Aina mpya ya ujambazi

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,879
Habarini wajameni,

Kumekuwa na ujambazi mpya siku hizi watu hawaji kuvamia wala nini, jirani zangu wawili wameibiwa kwa staili hiyo, wamekuja jamaa wameshika radio call wanajidai wanaongea "helooo huyo jamaa msimtoe mpaka nirudi mwacheni leo alale ndani" tukajua labda huyu jamaa ni polisi wakaulizia nyumba ya flani iko wapi wakaelekezwa wakaenda wamekaa ndani weee baada ya nusu saa wakatoka wamebeba begi wakaondoka.

Baada ya nusu saa watu wanasikia kelele kwenye nyumba ambayo hao wanaojifanya mapolisi wametoka.

Watu kwenda wanakuta wenye nyumba wamefungwa kamba jamaa wamebeba laptop, simu, tv na fedha hiyo ilikuwa saa tatu za asubuhi.

KUWA MAKINI CHUKUA TAHADHARI
 
Mbinu nyingine ambayo wameifanya mtaani kwetu, ilikuwa kwamba siku hiyo kulikuwa na mkutano wa mtaa na mwenyekiti wa mtaa akawa amesisitiza kuwa vijana na wanaume walio nguvu sio wazee watatakiwa kuweka mpango madhubuti wa kufanya doria usiku. Siku hiyo hiyo baada ya kikao hicho wezi wakatunga mbinu, wakaenda kwenye nyumba ya mtu, wakamgongea kijana wao dirishani maana hiyo nyumba haina fensi (sijui walijuaje dirisha la kijana yule), wakaanza kumfokea "YAANI WEWE UMELALA NDANI MUDA HUU, INA MAANA HUTAKI KUFANYA DORIA NA HALI LEO MWENYEKITI WA MTAA ALISISITIZA KUWA TUFANYE DORIA? TOKA NJE" yule kijana akatoka. Alivyotoka wakamuuliza mko wangapi humu? kijana akasema idadi. Mwamshe baba yako haraka (ilikuwa mbinu wajue kama baba yupo au hayupo). kijana akajibu kuwa baba yuko safari yuko mama tu. wakamwambia amwamshe mama yake. Yule mama alivyofika na yeye wakaanza kumfokea kuwa kwanini vijana wake hawaenda doria. Wanasema hao wezi mmoja wao alivaa suruali kama ya polisi. Basi wakamwamrisha mama afungue mlango waingie ndani, wakaingia ndio wakaanza kumpiga na mabapa ya mapanga, waliiba laki nne, mfuko wa sukari, tv flat screen.
 
Inamaana hyi tv nayo iliwekwa kwenye begi?,itakuwa nchi 20 hyo
 
Kuna ile style yao nyingine ya kufungulia maji.Wanachokifanya ni kwamba kama nyumbani kwako una bomba nje, jamaa wanakuja usiku wanafunguliua maji mpaka mwisho,sasa wewe jifanye kiherehere utoke nje kwenda kuyafunga......hapo ndo utajua kwanini Idd Amini Nduli anaitwa dada.Ni bora uyaache yamwagike bili isome mtapambana na mamlaka ya maji muda wa bill ukifika.
 
Huyo dogo naye hana akili,usiku wa manane unamfunguliaje mtu usiyemjua mlango,hao wacha waibiwe tu akili ziwakae sawa.
 
Kuna ile style yao nyingine ya kufungulia maji.Wanachokifanya ni kwamba kama nyumbani kwako una bomba nje, jamaa wanakuja usiku wanafunguliua maji mpaka mwisho,sasa wewe jifanye kiherehere utoke nje kwenda kuyafunga......hapo ndo utajua kwanini Idd Amini Nduli anaitwa dada.Ni bora uyaache yamwagike bili isome mtapambana na mamlaka ya maji muda wa bill ukifika.
Hii ya maji ni kali watawapata wengi na mimi ningekua mmoja wao asante mchangiaji maana nilikua fasta maji yakimwagika tu nawahi kuyafunga hata usiku wa manane
 
Wapigeni picha kabla ya halafu muwaambie 'You are Welcome tuonane Facebook Instagram etc.'
 
Wa hivyo sisi huku mtaani kwetu tuliwakomesha! Wamekuja na simu vyao vya upepo wakijidai kupiga piga nasi hapa jirani tukaanza kualikana tukawaweka kati. Tulivyowapekua ndo tukakuta kuwa ni wezi,, wacha tuwape kibano mpaka walihara!! Wamshukuru mwenyekiti wa mtaa aliwahi kuwapigia simu viherehere nao wakawahi!
 
Habarini wajameni,

Kumekuwa na ujambazi mpya siku hizi watu hawaji kuvamia wala nini, jirani zangu wawili wameibiwa kwa staili hiyo, wamekuja jamaa wameshika radio call wanajidai wanaongea "helooo huyo jamaa msimtoe mpaka nirudi mwacheni leo alale ndani" tukajua labda huyu jamaa ni polisi wakaulizia nyumba ya flani iko wapi wakaelekezwa wakaenda wamekaa ndani weee baada ya nusu saa wakatoka wamebeba begi wakaondoka.

Baada ya nusu saa watu wanasikia kelele kwenye nyumba ambayo hao wanaojifanya mapolisi wametoka.

Watu kwenda wanakuta wenye nyumba wamefungwa kamba jamaa wamebeba laptop, simu, tv na fedha hiyo ilikuwa saa tatu za asubuhi.

KUWA MAKINI CHUKUA TAHADHARI
TV imebebwa kwenye begi, hii itakuwa inch 11 flat
 
Wa hivyo sisi huku mtaani kwetu tuliwakomesha! Wamekuja na simu vyao vya upepo wakijidai kupiga piga nasi hapa jirani tukaanza kualikana tukawaweka kati. Tulivyowapekua ndo tukakuta kuwa ni wezi,, wacha tuwape kibano mpaka walihara!! Wamshukuru mwenyekiti wa mtaa aliwahi kuwapigia simu viherehere nao wakawahi!

Safi sana.
 
walizuga wako doria
Doria wanalinda nje sio majumbani mwa watu kijana alifanya makosa,unamuaminije mtu kizembe hivyo tena usiku,alitakiwa ajithibitishie identity na uhalali wa hao watu kuwasumbua usiku kabla hajawafungulia .Iko wazi kabisa kuwa hutakiwi kumfungulia mgongaji hodi usiyemfahamu usiku,security protocols zinatakiwa kufundishwa mashuleni na kwenye vyombo vya habari.Kuna kanuni za usalama ambazo ukizifuata mabaya mengi yatakuepuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom