Aina ya Sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa vinaweza kuwa sumu

Issa SLuu

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
2,303
1,801
Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu.

Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine.

Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula.

Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu.

Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi .

Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu.

Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora.

Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote.

Samaki na Maziwa
Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shida baadaye.

Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa. Huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.

Maji ya limao na Maziwa
Maziwa na limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika.

Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga na Mafuta ya mzeituni
CHANZO CHA PICHA,OTHER
Karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.

Pia karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile Karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.

Kwa mafuta ya mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.

Dawa pamoja na sharubati ya limao

Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.

Ameongeza kwa kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa ni hatari.

Nyama na mayai mabichi
Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu.

Inaweza kuwa sumu kwa wengine, zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.

Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.

Mtaalamu anasema kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio hujenga mwili.

"Mayai mabichi sio ya kuyaamini," Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba Haruna.

Wataalamu wanashauri watu kula kile wanajua kitakuwa na faida na haitawasababishia matatizo yoyote.

Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara.

Kuna aina nyingi sana ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara.

Mtu anapaswa kuwa mwangalifu katika uchaguzi wa vyakula ni vyema aweke vyeme virutubisho na kuepuka kuvichanganya.

COPY AND PASTE

BBCswahili
 
Mkuu sisi wapishi tunapika samaki na maziwa kila siku na hakuna shida wala tatizo lolote,Nyama mbichi na mayai tunatumia kwenye kutengenez ea burger,na hakuna shida yyt ,labda maziwa na ndimu hapo sawa,maziwa na ndimu tunatumia kutengenezea Pannil,na watu wanakula fanya utafiti tena
 
Yai bichi mbona ni dawa unakunywa zima? Nazungumzia yai lile yai la kuku wa kienyeji na siyo kuku hawa wa umeme.Pia sumu nyengine ni kulipika nanasi hapo umetengeneza sumu.
 
Kuna maneno kwamba kula tango na asali kwa wakati mmoja ni sumu. Kuna mtu aliniambia mda mfupi baada ya kuona nimetoka kulamba asali halafu nikawa nakula tango, sasa nashangaa imekuaje bado nasavaivu au itakua ni sumu inayoua taratibu baada ya mda mrefu?
 
Asali ukiilamba mwilini kinachoingia kwenye damu sucrose kama ile ya kwenye muwa, ambayo baadae inakuwa glucose. Tango sehemu kubwa ni maji na rouphage au kamba kamba, hizo fix tuu. Ni sawa na ile ya mtindi na asali oooh ukila sumu na unakufa, mimi ndiyo kila nikipiga mtindi naweka kijiko cha asali.
 
Mkuu sisi wapishi tunapika samaki na maziwa kila siku na hakuna shida wala tatizo lolote,Nyama mbichi na mayai tunatumia kwenye kutengenez ea burger,na hakuna shida yyt ,labda maziwa na ndimu hapo sawa,maziwa na ndimu tunatumia kutengenezea Pannil,na watu wanakula fanya utafiti tena
Mkuu shida haitokei. Leo Ni baadabya miaka na tatizo lenyewe Ni UGONJWA wa MBRANGA (VITILIGO) Jusababish2a na kula Samaki pamoja na maziwa kwa wakati mmoja
 
Maharagwe, mayai,mahindi, viazi,
Huu mchanganyiko ukijamba ni zaidi Mass destruction weapon
 
Eti samaki na maziwa! Usukumani tunapiga ugali kwa samaki tunasukumizia na maziwa, mbona hatujaathirika na chochote!
 
Aina ya sita ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu.

Kila binadamu ana kile alichojaaliwa na Mungu. Siku zote anachoamua mmoja kula huenda kikawa sumu kwa mwingine.

Chakula anachokula mtu kinaenda sanjari na hali ya kiafya. Wengine huumwa hadi kusababisha kupoteza uhai na hii ni baada tu ya kupendelea kuchanganya chakula.

Mtu mmoja anaweza kula sawa na kwa urahisi, ila kwa mwingine kikageuka sumu.

Hali hii huchochewa zaidi na matokeo ya baadae pale unaposhindwa kuweka mchanganyiko sahihi na wenye afya zaidi .

Kila aina chakula ina faida zake, ila kinapochanganywa kinaweza kusababisha shida kwa mtu.

Kwa watu ambao wanataka kuchanganya lishe ili kupunguza unene na vichocheo vyake ni vyema kushauriana na wataalamu jinsi ya kupanga lishe bora.

Mtaalam wa lishe wa Nigeria Habiba Haruna ameiambia BBC kuhusu aina sita za chakula ambazo zinaweza kuwa sumu kwa mtu yeyote.

Samaki na Maziwa
Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho lukuki na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi na hii inaweza kuleta shida baadaye.

Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa. Huweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha.

Maji ya limao na Maziwa
Maziwa na limao huwa haviwezi kukaa sehemu moja kwani vikichanganywa lazima maziwa yaweze kukatika.

Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengenezea sumu, vilevile yanaweza kuleta shida katika moyo.

Karanga na Mafuta ya mzeituni
CHANZO CHA PICHA,OTHER
Karanga ina umuhimu mkubwa sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi sana.

Pia karanga ina kiwango kikubwa sana cha protini na wanga, vilevile Karanga ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe, haswa kwa wale ambao wanataka kupunguza uzito.

Kwa mafuta ya mzeituni yanamsaada mkubwa pia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa, lakini mchanganyiko wa mafuta hayo na karanga yanaleta shida ila inashauriwa kutumika pale moja inapokosekana lakini sio kwa pamoja.

Dawa pamoja na sharubati ya limao
Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kuwa kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.

Ameongeza kwa kusema kuwa limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa ni hatari.

Nyama na mayai mabichi
Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu.

Inaweza kuwa sumu kwa wengine, zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.

Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.

Mtaalamu anasema kuwa mayai mabichi hayana virutubisho kwenye mwili wa binadamu, yakiwa bado kwenye hali hiyo hayapaswi kuliwa mpaka pale yatakapochemshwa au kukaangwa ndio hujenga mwili.

"Mayai mabichi sio ya kuyaamini," Anasema Mtaalamu wa chakula kutoka Nigeria, Habiba Haruna.

Wataalamu wanashauri watu kula kile wanajua kitakuwa na faida na haitawasababishia matatizo yoyote.

Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida kwa wengine lakini pia kunaweza kuwa na madhara.

Kuna aina nyingi sana ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara.

Mtu anapaswa kuwa mwangalifu katika uchaguzi wa vyakula ni vyema aweke vyeme virutubisho na kuepuka kuvichanganya.

COPY AND PASTE

BBCswahili
Dawa pamoja na sharubati ya limao
Sema, dawa pamoja na sharubati yoyote ile, si lazima iwe ya limao
tu.
Chukua vidonge kisha meza kwa kuvisukumiza na sharubati. Wewee, mziki wake utauona.
Nilishawahi shuhudia hii kitu toka kwa rafiki yangu!
 
kwa bibi ilikuwa Kila wakipika kitoweo chochote isipokuwa nyama mbichi ilikuwa ni lazima waweke maziwa kwenye kitoweo hicho, tumekula sana mchemusho wa samaki ulioungwa na maziwa kwa ugali na hakuna kibaya kilichotupata
 
Mkuu sisi wapishi tunapika samaki na maziwa kila siku na hakuna shida wala tatizo lolote,Nyama mbichi na mayai tunatumia kwenye kutengenez ea burger,na hakuna shida yyt ,labda maziwa na ndimu hapo sawa,maziwa na ndimu tunatumia kutengenezea Pannil,na watu wanakula fanya utafiti tena
Naungana na wewe maana ndimu tofauti na kukata maziwa sioni ishu nyingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom