Aipasua Maiti ya Baba Yake Kwaajili ya Wanafunzi Wake

ifolako

Member
Nov 8, 2010
98
0
5129446.jpg

Monday, November 15, 2010 2:05 AM
Kwa mara ya kwanza katika historia ya udaktari duniani, daktari mmoja nchini India ameweza kuzizuia hisia zake kwa kuitumbua na kuvichanganua viungo vya maiti ya baba yake wakati akiwafundisha wanafunzi wake somo la elimu ya mwili na viungo vya binadamu.Dr Mahantesh Ramannavar, profesa wa elimu ya mwili na viungo vya binadamu (anatomy) katika chuo kikuu cha KLE University katika mji wa Belgaum, Karnataka nchini India, aliipasua maiti ya baba yake jumamosi na kuitumia kuwafundishia wanafunzi wake.

Tukio hilo lilivuta waandishi wa habari wengi toka sehemu mbalimbali duniani huku baadhi ya televisheni za India zikirusha LIVE tukio hilo.

Dr Mahantesh akiwa na wanafunzi wake aliingia kwenye chumba cha upasuaji kwenye majira ya saa 10 alasiri ambapo mwili wa baba yake ambaye naye alikuwa daktari Dr Basavanneppa ulikuwa umeandaliwa kwaajili ya somo hilo.

Enzi za uhai wake, Dr Basavanneppa aliyefariki akiwa na umri wa miaka 89, aliandika wosia wa kumtaka mtoto wake autumie mwili wake kuwafundishia wanafunzi wake.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya udaktari duniani, mtoto kuipasua maiti ya baba yake na kuitumia kuwafundishia wanafunzi wake. Dr William Harvey wa London, Uingereza ndiye aliyekuwa akijulikana kwa kuipasua maiti ya dada yake.

Mama yake Dr Mahantesh pamoja na kaka zake na dada zake na watoto wao, nao walikuwepo kushuhudia tukio hilo la aina yake.

Akiongea baada ya tukio hilo Dr Mahantesh alisema kuwa ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kufuata wosia wa baba yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom