Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 787
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alikutana uso kwa uso na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na kusahau tofauti zao kwa muda.
'Mahasimu' hao walikutana jana uwanjani hapo na kusalimiana kwa kupeana mikono.Katika tukio la jana, Zitto alikutana na Karamagi uwanjani hapo alipokuwa akitokea nchini Kenya alikokwenda kuhudhuria kampeni za mgombea urais, Raila Odinga.
Karamagi alifika uwanjani hapo saa 8:00 mchana kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete aliyewasili uwanjani hapo kutoka ziarani nchini Marekani.
Karamagi aliyekuwa na mawaziri wengine na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika chumba cha watu mashuhuri (VIP), walipigwa na butwaa baada ya kumuona mbunge huyo akishuka ngazi akitokea katika sehemu ambayo wasafiri mashuhuri hutumia kupita.
Hali hiyo ilifanya karibu ukumbi mzima kukaa kimya kwa sekunde kadhaa kabla ya kuangua kicheko baada ya Zitto ambaye inasadikiwa alisafiri katika ndege moja na Rais Kikwete, kumshika mkono Waziri Karamagi huku waandishi wakichukua picha za tukio hilo. Kitendo hicho kilimshawishi Waziri Karamagi pia kuangua kicheko.
Hata hivyo, mbunge huyo alikaa katika eneo hilo muda mfupi na baadaye aliondoka uwanjani na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa viongozi hao waliotaka kujua alikokuwa ametokea na sababu za kufika wakati huo ambao rais aliwasili.
Tukio hilo la kusalimiana limetokea ikiwa ni mara ya kwanza kwa 'mahasimu' hao kukutana tangu Zitto asimamishwe kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari, mwakani, baada ya kuwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, wilayani Kahama uliosainiwa na waziri huyo jijini London, Uingereza.
Zitto aliwasilisha hoja hiyo akitaka kuundwa Kamati Teule kuchunguza mazingira ya utiaji saini mkataba huo.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2182
Mkuu Mwanakijiji cheki tena na source yako....naona mamboni tofauti apo.....
Hoja yangu imejibiwa, tufunge mjadala!