Airport Dar na Masanduku/mizigo yetu

Futota

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
521
87
Jamani haka ka mchezo ka kufungua masanduku/mizigo yetu airport Dar na kutuibia, kipindi kidogo cha nyuma tulipumzika. Sasa naona tabia hii imerudi tena. Kama wasipoiba kitu basi wanapaka sijui kemikali gani katika viatu nk. ambayo inaweka madoa yasitoka. Jamani hii ni nini lakini? Leteni experiences zenu, mtu ufanye nini au uripoti wapi ukifikwa na hivi?
 
ni kweli mkuu,,nakumbuka 2010 mzee wangu aliibiwa saa ya mkononi hapo jkia ambayo ilikuwa 2000 usd baada ya wao kumlazimisha aiweke kwenye bag,,it was a sad story,,,aliniita nikafuatilia lakini sikupata majibu sahihi,,
 
Sina uhakika na ukweli ya usemayo. Umesema tulete uzoefu wetu. Wa kwangu ni kama ifuatavyo:

Katika kipidi cha miaka ishirini iliyopita, nimekuwa nawasili JNIA kila Novemba na kuondokea hapo hapo kila Februari. Nimewahi kuibiwa mara moja (video camera), lakini sina uhakika iliibiwa Dar. Hiyo ilikuwa miaka minane iliyopita. Inawezekana sanduku yangu ilifunguliwa Singapore au Joberg vile vile. Sijaibiwa zaidi ya hapo.

Leta uthibitisho kwamba JNIA wanafungua sanduku na kuiba.
 
Ndio maana nikasema miaka ya nyuma tulipumzika kidogo na udokozi hapo JNIA. Mimi nafanya kazi nchi jirani na husafiri kurudi Bongo zaidi ya mara 3 kwa mwaka, na kwa mwaka huu 2013 nimeshapita hapo mara 6 wakati wakuingia na kutoka, Na mara 2 wakati wa kutoka sanduku langu limefunguliwa na vitu kuchukuliwa. Mara ya kwanza Blazer yangu ya bei ghali kidogo niliyoivaa mkutanoni ilibiwa hapo JNIA. Shida safari zote nikiibiwa nakuwa nimerudi kazini nje ya nchi hivyo vigumu kufuatilia. Na ndio maana nimekuja na mada hii, labda upo utaratibu wa mtu kupeleka malalamiko

Sina uhakika na ukweli ya usemayo. Umesema tulete uzoefu wetu. Wa kwangu ni kama ifuatavyo:

Katika kipidi cha miaka ishirini iliyopita, nimekuwa nawasili JNIA kila Novemba na kuondokea hapo hapo kila Februari. Nimewahi kuibiwa mara moja (video camera), lakini sina uhakika iliibiwa Dar. Hiyo ilikuwa miaka minane iliyopita. Inawezekana sanduku yangu ilifunguliwa Singapore au Joberg vile vile. Sijaibiwa zaidi ya hapo.

Leta uthibitisho kwamba JNIA wanafungua sanduku na kuiba.
 
Hata mimi nazungumzia miaka ya sasa. Naendelea kupita JNIA kila mwaka. Sisemi hakuna uwezekano wa watu pale kuiba, ila tuwe na uhakika kabla hatujawapa sifa mbaya. Unajuaje sanduku lako halifunguliwi na kuibiwa kwenye airport ya nchi jirani? Elaborate on this.
 
Mimi sijawahi kuibiwa nimepita zaidi ya mara 25 hapo,ila nakereka sana na tabia za kufungua mabegi au masanduku,huku ughaibuni tunapita air port kubwa zenye kila aina ya mitambo hawafungui vp nafika home nawaambia kabisa kuna nini lakini mpaka wafungue ndani wanakera sana,

Wife alisafiri mwezi feb hapo air port anadai kuna vitu vyake vimepotea hapo kwa sababu walifungua bag yake wakati anaondoka kweli air port ya Dar ni kero sana
 
Sina uhakika na ukweli ya usemayo. Umesema tulete uzoefu wetu. Wa kwangu ni kama ifuatavyo:

Katika kipidi cha miaka ishirini iliyopita, nimekuwa nawasili JNIA kila Novemba na kuondokea hapo hapo kila Februari. Nimewahi kuibiwa mara moja (video camera), lakini sina uhakika iliibiwa Dar. Hiyo ilikuwa miaka minane iliyopita. Inawezekana sanduku yangu ilifunguliwa Singapore au Joberg vile vile. Sijaibiwa zaidi ya hapo.

Leta uthibitisho kwamba JNIA wanafungua sanduku na kuiba.

Mkuu hilo usipinge, niko maeneo ya Buguruni daily vijana wanakuja na simu, batteries, digital cameras,laptops,Ipads e.t.c na wanakwambia kuna washkaji wao wapo JNIA ndo wanawapa wauze, it might be true mkuu....
 
Sina uhakika na ukweli ya usemayo. Umesema tulete uzoefu wetu. Wa kwangu ni kama ifuatavyo:

Katika kipidi cha miaka ishirini iliyopita, nimekuwa nawasili JNIA kila Novemba na kuondokea hapo hapo kila Februari. Nimewahi kuibiwa mara moja (video camera), lakini sina uhakika iliibiwa Dar. Hiyo ilikuwa miaka minane iliyopita. Inawezekana sanduku yangu ilifunguliwa Singapore au Joberg vile vile. Sijaibiwa zaidi ya hapo.

Leta uthibitisho kwamba JNIA wanafungua sanduku na kuiba.

Ondoa na yote unayosema bado sikuamini hata. Inaelekea wewe ni mfanyakazi wa JNIA. Pale uwanjani ni wezi wakubwa na ni mtandao wa hali ya juu kwani nahisi hata vingozi wanahusika maana wanajuwa wizi wa pale lakini hawafanyi kitu, hata ulalamikaje nothing happens.
 
sina uhakika na ukweli ya usemayo. Umesema tulete uzoefu wetu. Wa kwangu ni kama ifuatavyo:

Katika kipidi cha miaka ishirini iliyopita, nimekuwa nawasili jnia kila novemba na kuondokea hapo hapo kila februari. Nimewahi kuibiwa mara moja (video camera), lakini sina uhakika iliibiwa dar. Hiyo ilikuwa miaka minane iliyopita. Inawezekana sanduku yangu ilifunguliwa singapore au joberg vile vile. Sijaibiwa zaidi ya hapo.

Leta uthibitisho kwamba jnia wanafungua sanduku na kuiba.

march 2013 niliibiwa hapohapo... Simu 3 , saa mpya kabisa..... Ni wezi balaa ... Hapo airport
 
Huu mchezo nishasikia unafanyika sana hapo JKNIA yaani kama una bag la ku check in jamaa lazima walifungue halafu kama kuna aina yeyote ya delay na cancellation basi hapo maumivu yanakuwa makubwa zaidi..
 
aaah huu uwanja wizi ni kawaida yaani ukiweka begi lako unakaa kwa hofu hofu kama vile unaenda kigoma
 
Mimi sijawahi kuibiwa nimepita zaidi ya mara 25 hapo,ila nakereka sana na tabia za kufungua mabegi au masanduku,huku ughaibuni tunapita air port kubwa zenye kila aina ya mitambo hawafungui vp nafika home nawaambia kabisa kuna nini lakini mpaka wafungue ndani wanakera sana,

Wife alisafiri mwezi feb hapo air port anadai kuna vitu vyake vimepotea hapo kwa sababu walifungua bag yake wakati anaondoka kweli air port ya Dar ni kero sana
Na ukigoma kufungua wanadai umebeba unga.
 
Back
Top Bottom