Aina mbalimbali za vifo tunavyokumbana navyo wanadamu huwa zinanifikirisha sana!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Hili ndilo jambo ambalo pengine ni aina ya mambo yanayonifanya niwaze sana kuhusu kifo.

Kuna watu wakati wa kufa ni anakumbana na aina fulani sijui tuseme ni mateso? Nimewahi kushuhudia vifo mbalimbali mfano wakati nikiwa mdogo yupo kijana mmoja kwanza aliumwa sana (nadhani ilikuwa ni UKIMWI) siku ya kufa Nakumbuka kuanzia saa moja usiku ilikuwa ni mwendo mara nishushe kutoka kitandani, mara nipeleke nje, mara niletee kitu fulani! Huyu jamaa alisumbua sana hadi inafika saa saba usiku ndipo anakata roho na wakati wote huo tulikuwa naye bize akitushughulisha hili na lile. Nakumbuka pia wakati akikata roho alijirusha rusha sana na kunyoosha shingo. Midomo nayo kuachana, macho kufunguka kupita kipimo n.k... Lakini historia ya huyu mtu haikuwa mbaya na hata huo ugonjwa nadhani aliupatia gerezani ambapo alikuwa akipelekwa mara kwa mara kutokana na akili zake kutokuwa sawa (ni kama alikuwa anapelekwa kule kupumzishwa tu) maisha yake yote hakuwahi kuwa na akili timamu.

Mwingine nilishuhudia wakati akifa alishuka kutoka kitandani na akainama palepale akafa (alibaki hivyohivyo akiwa ameinama)

Aidha yupo niliyeshuhudia huyu ilikuwa ni kimyakimya tu hakuna sauti wala mguno. Alikuwa amekaa kwenye kiti akipiga story ghafla akakata palepale bila bughudha yoyote!

Mwingine (huyu alikuwa bibi mmoja) Yeye wakati anakata roho alitumia takriban masaa kumi na moja akitaja jina la Mungu (alikuwa akisema nani kama Mungu? Kwa hayo masaa hadi anakata roho!

Sasa nasikia wapo wengine hutoa choo... Na yupo mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa wengi hasa wanaume hutoa mpaka manii wakati wakikata roho (hii nini maana yake? Inasababishwa na nini? )

Hapa nadhani kina mshana jr na wengine wanaweza kunisaidia na pengine wanaweza kunipa mtazamo tofauti!
 
Kila nafsi itaonja umauti. Na maumivu yake ni makali sana kikubwa zaidi tujiandae kwa kutenda yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na kuacha aliyoyakataza.
 
Mkuu jibu la hapa litategemea ww imani yako umeijengaje. Maandiko kwa sisi wakristo yanasema kila nafsi itaonja mauti Na baada ya kifo hukumu. Kuna sehemu mbili Tu roho ya mtu inaenda baada ya kufa Ni either kuzimu au paradiso. Kumbuka mfano WA Tajiri Na Lazaro. Nakuhakikishia kifo cha tajiri Na lazaro vilikuwa tofauti. Mtu kam unakufa katika dhambi amini utakutana na kifo cha maangaiko maana roho ya mtu huyo tayari inakuwa inajua inaenda katika dhiki Na kinyume chake mtu anayekufa katika Bwana anakuwa kalala Tu mm nakumba mama mdogo wangu alikuwa ameokoka kabla ya one hour hajafa aliomba maombi mazito akinena kwa lugha alipo maliza akakaa kimya ndo ikawa basi. Ndo maana maandiko yanasema heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa maana matendo Yao yatafuatana nao hivyo Kama hutaki kifo cha mahangaiko au mateso andaa maisha yako Na hakuna jinsi nyingine ya kuandaa maisha yako inaanza kwa kumkili Yesu kuwa Bwana Na mwokozi wa maisha yako Na kuokoka Na safari inaanzia hapo. Huo ndo mchango wangu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom