AirArabia Sasa kutua Nairobi...Tanzania vipi?

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
43
Wadau kuna taarifa ya kuwa Shirika la Ndege la AirArabia ya Serikali ya Sharjah ya UAE, itaanza safari zake Dubai/Sharjah-Nairobi soon..

tetes zilizopo ni kuwa Nauli itakuwa chini ya dola 300 (dh1000)

Hili shirika ndio shiriko lenye viwango nafuu vya usafiri kwa sehem kubwa za Middle East, Africa na Asia, wao principal kubwa wanayotumia ni kuwa Chakula hakiwi included ktk overal fair...

Kwa utaratibu huu Jiji la Nairobi litazidi kufurika na kuna uwezekano wafanya biashara wadogo waendao dubai huenda waka opt hii njia ya kwenda Nairobi, then wakirudi wanaweza rudi kwa precision au kwa basi za kuja DSM...

napenda kuwauliza wadau wenzangu..vipi Bongo tutanufaika na cheapest flight kama Hizi?....je hapa hakuna ufisadi wa 10% ya kuwaleta serious investor? mwenye pua za kunusa anaweza kuteletea nyeti zaid!!!
 
Hii ni kama Ryanair ya kiarabu.

Kwanini wasiruke kuja kwetu Tanga jamani? au ndio mmetusahau kabisa toka Tanga [jiji la viwanda lilivyofilisika?
 
Hii ni biashara na hamna cha ufisadi. Hauwezi kumlazimisha mwekezaji awekeze kama anaona hamna maslahi! Huyo AirArabia akiona kuna maslahi atajimwaga wala hamna haja ya kumbembeleza!
 
Nasikia ukitaka kwenda nchi yoyote Afrika from Tanzania, lazima upitie Afrika ya Kusini, Kenya au Ethiopia. Ukilinganisha na mataifa mengine ya Africa, sisi tuko mkiani au "average"?




.
 
Umechelewa

EMIRATES wamepiga mikwara serikalini kuwa hiyo ndege ikija Dar wanasusa route ya Dar-Dubai

kama kuna mwenye info tofauti basi naamini utaletewa
 
Back
Top Bottom