Aina za wanawake

Man Mudi

Senior Member
Oct 13, 2014
159
113
AINA NNE YA WAKE.

Katika ndoa mwanaume hukutakana na Aina nne za wake. Na Aina hizo zinaathari katika ndoa yake kwa namna moja au nyingine. Na aina hizo ni.

1. Mke penzi kubwa.

Mke penzi kubwa ni mke ambaye ana mapenzi makubwa sana na mume wake. Na huyuko tayari kujiingiza kwenye pirika zozote za kutafuta maisha Bali hutosheka na kile akileta mume wake. Na hutosheka kuilea familia yake na mume wake.

2. Mke penzi kubwa na shughuli.

Mke wa namna hi ni mke ambaye ana mapenzi makubwa na mume wake na pia anapenda kujishughulisha na kutafuta kipato imma kufanya biashara au kazi. Lakini mapenzi yake kwa mume wake ni makubwa zaidi kuliko mapenzi ya shughuli hizo za utafutaji. Na yuko tayari kuziacha shughuli hizo kwa ajili ya utii kwa mume wake.

3. Mke shughuli na penzi.

Mke wa namna hii ni mke mwenye mapenzi na shughuli ya kumuingizia kipato kuliko ana alivyo na mapenzi na mume wake. Na hata akitakiwa ayape mapenzi hayo asilimia kubwa basi asilimia 51 itaenda kwenye kazi asilimia 49 itaenda kwa mume. Ila mume akiwa na kipato kikubwa basi hupata asilimia nyingi ya penzi la mume huyo kuliko shughuli za kuingiza kipato.

4. Mke shughuli.

Mke wa namna hii ni mke ambaye kuolewa kwake ni kama Utaratibu tu wa maisha lakini mapenzi yake makubwa yako kwenye shuguliza za utafutaji imma ni biashara au kazi zake. Ama suala la kipi akipendacho zaidi kati ya mume wake au shughuli zake za utafutaji majibu yake yako wazi shuguli kwake ndio kila kitu. Mume ni ziada tu katika maisha yake. Hata asipokuwepo sawa tu kwake.

Wake na pesa.

Ama kuhusu wake na pesa pia kuna makundi manne ya wake kuhusu pesa. Na makundi hayo ni kama ifiatavyo.

1. Kuna wake pesa kwao sio kipaumbele kabisa katika maisha ya ndoa wana moyo wa kukinai kwa kile kilichopo. Kwao heshima, thamani na mapenzi ya dhati ndio kikomo cha furaha yao katika ndoa.

2. Kuna wake ambao pesa na penzi hutaka viwe Sawa, pesa ziwepo na mapenzi yawepo. Kimoja kikipungua basi huiona ndoa kwake haijamkalia vizuri.

3. Kuna wake ambao pesa kwanza ama kuhusu mapenzi wanasema wamewaachia njiwa na mumewe wake. Pesa ikiwepo ndio huzalisha penzi, hakuna pesa bando la penzi linasoma sifuri. Kwa hivyo akiwa ajishughulishi na utafutaji matumizi yake utafurahi na roho yako hajui mume kukosa. Na kama ajishughulisha akitoa hata pesa ya kiberiti mume atailipa. Na Hawa wa namna hii hufikia kumuua mume abaki na Mali ikiwa mume ni tajiri. Au kazipata pesa wakiwa pamoja.

4. Kuna wake ambao ni penzi na pesa. Hawa ni wale wake ambao ni watafutaji sana katika biashara na kazi zao. Lakini pesa zao ni kwa ajili ya kuboresha penzi lake na mume wake kwa kumsaidia pale alipokwama, kuleta maendeleo katika familia...

Na tabia hizo huathiriwa na malezi, elimu, tamaduni, uchamungu na kuiga..... Na hubadilika kutokana na mambo hayo hayo. Na kubadilika kwake kutokana upande mzuri kwenda mbaya ni Ukosefu wa ufahamu mzuri na uchamungu na kubadilika kwake kutoka katika sehemu mbaya Kuja nzuri ni baada ya kupata ufahamu mzuri na uchamungu.
 
Hapa ndio ndio unaona mtihani kwetu sisi wanaume ktk kupata mke sahihi huwa ni changamoto sana dada zetu mna jambo la kijifunza
 
Back
Top Bottom