Jaji Tz
Member
- Feb 16, 2015
- 33
- 19
The Diplomat
Air Tanzania (ATCL) ni shirika la umma na limekodishiwa ndege na serikali kutoa huduma kwa wananchi ,na kwa mara kadhaa hasa kipindi hiki cha corona halijatengeneza faida shirika kama shirika lakini faida ya ndege hizi ni kubwa hasa kwenye sekta nyingine za uchumi ikiwemo biashara na kurahisisha mzunguko wa watu na bidhaa pamoja na kuongeza utalii kubwa zaidi ni kuitangaza nchi yetu kimataifa (National image branding ) ndege zetu zinaporuka mataifa mbalimbali Duniani.
Lakini pia kufufuliwa kwa shirika la ATCL (Air Tanzania) imeongeza fursa za ajira kwa watanzania ambapo kabla ya shirika kufufuliwa kulikuwa na watumishi 171 na sasa watumishi 540 wameajiriwa na na inatarajiwa kuongezwa ambapo marubani watatu wanategemewa kuongezwa katika shirika hili.
Sambamba na Mafanikio hayo Serikali imedhamiria pamoja na ununuzi wa ndege nyingine kununua ndege moja kubwa ya mizigo itakayosafirisha bidhaa zinazoharibika kwa haraka hasa bidhaa za kilimo ikiwemo maua ,mbogamboga na matunda na hii ni kutokana na uzalishaji mkubwa wa bidhaa hizo hapa nchini ,hii italeta tija kwenye sekta ya kilimo na ufugaji na kuongeza biashara za nje (Export) na hivyo kuongeza wigo wa mapato na tija kwa sisi watanzania.
#TanzaniaYetu
#KaziIendeleee