Aina za biashara za reja reja zinazoweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo ama na mtu hata mwenye kipato cha chini

Livingson1

Member
Jul 13, 2021
30
26
1. Genge la mboga mboga na matunda. Hii ni biashara ambayo mtu ataweza kuanzisha kwa mtaji mdogo kabisa na ikampatia kipato cha kujiendesha kimaisha ama kutunza familia, kulipa kodi ya pango n.k

2. Duka la reja reja. Hii ni aina nyingine ya biashara ambayo utaweka vitu vya matumizi ya kila siku mfano sabuni, sukari, kiberiti, mchele, unga, n.k. hii ina tija maana muuzaji anauza vitu ambavyo ni matumizi ya kila siku ya nyumbani

3.Biashara ya kuuza miwa. Hii pia mtaji wake ni mdogo kabisa. Hapa kinachohitajika ni mkokoteni mdogo wa chuma, ndoo safi, vifuko vya kuwekea baada ya kuchonga, kisu na sehemu ya kuwekea uchafu ili kulinda mazingira

4. Biashara ya juice ya matunda au miwa. Hii hufanyika katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vile sokoni, stand, vyuoni, hospital n.k

5.kuziba pancha. Kwenye matairi ya boda, bajaji, gari, baiskeli n.k

6. Tuition centre. Hii ni kwa wale wenye taaluma mfano waalimu wanaweza wakaungana wakaunganisha nguvu kiuchumi na kufungua tuition centre

7. Stationary kwaajili ya kuchapisha, kutoa kopi, binding, lamination ,n.k hii pia inakuwa kwenye mikusanyiko kama shuleni, vyuoni, sokoni, pembezoni mwa ofisi za serikali za mtaa n.k

8. Car washing. Hapa kikubwa kuwa na chanzo cha maji, pump na baadhi ya vifaa vya kuoshea gari

9. Kuchoma mandazi ama chapati. Kila asubuhi watu huhitaji vitafunwa hivi kwaajili ya kufungua kinywa hivyo ni biashara nzuri, cha kuzingatia usafi na ubora

10. Kuchoma/ kukaanga chips. Chipsi hupendwa na watu wengi hivyo ni biashara nzuri kwa mtaji mdogo

11. Kutengeneza keki. Keki kwenye harusi, birthday, sherehe ya komunio, kipaimara n.k

12. Kutengeneza biryani. Mfano mudi mabiryani anavyopiga pesa sasa

13. Duka la nguo za mtumba ama viatu vya mtumba, mabegi n.k

14. Saloon. Hapa inaweza kuwa saloon ya wanaume ama saloon ya wanawake.

Na kuna nyingine nyingi ambazo sijazitaja hapa

ANZA NA KIDOGO ULICHONACHO
JIWEKEE MALENGO KILA MWAKA NA HAKIKISHA UMEFIKIA MALENGO YAKO

CHANGAMOTO ZIPO LAKINI CHANGAMOTO ZINATOKEA KUKUONYESHA KUWA UNAKOSEA ILI UBADILISHE PLAN KUFIKIA MALENGO 🤔
 
Ni mtazamo, unaeza ongeza chache hapo
 
Back
Top Bottom