Aina mpya ya utawala unaozaliwa na vyama vya siasa vya upinzani ni tisho kwa mustakabali wa Tanzania. Watanzania tuvikatae

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Kila nikiutafakari upinzani wa Tanzania nakosa majibu na kunifanya niwaze juu ya hatima ya Tanzania kama ukishika dola siku za usoni lakini juu ya upinzani kushika dawa sifikrii kwa sababu hata mtoto mdogo hawezi wala kuota kitu kama hicho. Kitu kinachofanya niwaze na kufikiria ni huu upinzani wa kustaajabisha uliobeba taswira za kutisha kama ‘ukanda’, ‘udini’, ‘ umimi’ na sasa kuna ‘ usultani’.

Madhila ya taswira hizo za kutisha tumeziona kupitia vyama vya upinzani Tanzania na bado zinaendelea kuonekana kupitia kwa wanachama na viongozi wa vyama hivyo. Napata mashaka kuona kuwa Tanzania kuna siasa za kustaajabisha za upinzani ambazo zinaweka tishio la kurudi kule tulipotoka.

Upinzani huu mpya wa Tanzania unazaa ‘usultani’. Usultani unaozaliwa na huu upinzani unafichwa katika vazi la kisiasa na kufanya watu kushindwa kuutambua. Kwa ufupi, usultani ni utawala ambao sultani ndio kila kitu na hapingwi kwa lolote. Siasa la Tanzania kupitia upinzani ndio unaenda kurudisha usultani( utawala uliokataliwa na wazanzibari kwa mapinduzi). Hii ni aina mpya ya utawala ambao ni tishio kwa mustakabali wa Taifa letu

Kabla sijaendelea, napenda kuuelezea huo usultani na chama kinachohusika kuulea na kuukuza huo usultani kwa sasa ni ACT-Wazalendo chini ya uongozi wa Zitto Z. Kabwe na Juma duni Haji kama kiongozi mkuu na kiongozi mkuu msaidizi. Katika uteuzi wa kiongozi mkuu msaidizi hatukuona vikao vikiketi na wajumbe kupitisha jina ila tumeletewa jina tu na Kingozi mkuu wa chama ambaye ni kinyume na demokrasia na halali katika utawala wa kiimla na usultani ni mmoja wapo.

Cha kushangaza Zaidi bwana ZZK amejivika cheo cha kiongozi mkuu wa chama na hapo hapo kuna cheo cha mwenyekiti wa chama ambacho ndicho kinapigiwa kura na wajumbe na cheo cha ZZK kuwa ni Zaidi ya mwenyekiti. Cheo alichonacho ZZK hakipigiwi kura ili kumchagua na hivyo kujivika madaraka yote ya kisultani ndani ya chama, itakuwaje akipewa nchi atajivika madaraka yapi?

La kustaajabisha Zaidi ni hili la mwenye kadi namba moja ndani ya ACT – Wazalendo, tangu mwaka 1995- ? amekuwa akichukua fomu ya urais wa Zanzibar bila mafanikio na hiyo ndio damu halisi ya kisultani. Sultani hana ukomo wa kuongoza na raia huyo namba 1 ndani ya ACT anaonesha akipata urais hatotamani kuondoka madarakani.

Leo hii watanzania wanapotaka kufumbia macho aina hii ya usultani unaotaka kushamiri Tanzania watakuwa na wajibu wa kufanya mapinduzi mengine ili kuuondoa utawala wa kisultani kama wakishika dola siku moja. Tanzania ni ya watanzania na usultani tuliukataa kwa mapinduzi , iweje leo kizazi hiki wauone tena katika vazi la kisiasa? Tuukate usultani huu chipukizi , tukate shima usiweze kumea.

Mimi kama mtanzania, nitaipigia kura CCM 2020 na kumpigia kura mgombea wa CCM kwa ngazi zote kwa sababu sitotaka kupigia kura’ usultani’, ‘ utemi’, ‘ umimi’, ‘ ukanda’, n.k. kwa sauti ya pamoja , watanzania tuseme naliona tishio la usultani , nachagua kuwa nao mbali kwa kuichagua CCM
 
Tupe tofauti na kiti cha mwenyekiti wa ccm ambaye kwenye kura alipata 100% bila hata kura moja kumkataa wala kuharibika!
 
usultani ni kuwa rais na mwenyekiti chama
usultani ni kitendo cha kupora haki ya katiba mpya kwa raia wako

usultani nipamoja kuzuia bunge live
usultani nipamoja kufanya uchaguzi hewa ili mradi uchaguzi
 
Ungejua hao chipukizi unaowazungumzia walivyo na hasira na hii CCM hata usingethubutu kuwataja.

Watu hawako tayari kuangalia Sera wala itikadi ya chama wanachohitaji CCM ikae pembeni kwanza mengine yatafuata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ww si Mtanzania mwenye uweledi wa kusoma alama za nyakati.

Jiongeze kwa kutumia busara na hekima Kidogo upate kujua hizo sifa za Udini, Ukanda na Imani ni Chama kipi?
ndy msingi wake ktk Awamu hii.
 
Toka nizaliwe sijawahi kuona cheo cha mwenyekiti wa ccm kikagombewa na kupigiwa kura
 
toka nizaliwe sijawahi kuona cheo cha mwenyekiti wa ccm kikagombewa na kupigiwa kura
bora CCM kuna mwenyekiti anayeidhinishwa kwa kupigiwa kura na kura zisipotosha hapewi huo uenyekiti. sasa tuje kwa ACT, nafasi ya zito inapatikanaje? mamlaka yake ya kiongozi mkuu wa chama yanatofautishwaje na mamlaka ya mwenyekiti? hapo ndipo utakapoona usultani unapoanzia
 
bora CCM kuna mwenyekiti anayeidhinishwa kwa kupigiwa kura na kura zisipotosha hapewi huo uenyekiti. sasa tuje kwa ACT, nafasi ya zito inapatikanaje? mamlaka yake ya kiongozi mkuu wa chama yanatofautishwaje na mamlaka ya mwenyekiti? hapo ndipo utakapoona usultani unapoanzia
huo ndiyo usultani kwanini asishindanishwe na wana ccm wenzie? wanachama wa ccm wanaenda kupiga chapa lakini maamuzi ya nani awe mwenyekiti wanakuwa wameamua watu wengine
 
Wanafunzi wa chuo cha magogoni mtapata tabu sana na propaganda zenu za karne ya 20

Sent using Boeing 737-MAX 8
 
Back
Top Bottom