Air Tanzania new logo: I think we need to write to CEO

david mattaka hana tofauti na jakaya mrisho kikwete,hawa ni wale wale punda na masikio yake,kweli sisi watanzania ni mahodari wa kusahau historia,basi ni waambieni kwa 2010 jk atapata zaidi ya asilimia 90 katika uchaguzi.
mungu atupe uzima.
 
hahahahahahahah kama nisiku nimecheka ni leo maana hapa ni kukopi na pest tuu kuanzia family level hadi national level. Yaani sina mbavu mkuu hiii ni kwali kwa kweli au ndio tricle down effect yenyewe?. Ila kweli blog zetu zinatabia ya kukopi na kupest kuanzia maandishi hadi picha bila ya kuacknowledge.

Kwa hiyo jamani tusiwalaumu hawa jamaa wa LOGO maana hili ni tatizo la kitaifa.

Mataka hujakosea bwana kukopi
 
Asante wote mliochangia.

Kuna walioona umuhimu wa kuwa na unique identity.
Kuna walioona hata ukiwa na logo ya (kijinga?) ni sawa ilimradi unapata faida.
Na kuna waliotaka kupanua wigo na kuanza kumshambulia CEO kutokana na historia yake.

Mwisho wa yote nimeona nitumie njia ya kistaarabu ya kumtumia barua, bahati mbaya e-mail pekee niliyonayo ni bookings@airtanzania.com (ajabu www.airtanzania.co.tz ambayo ina identity zaidi ya Tanzania ni mali ya africaonline!)

Naituma barua kwenye hiyo e-mail lakini kama kuna mwenye his personal e-mail tafadhali saidia kufikisha ujumbe. Nime"attach" barua hapa.

Yote haya ni mawazo yangu tu...yanaweza kuwa yako sahihi au la, au naweza kusahihishwa na kuelezewa zaidi. Kwa mimi nimemaliza dukuduku langu.
 

Attachments

  • Air Tanzania Logo.pdf
    149.3 KB · Views: 126
Back
Top Bottom