Aina mpya ya “Tattoo” inayofutika yagunduliwa nchini Marekani. Je, uko tayari kuchora?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
buj6ny.png

Kampuni moja changa Ephemeral ya jijini New York nchini marekani, imetengeneza aina mpya ya wino wa tattoo ambayo inauwezo wa kufutika baada ya mwaka mmoja katika kutengeneza masoko ya wateja wapya wa “tattoo.”

“Itafutika tuu hivyo sina wasiwasi’’ maoni ya kati ya wachoraji wapya wa hii tatoo Bi.Abigail Glasgow aliyechora herufi ya kwanza ya jina la mchumba wake mkononi kwake.

Kwa miaka mingi wasanii wa kuchora “tattoo” haswa wa bara la asia wamekua wakichora watu tatoo ambazo hufutika kidogo baada ya muda mrefu sana,kumekua na madai kwamba wino wa mboga mboga “vegetable ink” na kuchora juu juu husababisha tatoo kufutika baaada ya muda.

Lakini ukweli ni kwamba “tattoo” hazifutiki kabisa bali huanza kufubaa na mara nyingi husabaisha makovu na vidonda.

Baada ya miaka sita ya majaribio hatimaye kampuni ya Ephermal imetengeneza aina ya wino unaoundwa na aina ya polima zizoweza kuoza “biodegradable polymers”, ambazo zinafutika baada ya kati ya miezi 9 hadi 15 ya kuchora ambazo hupitia mchakato ule ule wa tattoo za kawaida.

Hatua hii kubwa haikuja kirahisi. Ilikua ni zao la hofu aliyekuwa nayo mmoja wa waanzilishi wa kampuni hii Josh Sakhai akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha New York ambapo alitamani kuchora tattoo ya kudumu lakini alikuwa na uoga sana jinsi ambavyo angechukuliwa na wanafamilia yake waliokuwa na asili ya Iran, hivyo akaamua kutengeza wino ambao ungefutika baada ya muda fulani. Katika mchakato huu alitumia fomula zaidi ya 50 ambazo zote alizifanyia majaribio mwilini mwake.

Studio yao ilifuguliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Machi Williamsburg mjini Brooklyn ambapo hadi sasa wino unaopatikana ni mweusi tuu.Ephemeral tattoo hugharimu dola 175 na 450 za kimarekani sawa na 404,080 na 1,039,065 shilingi za kitanzania.

“Tunachofanya ni kuonesha uwezekano wa tatoo kwa wateja ambao hapo kabla walikuwa na hofu ya kuchora tattoo”. Alisema Josh.
 
Sitakaa kuchora tattoo ktk mwili wangu wote ninaowapenda wamekuwa tattooed moyoni mwangu...na katika damu yangu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom