Aiomba serikali imkamate aliyemkata nyeti! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aiomba serikali imkamate aliyemkata nyeti!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ehud, Mar 22, 2011.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Babu Abdallah Kifo (67) amemuomba mkuu wa nchi na serikali yake imsaidie kumsaka kijana aliyemkata sehemu zake nyeti ili aweze kumfikisha kwenye mamlaka husika.

  Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Bw. Seleman Jafo juzi, Babu huyo alisema kijana aliyemfanyia unyama huo hujitokeza kijijini hapo mida ya night na kujidai...huku viongozi wa kijiji hicho wakiwa wakimya kwa kushindwa kumchukulia hatua stahili.

  "Mtuhumiwa huyu akionekana kijijini hapa ananitishia kuniua wala sijui ni kwa nini hakamatwi kupelekwa polisi," alisema Bw. Kifo.

  Bw. Kifo alipatwa na mkasa huo Oktoba 22, mwaka jana alipovamiwa nyumbani kwake na vijana watatu waliomkaba na kumkata nyeti zake.

  Baada ya tukio hilo alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) ambako alilazwa na kutibiwa ambako sasa anaendelea vizuri lakini amekuwa mlemavu.

  Bw. Kifo anasema chanzo cha mkasa huo ni fedha alizokuwa anadaiwa sh. 450,000 alizokopa kwa mtu mmoja lakini alishindwa kuzirudisha kwa muda waliokubaliana, hivyo kumnyang'anya mabati 20.

  Alisema alilipa sh. 300,000 na kubakiza deni la sh. 150,000, hivyo kutaka arudishiwe mabati yake ambayo aligoma kuyatoa.

  Bw. Kifo alisema kulitokea mtafaruku mkubwa uliosababisha mtu huyo awalipe fedha vijana watatu ili wamkate nyeti kumkomoa.


  Aiomba serikali imkamate aliyemkata nyeti!
   
Loading...