Aina mpya ya wizi imeingia jijini

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
4,712
5,368
Habari ya kweli iliyotokea siku chache zilizopita.

Kuna dada mmoja anasoma chuo fulani Buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa Lugalo hosp. na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli. Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo Buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu vizuri.

Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.

Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada ikabidi awahishwe Mwananyamala hosp. lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo Regency hosp,hivyo akawahishwa Regency na kupata matibabu.

Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa,tigo pesa na benki ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.

Na benki walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.

Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia ‘’kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye.

HIVYO NI KUOMBA MUNGU NA KUWA WAANGALIFU
 
mhh, utata kidogo hapa:

1.mie ninavyojua huwezi chukua zaid ya 1 M kwa ATM chin ya masaa 24
2.au assumption 1m CRDB, 1M NMB na laki 5 m-pesa, na lak 5 tigopesa?

heb tuweke waz hapo kwanza wakati tunachukua taadhari
 
mhh, utata kidogo hapa:

1.mie ninavyojua huwezi chukua zaid ya 1 M kwa ATM chin ya masaa 24
2.au assumption 1m CRDB, 1M NMB na laki 5 m-pesa, na lak 5 tigopes
heb tuweke waz hapo kwanza wakati tunachukua ataadhari
asipo jibu haya maswali hii story ni ya kutunga
 
/utapeli umekuwa fani ya watu wengi sana Bongo. Tujihami na watu wanojifanya kukujua huku huna kumbukumbu ya kuwafahamu. Tujiepushe na offer kutoka kwa watu tusiowajua kwani ni hatari sana.
 
Hawa jamaa wapo ni kama miezi 6 sasa, wanajua vizuri sana kuku sanya taarifa muhimu za wanayetaka kumpora, kwa navyojua mimi wanaushawishi mkubwa wa kuweka mazingira ya kuwa waliyomlenga atanufaidika au atapata faida kubwa zaidi ya kiasi kinacho itajika. Ila huwa wanataka cash,
 
Utapeli umezidi watu tuwe makini sana na tumuombe Mungu atulinde tunapotoka nyumbani na kurudi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom