya safari akauchuna na kuondoka zake huku akinitazama kwa jicho la ushenzi. Nilipo muhadithia jamaa yangu mmoja ambae ni mhasibu pia akaniambia wale ni wababaishaji na sijui hata kama ethnic ya uhasibu wanaijua.

My take,
Serikali pamoja na watu wa idara ya mapato tupieni jicho airport maana kuna ushenzi wa hali ya juu. Na sitalifungia jicho hili suala nitahakikisha namfikishia kitilya alivalie njuga
 
nchi hii kila mahala kumeoza, airport pameoza, bandari pameoza, tra pameoza, polisi kumeoza uozo uozo uozo wa rushwa kila mahala
 
Hiyo tabia mbona ipo muda mrefu...? Na watu tumelizwa sana hapo airport na hao jamaa.
 
Kuna rushwa sana Airport,wanapenda sana ukizubaaa utaliwa hela hasa kama unatoka nje ya nchi,vile vile wanakupiga mkwara na kama hujui sheria basi inakula kwako,inabidi uchunguzi ufanyike.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Na wahasibu ndo wameoza zaidi ya wote....... Wachakachuaji wakubwa kwa hiyo na yeye kakumbana na wenzake.
 
Mkuu. Sio kila mhasibu ni jambazi na fisadi mm binafsi nina audit firm yangu na sijawahi kumdhulumu mtu wala serikali yangu so na mm sipendi kudhulumiwa
 
Rais wao mwizi, watakuwa wananch mkuu, hii ni nchi ya majuha akili zao zishaoza kwenye rushwa, muda wote ufikiria kuiba na sio utendaji wa kazi

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nikiwa muathirika mkuu wa jambo hili limeniuma sana tena sana na sijui watanzania wangapi washafanyiwa hili jambo. Nikiwa miongoni wa wasafiri na kusubiri mizigo yetu pale sehemu ya kukusanyika mizigo nami nilikua na ka TV kangu nimekuja nacho kumbe sikua peke angu na kulikua na wazungu nao walikua na ma music system na vifaa vya electronic vyingine.

Baada ya kupakia kwenye kitoroli changu nikasimama nyuma ya wale wazungu hapo ndo wakaja watu wawili mmoja akajitambulisha kama TRA na mwengne kama ofisa usalama nikawauliza shida yao wakanijibu hii tv ukailipie ushuru nikamwambia sawa but na wale wazungu pia wakalipie ushuru music system zao yule jamaa wa TRA akaja juu wewe usituchagulie mtu wa kulipa ushuru nikamjibu mimi ni mhasibu na najua wajibu wa kulipa kodi so waite na wale walipe otherwise nitatafuta haki mbele ya safari akauchuna na kuondoka zake huku akinitazama kwa jicho la ushenzi. Nilipo muhadithia jamaa yangu mmoja ambae ni mhasibu pia akaniambia wale ni wababaishaji na sijui hata kama ethnic ya uhasibu wanaijua.

My take,
Serikali pamoja na watu wa idara ya mapato tupieni jicho airport maana kuna ushenzi wa hali ya juu

sasa kama na huyo unayemwita usalama wa taifa njaa imemuathiri hadi kwenye ubongo unadhan juna jipya hapo,mwakyembe kaz unayo
 
wale nilishawasoma ukishuka na emirates mchana ndo unawakuta,ukishuka na swiss au klm huwakuti huwa najiuliza why na sipati jibu
 
Ule uwanja kuupa Jina la Mwalimu Nyerere ni aibu kubwa sana, ni bora wangeubadilisha jina na kuita Mkapa au Kikwete kwa jinsi ulivyojaa rushwa. Mwalimu alikuwa sio mlarushwa au mfujaji wa mali zetu. Uwanja wenyewe mchafu, vyoo vichafu, wafanyakazi walarushwa kama waajiriwa waliopangishwa na watanzania kule Magogoni. Hauna maana au faida yoyote kwa watanzania. Tena ukishuka pale ukiwa mtanzania ndio wanakuumiza sana kuliko mgeni, hii nchi imelaaniwa sana wenyewe kwa wenyewe hatupendani.
 
wale nilishawasoma ukishuka na emirates mchana ndo unawakuta,ukishuka na swiss au klm huwakuti huwa najiuliza why na sipati jibu

Ni kweli nilishuka na emirates bt sitakomea kwao nitahakikisha hili suala namfikishia kitilya
 
Ukienda nchi za wenzetu wanavowathamin raia wao utaona hadi raha shuka kwetu na wakujue mtanzania utafurahi na roho yako
 
Wakiona huna kitu cha kuwapa rushwa wanaomba vitu mpaka perfume utafikiri wamerithi kwa Kikwete kuombaomba. Wafanyakazi wote pale Kikwete International Corruption Airport ni Majambazi na waporaji wa mali za watanzania, wageni wanawaogopa Wapumbavu sana wale wezi Kikwete International Corruption Airport
 
Kwa kweli sijui ni sehemu gani ya airport yetu hainuki.

Unapo "check-in" kuna wale walinzi wanaozungukazunguka pale kwenye ile "hall". Wao wamejitafutia kazi ya ziada ya kukuuliza kama una cheti cha chanjo. Kama huwa wanaweza kukutafutia haraka haraka. Halafu ukiwa unapima mizigo wanaanza ushabiki wa kilo zilizozidi wakitafuta uhonge kitu fulani ili uachiwe.

Unapoingia nchini ukifika sehemu ya kuchukulia mizigo unakutana na kundi la watu ambao hawajawasili na ndege bali wapo mle ndani kukusaidia kusukuma toroli lako, kama ukipenda, hulazimishwi. Kwa hiyo tuna wapiga debe mpaka ndani ya viwanja vyetu vya ndege.
 
Ni kweli nilishuka na emirates bt sitakomea kwao nitahakikisha hili suala namfikishia kitilya
Kitilya hafanyi lolote kwani unadhani hajui anayajua vizuri sana,kuna yule mama pale ndio mkubwa wao yule mwenye vijiguu kama kuni za nyongeza ndio kisirani,nilikwenda na rice cooker ya kg1 nikamwambia mwambia niya mdogo wangu yuko shule alinambia lete risiti nikamwambia sina basi nenda pale kalipia yule jamaa atakuandikia,alinikera nikamwambi aiwache nipe risiti nikirudi ntaichukua..
 
Nikiwa muathirika mkuu wa jambo hili limeniuma sana tena sana na sijui watanzania wangapi washafanyiwa hili jambo. Nikiwa miongoni wa wasafiri na kusubiri mizigo yetu pale sehemu ya kukusanyika mizigo nami nilikua na ka TV kangu nimekuja nacho kumbe sikua peke angu na kulikua na wazungu nao walikua na ma music system na vifaa vya electronic vyingine.

Baada ya kupakia kwenye kitoroli changu nikasimama nyuma ya wale wazungu hapo ndo wakaja watu wawili mmoja akajitambulisha kama TRA na mwengne kama ofisa usalama nikawauliza shida yao wakanijibu hii tv ukailipie ushuru nikamwambia sawa but na wale wazungu pia wakalipie ushuru music system zao yule jamaa wa TRA akaja juu wewe usituchagulie mtu wa kulipa ushuru nikamjibu mimi ni mhasibu na najua wajibu wa kulipa kodi so waite na wale walipe otherwise nitatafuta haki mbele ya safari akauchuna na kuondoka zake huku akinitazama kwa jicho la ushenzi. Nilipo muhadithia jamaa yangu mmoja ambae ni mhasibu pia akaniambia wale ni wababaishaji na sijui hata kama ethnic ya uhasibu wanaijua.

My take,
Serikali pamoja na watu wa idara ya mapato tupieni jicho airport maana kuna ushenzi wa hali ya juu. Na sitalifungia jicho hili suala nitahakikisha namfikishia kitilya alivalie njuga

asante,walinipora euro 100 yangu hao watu wanajiita usalma wa taifa wakiongozwa na jamaa mmoja anaitwa somebody mujwambusi kwa kisingizio nimebeba unga.wamenisachi hawajakuta kitu wakaishia kupora pesa bila kosa.naandaa hicho kisa kamili ntakileta hapa:A S angry:
 
Kitilya mwenyewe mla rushwa asingekuwa mla rushwa haya yasingetokea chini ya utawala wake, Kwa ujumla TRA imeoza kwa rushwa na mapato wanayakusanya ni pungufu kwa zaidi ya aslimia sabini pamoja na kujigamba wanavuka lengo
 
J Kikwete International Corruption Airport inanuka wizi na rushwa, wafanyakazi wenyewe ndio wakina Pdidy wanjaa utafikiri hawalipwi mshahara, wezi sana wakiona wageni wanawaogopa kisa hawajui kuzungumza ingilishi, ndio kisa cha kutowasumbua abiria sio watanzania
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom