Aina ya Virusi vya Corona vya India na Uingereza vyagunduliwa Afrika Kusini

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Aina mpya ya Virusi vya COVID19 kutoka India na Uingereza imegunduliwa nchini Afrika Kusini, Wizara ya Afya imeeleza.

Visa 11 vya maambukizi ya aina ya Virusi vya B.1.1.7 (Uingereza) na visa 4 vya B.1.617.2 (India) vimegunduliwa katika majimbo ya Gauteng na Kwazulu-Natal, na waathirika wamekuwa na historia ya kusafiri nchini India na Bahrain.

Waziri wa Afya amebainisha kuwa virusi vya B.1.1.7 vimegundulika baada ya kupima sampuli za wakazi, ikimaanisha kuwa vimekwishaanza kusambaa kwa wakazi.

Taasisi ya Kupambana na Magonjwa ya Afrika Kusini (NICD) imesema kuwa inaelekeza nguvu katika kuelewa madhara ya aina hiyo mpya ya virusi kwa wakazi wa Afrika Kusini na kupambana navyo.

Afrika Kusini imerekodi visa zaidi ya milioni 1.5 vya maambukizi ya COVID-19 na vifo 54,724.

Chanzo: Xinhua
 
Back
Top Bottom