Airport - Karamagi uso kwa uso na Zitto

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Kwa mara nyingine tena viongozi wa upinzani na wa CCM wanagongana airport..(nyama za mashirika ya ndege???). Safari hii ni Mhe. Zitto akitokea Nairobi kwenye mkutano wa Raila Odinga na akagongana airport na baadhi ya mawaziri wa CCM ambao walikuja kumpokea Rais... Mawaziri wengine hawakuonesha husuda miongoni mwao ni mama Meghji... Mhe. Karamagi naye alikuwepo lakini alijifanya hakumuona Zitto na hivyo kuamua kumchunia kimya kimya... More details to come...
 
Hilo Mkuu ni la kutegemewa kabisa kabisa, nadhani huyo jamaa anajiuliza muungwana atafanya nini akitinga home....nahisi kuna kitu, ngoja tuone....

Zitto kwani naye ni chungwa ama inakuwaje hapo?
 
Ningelikuwa mimi Zitto ningeenda kumpa mkono Karamangi.

Ukitaka kuumbua watu kuna njia nyingi sana.
 
Thread Failed. why do we have to make a big deal out of every little thing ? jamani, mwanakijiji vipi tena wewe mkuu ? kama karamagi kamchunia zitto thats them, tunachotaka maendeleo, salamu zao hazina umuhimu kwenye taifa letu !
 
There are three possibilities/probabilities

1. Mh. Karamagi Kumchunia Mh. Zitto
2. Mh. Zitto Kumchunia Mh. Karamagi
3. Waheshimiwa wote wawili kuchuniana.

Swali: convince us why #2. and not #1 or # 3 above?
 
Thread Failed. why do we have to make a big deal out of every little thing ? jamani, mwanakijiji vipi tena wewe mkuu ? kama karamagi kamchunia zitto thats them, tunachotaka maendeleo, salamu zao hazina umuhimu kwenye taifa letu !

Mzee anaelekea kubaya!!! Unapomshambulia mtu/kiongozi beyond mambo yanayohusu maslahi ya taifa,,, ni ushabiki ambao hauna uzalendo ambao tuna-claim hapa!

Naanza kukumbuka watu waliokuwa wakereketwa/wafukukutwa/ngangari/ngunguri!!! Hoja zao zilikuwa hazitofautiani sana na ujumbe wa thread hii!!!

No wonder watu makini kama Said Yakub siwasikii tena!!!
 
There are three possibilities/probabilities

1. Mh. Karamagi Kumchunia Mh. Zitto
2. Mh. Zitto Kumchunia Mh. Karamagi
3. Waheshimiwa wote wawili kuchuniana.

Swali: convince us why #2. and #1 or # 3 above?

Hapo! hapo! hapo sasa!
 
..ningemchunia!

..it's convinient,hasa ukizingatia hali ya hewa ilivyo angani!

..it's natural!
 
wakuu wote nasemba muendeleze mapambano no changes yeyote toka kwa JK.Ndiyo maana kaitwa Muungwana na mtauona uungwana wake sasa .Hana atakalo fanya wote genge moje . Hoja ya Kilitime sitaki iniulie muda na kama hajaona haja kutofautiana kwa maslahi ya Taifa lakini mkiwa kama wanadamu uso kwa uso salaam na upendo ni muhimu basi hapa kuna shida kubwa kwa upande wako na huyu Kanda Pinzani. Wagombane kwenye jukwaa la Siasa tofauti ziwepo lakini upendo na utu ubakie pale pale au ?
 
Nadhani tunaweza kuliangalia hili wka upana zaidi...

Zito an Karamago wote ni wanasiana....na kwa utaratibu wetu walau wa kipindi hiki nimeona mara nyingi viongozi mbalimbali wa 'upinzani' walishiriki kwa pamoja mambo mbalimbali kama vile mechi za timu ya taifa

Hiyo inanipa imani kuwa kuweka siasa pembeni, ule utanzania na hususan undug kati yetu bado upo..wala kwa mwonekano wa nje
Ni katika misngi hiyo ningetegemea kuwa wangesalimiana katika maana ya salamu za kindugu kuweka 'uadui' wa kisiasa pembeni...

Ila kama imetokea kama ilivoelezwa hapa, nadhani ni njia ya kutuonyesha kuwa suala la Buzwagi limemshika pabaya hadi nadhani uvumilivu unamshinda anajenga chuki....

Katika hili sina hakika kama nani kamkwepa mwenzie, labda tusubiri habari zaidi kama tulivoahidiwa...
 
Kilitime, what are you doing in JF kama SY ambaye ndo SI unit yako ya mtu makini haingii tena humu? kwa hiyo na wewe siyo mtu makini?

Get life!
 
Kwa mara nyingine tena viongozi wa upinzani na wa CCM wanagongana airport..(nyama za mashirika ya ndege???). Safari hii ni Mhe. Zitto akitokea Nairobi kwenye mkutano wa Raila Odinga na akagongana airport na baadhi ya mawaziri wa CCM ambao walikuja kumpokea Rais... Mawaziri wengine hawakuonesha husuda miongoni mwao ni mama Meghji... Mhe. Karamagi naye alikuwepo lakini alijifanya hakumuona Zitto na hivyo kuamua kumchunia kimya kimya... More details to come...
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alikutana uso kwa uso na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kusahau tofauti zao kwa muda.

'Mahasimu' hao walikutana jana uwanjani hapo na kusalimiana kwa kupeana mikono.Katika tukio la jana, Zitto alikutana na Karamagi uwanjani hapo alipokuwa akitokea nchini Kenya alikokwenda kuhudhuria kampeni za mgombea urais, Raila Odinga.

Karamagi alifika uwanjani hapo saa 8:00 mchana kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete aliyewasili uwanjani hapo kutoka ziarani nchini Marekani.

Karamagi aliyekuwa na mawaziri wengine na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika chumba cha watu mashuhuri (VIP), walipigwa na butwaa baada ya kumuona mbunge huyo akishuka ngazi akitokea katika sehemu ambayo wasafiri mashuhuri hutumia kupita.

Hali hiyo ilifanya karibu ukumbi mzima kukaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuangua kicheko baada ya Zitto ambaye inasadikiwa alisafiri katika ndege moja na Rais Kikwete, kumshika mkono Waziri Karamagi huku waandishi wakichukua picha za tukio hilo. Kitendo hicho kilimshawishi Waziri Karamagi pia kuangua kicheko.

Hata hivyo, mbunge huyo alikaa katika eneo hilo muda mfupi na baadaye aliondoka uwanjani na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa viongozi hao waliotaka kujua alikokuwa ametokea na sababu za kufika wakati huo ambao rais aliwasili.

Tukio hilo la kusalimiana limetokea ikiwa ni mara ya kwanza kwa 'mahasimu' hao kukutana tangu Zitto asimamishwe kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari, mwakani, baada ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama uliosainiwa na waziri huyo jijini London, Uingereza.

Zitto aliwasilisha hoja hiyo akitaka kuundwa Kamati Teule kuchunguza mazingira ya utiaji saini mkataba huo.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2182

Mkuu Mwanakijiji cheki tena na source yako....naona mamboni tofauti apo.....
 
Mzee anaelekea kubaya!!! Unapomshambulia mtu/kiongozi beyond mambo yanayohusu maslahi ya taifa,,, ni ushabiki ambao hauna uzalendo ambao tuna-claim hapa!

Naanza kukumbuka watu waliokuwa wakereketwa/wafukukutwa/ngangari/ngunguri!!! Hoja zao zilikuwa hazitofautiani sana na ujumbe wa thread hii!!!

No wonder watu makini kama Said Yakub siwasikii tena!!!

kabisa, hiki kitu hakimake sense ! swali zuri sana umeuliza Kilitime !
 
..ningemchunia!

..it's convinient,hasa ukizingatia hali ya hewa ilivyo angani!

..it's natural!

heheee, i wonder kama wangesalimia if that would make any difference ! labda jamaa wote (zitto, karamagi) ni freemansons hivyo walipeana ishara zao wenyewe waliokuwepo pale ( mwanakijiji hukuwepo ) labda hawakuelewa !
 
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alikutana uso kwa uso na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kusahau tofauti zao kwa muda.

'Mahasimu' hao walikutana jana uwanjani hapo na kusalimiana kwa kupeana mikono.Katika tukio la jana, Zitto alikutana na Karamagi uwanjani hapo alipokuwa akitokea nchini Kenya alikokwenda kuhudhuria kampeni za mgombea urais, Raila Odinga.

Karamagi alifika uwanjani hapo saa 8:00 mchana kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete aliyewasili uwanjani hapo kutoka ziarani nchini Marekani.

Karamagi aliyekuwa na mawaziri wengine na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika chumba cha watu mashuhuri (VIP), walipigwa na butwaa baada ya kumuona mbunge huyo akishuka ngazi akitokea katika sehemu ambayo wasafiri mashuhuri hutumia kupita.

Hali hiyo ilifanya karibu ukumbi mzima kukaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuangua kicheko baada ya Zitto ambaye inasadikiwa alisafiri katika ndege moja na Rais Kikwete, kumshika mkono Waziri Karamagi huku waandishi wakichukua picha za tukio hilo. Kitendo hicho kilimshawishi Waziri Karamagi pia kuangua kicheko.

Hata hivyo, mbunge huyo alikaa katika eneo hilo muda mfupi na baadaye aliondoka uwanjani na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa viongozi hao waliotaka kujua alikokuwa ametokea na sababu za kufika wakati huo ambao rais aliwasili.

Tukio hilo la kusalimiana limetokea ikiwa ni mara ya kwanza kwa 'mahasimu' hao kukutana tangu Zitto asimamishwe kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari, mwakani, baada ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama uliosainiwa na waziri huyo jijini London, Uingereza.

Zitto aliwasilisha hoja hiyo akitaka kuundwa Kamati Teule kuchunguza mazingira ya utiaji saini mkataba huo.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2182

Mkuu Mwanakijiji cheki tena na source yako....naona mamboni tofauti apo.....

Bora watu muanze kuamka hapa, maana msione mtu ana post nyingi mkataka kumuachia tu aseme kila kitu kirahisi na kikaenda tu, watu wote JF wawajibike sawa just like any other member ! Sishabikii ila hali ya hewa inabadirika JF which is good !
 
Kada Mpinzani, kwa jinsi Mkjj alivyoiweka hapa, huwezi kutumia maneno uyasemayo... Inaonekana una KINYONGO naye. Yeye ndiye wa kwanza kuweka kwamba ZK alikutana uso kwa uso na hao viongozi, sasa swala la kumchunia na kutomchunia lisiwe sababu ya kuanza kubadili mwelekeo... Kwa wanaoona hii si issue ya kujadiliwa hawaelewi nini maana ya HABARI... NAWAPONGEZA MWANANCHI KWA KULIONA HILO japo nadhani picha ya Kamaramagi na ZItto ingekua ni habari nzuri ya kuuza kwa wasomaji, lakini watu walibanwa kama Mtanzania walivyopewa "AGIZO toka JUU" wakaiweka picha ukurasa wa ndani wakati wao walitaka kuiweka ukurasa wa mbele. Kwa mkjj kuweka hapa alivunja ukimya na ndipo mjadala ukaanza na habari zaidi zitakuja kuhusiana na suala hilo. Kwa hiyo kwa wenye habari zaidi wazilete si kuanza kupondana. Habari huvunja habari nyingine
 
Kwa muda mrefu nimekuwa na wasiwasi juu ya michango ya wadau humu foramuni. Wachangiaji wameweka ushabiki mwingi sana mbele mbaya zaidi bila hata kufikiria vizuri. Ahsanteni wale mlio,uona yule aliyejipa jina laa uzee wa kijijini jinsi anavyotumika kueneza sumu hii ya chuki kwa watanzania.
Ndio kwanza nimetoka kuangalia picha iliyopo kwenye gazeti la Mtanzania, bashasha iliokuwepo kwenye wajihi wa waziri Nazir alipokutana na ndugu Zuberi haionyeshi chuki hiyo iliyoelezwa na Mwanakijiji, inawezekana mwanakijiji hakuwepo lakini cjanzo chake kilikuwa ni kibovu mno.
Kingwele wa Kingwele.
 
Bora watu muanze kuamka hapa, maana msione mtu ana post nyingi mkataka kumuachia tu aseme kila kitu kirahisi na kikaenda tu, watu wote JF wawajibike sawa just like any other member ! Sishabikii ila hali ya hewa inabadirika JF which is good !

Heshima ya JF ipo palepale,na hakuna anayetegemea mawazo ya mtu hapa,wewe Kada Mpinzania naona una chuki binafsi na Mwanakijiji.Hali ya hewa ya JF bado haijabadirika kama unavyodai,ila imebadirika kwa kuogopwa na mafisadi,kutoa mawazo makini,kuelimisha jamii,sasa wewe sijui unaposema hali imebadirika unamaanisha nini?Sidhani kama tutafika endapo tutakalia umbea badala ya kuongelea masuala ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom