Aina nne za Hati za Ukaguzi zinazotolewa na CAG

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Baada ya kukamilisha ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali hutoa Hati ya Ukaguzi kwa kila taasisi ya umma aliyoikagua. Hati ya Ukaguzi ni maoni ya Mkaguzi yatokanayo na ukaguzi alioufanya kwenye hesabu za taasisi au mamlaka yoyote ya umma.

Hati ya Ukaguzi hutolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuonesha ni kwa kiwango gani hesabu alizozikagua zimeandaliwa kwa kuzingatia viwango wya kimataifa vya uandaaji hesabu katika sekta ya umma (IPSASs) pamoja na matamko yanayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu a Wakaguzi Hesabu (NBAA) na Sheria za nchi husika.

Katika ukaguzi wake, CAG hutoa aina nne za Hati za Ukaguzi kama ifuatavyo; Hati Inayoridhisha, Hati Yenye shaka, Hati Mbaya na kushindwa kutoa Maoni/Hati. Mkaguzi anapotoa hati ya ukaguzi inayoridhisha, haimaanishi kuwa taasisi iliyokaguliwa haina dosari yoyote.

Hii ni kwa sababu ukaguzi hufanywa kwa kuchagua miamala michache (sample transactions) na siyo miamala yote (all transactions) iliyofanywa na taasisi husika.
 
Back
Top Bottom