Aina mbalimbali za utekaji nyara: Utangazaji dau unavyoweza kusaidia kwenye uchunguzi (possible scenarios)

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,985
22,512
1539621763203-png.899078

1.Utekaji uliozoeleka ambao ni "basic kidnapping"

Hii inachukuliwa kuwa aina ya awali kabisa ya utekaji nyara na inaweza kufanyika kwa karibu sehemu zote za dunia na kwa maandalizi kidogo sana, na risk ndogo ya kushindwa. Katika matukio mengi, wateka nyara watajaribu kuwalenga watu wafanyabiashara wa ndani ya nchi, au familia zao - watu ambao wanaofikiriwa kuwa "wako vyema."

2. Utekaji wa watu walioko matawi ya Juu na wenye mafaniko makubwa

Utekaji mwingi sana ambao huwa unaonekana kwenye movies, ni wa aina hii. Katika hii situation/scenario, wahalifu hukusanya taarifa kuhusu tabia binafsi au taratibu za usalama za mtu huyo(kwa Mo Dewji hili lilitokea). Mara baada ya mtekwaji kuchukuliwa, fidia uhitajika. Katika hali kama hizo, utekaji nyara mara nyingi unakuwa ni jitihada za kupata pesa.

3. Utekaji chui ama "Tiger kidnapping"

Ikiwa uhalifu unahusisha kuchukua mateka ili kumshawishi atoe ushirikiamo, mfano afanye wizi,au abadili msimamo flani, asaini makubaliano flani nk, basi inajulikana kama tendo la utekaji nyara aina ya “Tiger kidnapping” Katika situation hii, mateka atashikiliwa mpaka pale madai yao yote watekaji hao yatakapokuwa yametimia na mtekwaji kusalimu amri.

4. utekaji wa haraka"Express kidnapping"

Katika hii situation, mtu huchukuliwa na wanalazimishwa kutoa kiasi cha fedha (wenyewe) nje ya benki au ATM. Ikiwa kila kitu kinaenda vizuri, huyo aliyetekwa huachiwa huru. Mara nyingi, aina hii ya utekaji nyara hutokea kwenye maeneo ya miji ambapo kuna ATM nyingi. Kwa mara chache sana, mwathirika ataendelea kushikiliwa kwa madai ya ransom/fidia kutoka kwa wanafamilia.

5. "Virtual kidnapping"(kimtandao)

Utekaji huu ambao ni wa aina mpya, ni more of a scam tofauti na utekaji nyara halisi. Katika situation hizi, wahalifu watasubiri mpaka ule muda ambao unakuwa haupatikani kabisa hewani, kisha wanawasiliana na ndugu wa familia au washiriki wako wa biashara, wanatoa madai kuwa wanamshikilia na wanadai fidia/pesa. Aliyetajwa kuwa katekwa mara nyingi huwa hata hajui kilichotokea wala kinachoendelea.

Angalizo: Kuna taarifa ambazo tayari zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kuna ambazo zimefunguliwa threads lakini zimeunganishwa kwenye ile main ya utekwaji wa Mo. Sidhani kama ni sahihi.

Lakini kama habari za madai ya ransom payments kutoka kwa watekaji ni ya kweli, basi utekaji huu unaangukia kwenye either utekaji wa watu maarufu ama high profile people kwasababu ya pesa, au "utekaji chui" AKA "Tiger kidnapping", ili kumlazimisha kufanya jambo flani nk

Kabla sijaenda mbele zaidi, jambo muhimu kuwekana sawa hapa, hadi sasa hivi hakuna taarifa zozote zilizowekwa wazi kuhusiana na hao watekaji na kile wanachohitaji, lakini taarifa zilizoko, ni kwamba wanadai usd 2b! Hicho ni kiasi kikubwa sana ambacho sidhani kama wanaweza kulipa, labda wawe wameanzia dau la juu kama bargaining strength na kwamba wataweza kushusha dau hilo.

Kama sivyo, kama wakikataa kupunguza dau hilo, basi nia yao moja kwa moja itaweza kufahamika kuwa ni roho yake waliitaka.

Habari hizi naziamini kwa kiasi kikubwa kutokana na uamuzi waliouchukuwa familia ya Mo, wa kutangaza dau hilo. Uamuzi kuntu kabisa, wenye busara na werevu wa hali ya juu sana.

Kwa mfano scenario moja hapa, ni uwezekano wa watekaji kusalitiana kutokana na dau lilotangazwa. Hiyo ni moja.

Pili, inasaidia kwasababu wananchi wanakuwa "vigilantes", kwa maana wanakuwa makini na kutizama mazingira yao. Mwingine, pengine aliona tukio ambalo anahisi labda kuna kitu kinafichwa nk.

Mfano mtu anaweza alikuwa amekaa mahali kitaa akaona surf inaingia kwa kasi kwenye nyumba, hoteli, au labda inaelekea njia Fulani. Pengine Mo amefichwa pahala ambapo kuna mtu ameona activities ama matukio ambayo siyo ya kawaida lakini akapuuza. Utangazwaji wa dau, utasaidia kuwafikirisha wadau zaidi.

Hata kama siyo wale walioko kwenye inner circle ya watekaji, bado lazima kuna mtu ambaye siyo wa inner circle amenusanusa movements nk. kuna polisi ambao pia huwa wananusanusa mambo kama hayo ama taafira za aina hiyo. wanaweza kufuatilia kiana kwasababu ya dau.

Pia kutangaza dau kutaweza kusaidia kwenye issue nzima ya kutekwa kwa Mo Dewji. Kikawaida, watu wa system ni watu wanaofanya kazi ambazo wamekula viapo. Na wanakuwa wametumwa... Situation ikiwa ni wao, basi hatutasikia madai ya ransom au mahitaji ya pesa. Labda wafanye hivyo kama geresha baada ya kuamuwa kuwa wanamuachia huru. Na ikiwa hivyo kama ni kitengo, basi inaweza kuangukia pia kwenye aina ya utekaji ya tiger kidnapping kama nilivyoelezea hapo awali, ambapo mtekwaji kuna mambo ambayo atalazimishwa kukubaliana nayo, na inaweza kuwa siri hata mambo ambayo wamemfanyia wakayatumia kum blackmail ili asiweze kuwageuka. Kuna wanaosema ndicho kilichotokea kwenye ule utekaji wa msanii Roma Mkatoliki.

Uzuri mmoja wa kutangaza dau, kuna kitu kinaitwa "Pandora box", inakuwa opened, one thing leads to another...

Somewhere, somehow, someone saw something crucial to this case. Kwasababu hata kama watekaji ni wa kitengo na hawatasalitiana, lazima kuna mtu mahali ameona tukio ambalo ni suspicious ama siyo la kawaida, movements zisizo za kawaida, kumbuka bado ni Mi ni binadamu na siyo percel. However, changamoto nyingine kubwa, ni kwamba, kama ni watu wa system, halafu kuna taarifa zimepatikana, je familia ya Mo hawatakwamishwa na polisi kama ambavyo wamekuwa wamefanya kwenye matukio mengine ambayo bila shaka wanafahamu kuwa ni kazi ya kitengo? Je kama familia ya Mo ikipata hizo taarifa za watu waliomteka, na ikiwa wakati huohuo ni watu wa kitengo, watachukuwa hatua gani? Certainly sidhani kama wataweza kuwashikirisha polisi, unless wawe tayari na Imani kwamba systema haihusiki na utekwaji nyara wa Mo.

Jambo jingine linalonishangaza, ni jinsi ambavyo wame handle situation hao polisi. Sikumbuki kutajwa kwa rangi ya gari ya Toyota Surf iliyoonekana kwenye cctv. Kwasababu issue kama hiyo, ndiyo ingesadia Zaidi sana upande wa dau lilotangazwa, maana ninaamini kila mtu ambaye angekuwa ameiona surf yoyote mahali popte yenye rangi hiyo, basi angeweza kuvuta kumbukumbu ya jambo lolote lile lilotkea kuhusiana na hiyo surf.

Ni kweli kuna nyakati polisi huwa wanashikilia taarifa flani flani kwasababu za kiupelelezi. Lakini siyo kwenye issue kama hii. Hilo ndilo linawapa wadau mashaka.
 
hazipiti siku tatu ataachiwa tu. me naona wametumia mbinu isiyo ya moja kwa moja kusema wanataka kiasi fulani. nahisi moja kwa moja watakuwa na mawasiliano na familia yake.
Kama itakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na familia yake, je haitakuwa wamechemsha kutangaza tena dau? Au labda wanataka kuwapima waone kama watageukana? Kwasababu mara nyingi, watu wa ransom huwa hawataki uwajulishe polisi wala kuwashirikisha.Kuhusu kutumia mbinu nakubaliana na hoja.
 
mkuu kutaja kiwango cha pesa geresha tu. hawezi siku zote hizi wawe hawajasema wanataka nini. hawa walijipanga. wangepatana kimya kimya, na familia kumchukua kiserikali ingekuwa ishu. so wamewambia wekeni dau. halafu tukishawapa mtasema kuna mtu amewawezesha kumpata, ila kasema msimtaje kwa sababu za kiusalama wake.
 
hazipiti siku tatu ataachiwa tu. me naona wametumia mbinu isiyo ya moja kwa moja kusema wanataka kiasi fulani. nahisi moja kwa moja watakuwa na mawasiliano na familia yake.
Kama ni criminals tu wenye kuhitaji pesa, utakuwa upo sahihi kabisa. Kama ni watu wa system, then hapo kuna ka hatihati flani hapo. Mara nyingi hao huwa wanafanya mission kwenye "a closed neat group", kwahiyo kwenye group hilo ambapo mara nyingi linakuwa dogo tu, huwa si rahisi kusalitiana maana ni rahisi kujulikana. Labda iwe imetokea kuna walionusanusa bila kujulikana, of which hilo linawezekana kabisa. Itakuwa rahisi Zaidi kumpata ikiwa ni criminals.

Kama ni system na wameamuwa kuifanya kuwa mbinu yao, basi pia hilo linaweza kutokea kwa haraka. Lakini hata ikiwa hivyo, lazima watakuwa wametumia ile "tiger kidnapping".

Na ni ukwlei usioweza kupingika kuwa kama asipopatikana, kuna uwezekano mkubwa serikali ikashindwa kukwepa lawama.
 
mkuu kutaja kiwango cha pesa geresha tu. hawezi siku zote hizi wawe hawajasema wanataka nini. hawa walijipanga. wangepatana kimya kimya, na familia kumchukua kiserikali ingekuwa ishu. so wamewambia wekeni dau. halafu tukishawapa mtasema kuna mtu amewawezesha kumpata, ila kasema msimtaje kwa sababu za kiusalama wake.
Mhn!binafsi nilikuwa sijaifikria hiyo angle kihivyo. Kwahiyo uanchosema ni kwamba familia tayari ishakubaliana na serikali na hata hilo dau wamepanga na serikali litangazwe kama zuga?
 
Kama ni criminals tu wenye kuhitaji pesa, utakuwa upo sahihi kabisa. Kama ni watu wa system, then hapo kuna ka hatihati flani hapo. Mara nyingi hao huwa wanafanya mission kwenye "a closed neat group", kwahiyo kwenye group hilo ambapo mara nyingi linakuwa dogo tu, huwa si rahisi kusalitiana maana ni rahisi kujulikana. Labda iwe imetokea kuna walionusanusa bila kujulikana, of which hilo linawezekana kabisa. Itakuwa rahisi Zaidi kumpata ikiwa ni criminals.

Kama ni system na wameamuwa kuifanya kuwa mbinu yao, basi pia hilo linaweza kutokea kwa haraka. Lakini hata ikiwa hivyo, lazima watakuwa wametumia ile "tiger kidnapping".

Na ni ukwlei usioweza kupingika kuwa kama asipopatikana, kuna uwezekano mkubwa serikali ikashindwa kukwepa lawama.
mkuu me naona walifanya makubaliano ishu ni kutengeneza mazingira ya jinsi ya kuliacha hili swala. so nyie tangazeni dau. then tunammrudisha.. harafu mtasema kuna msamalia katusaidia kumpata baada ya kutangaza dau. kama ujuavyo kiserikali huwaga si vyema kufanya makubaliano na wahalifu. na hata ikifanya nao huwa siri mno. coz ni aibu mno serikali kusanda mbele ya waharifu halafu inakuwa inachochea na wengine kufanya uhalifu kama huo.
 
Tanzania imebarikiwa wachambuzi mahiri sana wa matukio mbalimbali, siasa, uchumi n.k chakufurahisha tu ni kuwa ukimuona mchambuzi unaweza usiamini amekaa kijiweni hana A wala B lakini anauwezo mkubwa sana wa kuchambua hihihi
 
Mkuu kama ni uchambuzi unaomake sense, kuna shida gani huyo mtu alipo?Location yake inaathiri vipi mawasiliano yake na uwezo wake wa kuchambua?Fafanua Zaidi. And if that was the case, yani mimi ni mtu anayekaa kijiweni halafu najitolea kununua bundles ili niweze kuposti uchambuzi hapa, whats the problem, maana hata sioni pointi yako hapa?
 
“Somewhere, someone saw something” tuishie hapa ila binafsi siamini kama jamaa bado yupo hai
Yesir! Somewhere, somehow, someone saw something!

I believe also, it is possible that "somewhere, somehow, someone is going to pay"

Hapo kwenye kuhusiana na wewe kuamini kwamba hayuko hai, itakolezea zaidi tuhuma kuwa system ndo wako responsible kwa utekaji wa Mo. Kwasababu kikawaida hao watu wa system huwa hawatoi masharti yoyote ya pesa wala hawadai ransom. Unless kuna mmojawapo ambaye ni "rougue", au kuna ambaye amenusa movements na wao waliofanya utekaji hawajui kama alifahamu. Kama ni system, kwasasa juhudi itakuwa ni kujaribu kuziba mianya ya wale wanaofahamu na pengine kuhakikisha wanaofahamu wanakuwa chini ya uangalizi ama "monitored"
 
1539621763203-png.899078

1.Utekaji uliozoeleka ambao ni "basic kidnapping"

Hii inachukuliwa kuwa aina ya awali kabisa ya utekaji nyara na inaweza kufanyika kwa karibu sehemu zote za dunia na kwa maandalizi kidogo sana, na risk ndogo ya kushindwa. Katika matukio mengi, wateka nyara watajaribu kuwalenga watu wafanyabiashara wa ndani ya nchi, au familia zao - watu ambao wanafikiriwa kuwa "wako vyema."

2. Utekaji wa watu walioko matawi ya Juu na wenye mafaniko makubwa

Utekaji mwingi sana ambao huwa unaonekana kwenye movies, ni wa aina hii. Katika hii situation/scenario, wahalifu hukusanya taarifa kuhusu tabia binafsi au taratibu za usalama za mtu huyo(kwa Mo Dewji hili lilitokea). Mara baada ya mtekwaji kuchukuliwa, fidia uhitajika. Katika hali kama hizo, utekaji nyara mara nyingi unakuwa ni jitihada za kupata pesa.

3. Utekaji chui ama "Tiger kidnapping"

Ikiwa uhalifu unahusisha kuchukua mateka ili kumshawishi atoe ushirikiamo, mfano afanye wizi,au abadili msimamo flani, asaini makubaliano flani nk, basi inajulikana kama tendo la utekaji nyara. Katika situation hii, mateka atashikiliwa mpaka pale madai yao yote watekaji hao yatakapokuwa yametimia na mtekwaji kusalimu amri.

4. utekaji wa haraka"Express kidnapping"

Katika hii situation, mtu huchukuliwa na wanalazimishwa kutoa kiasi cha fedha (wenyewe) nje ya benki au ATM. Ikiwa kila kitu kinaenda vizuri, huyo aliyetekwa huachiwa huru. Mara nyingi, aina hii ya utekaji nyara hutokea kwenye maeneo ya miji ambapo kuna ATM nyingi. Kwa mara chache sana, mwathirika ataendelea kushikiliwa kwa madai ya ransom/fidia kutoka kwa wanafamilia.

5. "Virtual kidnapping"(kimtandao)

Utekaji huu ambao ni wa aina mpya, ni more of a scam tofauti na utekaji nyara halisi. Katika situation hizi, wahalifu watasubiri mpaka ule muda ambao unakuwa haupatikani kabisa hewani, kisha wanawasiliana na ndugu wa familia au washiriki wako wa biashara, wanatoa madai kuwa wanamshikilia na wanadai fidia/pesa. Aliyetajwa kuwa katekwa mara nyingi huwa hata hajui kilichotokea wala kinachoendelea.

Angalizo: Kuna taarifa ambazo tayari zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kuna ambazo zimefunguliwa threads lakini zimeunganishwa kwenye ile main ya utekwaji wa Mo. Sidhani kama ni sahihi.

Lakini kama habari za madai ya ransom payments kutoka kwa watekaji ni ya kweli, basi utekaji huu unaangukia kwenye either utekaji wa watu maarufu ama high profile people kwasababu ya pesa, au "utekaji chui" AKA "Tiger kidnapping", ili kumlazimisha kufanya jambo flani nk

Kabla sijaenda mbele Zaidi, jambo muhimu kuwekana sawa hapa, hadi sasa hivi hakuna taarifa zozote zilizowekwa wazi kuhusiana na hao watekaji na kile wanachohitaji, lakini taarifa zilizoko, ni kwamba wanadai usd 2b! Hicho ni kiasi kikubwa sana ambacho sidhani kama wanaweza kulipa, labda wawe wameanzia dau la juu kama bargaining strength na kwamba wataweza kushusha dau hilo. Kama sivyo, kama wakikataa kupunguza dau hilo, basi nia yao moja kwa moja iatweza kufahamika kuwa ni roho yake waliitaka.

Habari hizi naziamini kwa kiasi kikubwa kutokana na uamuzi waliouchukuwa familia ya Monwa kutangaz adau hilo. Uamuzi kuntu kabisa, wenye busara na werevu wa hali ya juu sana.

Kwa mfano scenario moja hapa, ni uwezekano wa watekaji kusalitiana kutokana na dau lilotangazwa. Hiyo ni moja.

Pili, inasaidia kwasababu wananchi wanakuwa "vigilantes", kwa maana wanakuwa makini na kutizama mazingira yao. Mwigine pengine aliona tukio ambalo anahisi pengine kuna kitu kinafichwa nk. Mfano mtu anaweza alikuwa amekaa mahali kitaa akaona surf inaingia kwa kasi kwenye nyumba, hoteli, au labda inaelekea njia Fulani. Pengine Mo amefichwa pahala ambapo kuna mtu ameona activities ama matukio ambayo siyo ya kawaida lakini akapuuza. Utangazwaji wa dau, utasaidia kuwafikirisha wadau zaidi.

Hata kama siyo wale walioko kwenye inner circle ya watekaji, bado lazima kuna mtu ambaye siyo wa inner circle amenusanusa movements nk. kuna polisi ambao pia huwa wananusanusa mambo kama hayo ama taafira za aina hiyo. wanaweza kufuatilia kiana kwasababu ya dau.

Pia kutangaza dau kutaweza kusaidia kwenye issue nzima ya kutekwa kwa Mo Dewji. Kikawaida, watu wa system ni watu wanaofanya kazi ambazo wamekula viapo. Na wanakuwa wametumwa... Situatio ikiwa ni wao, basi hatutasikia madai ya ransom au mahitaji ya pesa. Labda wafanye hivyo kama geresha baada ya kuamuwa kuwa wanamuachia huru. Na ikiwa hivyo kama ni kitengo, basi inaweza kuangukia pia kwenye aina ya utekaji ya tiger kidnapping kama nilivyoelezea hapo awali, ambapo mtekwaji kuna mambo ambayo atalazimishwa kukubaliana nayo, na inaweza kuwa siri hata mambo ambayo wamemfanyia wakayatumia kum blackmail ili asiweze kuwageuka. Kuna wanaosema ndicho kilichotokea kwenye ule utekaji wa msanii Roma Mkatoliki.

Uzuri mmoja wa kutangaza dau, kuna kitu kinaitwa "Pandora box", inakuwa opened, one thing leads to another...

Somewhere, somehow, someone saw something crucial to this case. Kwasababu hata kama watekaji ni wa kitengo na hawatasalitiana, lazima kuna mtu mahali ameona tukio ambalo ni suspicious ama siyo la kawaida, movements zisizo za kawaida, kumbuka bado ni binadamu na siyo percel. However, changamoto nyingine kubwa, ni kwamba, kama ni watu wa system, halafu kuna taarifa zimepatikana, je hawatakwamishwa na polisi kama ambavyo wamekuwa wamefanya kwenye matukio mengine ambayo bila shaka wanafahamu kuwa ni kazi ya kitengo? Je kama familia ya Mo ikipata hizo taarifa za watu walimoteka, na ikiwa wakati huohuo ni watu wa kitengo, watachukuwa hatua gani? Certainly sidhani kama wataweza kuwashikirisha polisi, unless wawe tayari na Imani kwamba systema haihusiki na utekwaji nyara wa Mo.

Jambo jingine linalonishangaza, ni jinsi ambavyo wame gandle situation hao polisi. Sikumbuki kutajwa kwa rangi ya gari ya Toyota Surf iliyoonekana kwenye cctv. Kwasababu issue kama hiyo, ndiyo ingesadia Zaidi sana upande wa dau lilotangazwa, maana ninaamini kila mtu ambaye angekuwa ameiona surf yoyote mahali popte yenye rangi hiyo, basi angeweza kuvuta kumbukumbu ya jambo lolote lile lilotkea kuhusiana na hiyo surf.

USD 2 bn mbona nyingi sana jaman, yaani mtu ahangaike miaka yooote hiyo, leo Mtu aje tu aamke kuwa tajiri?
 
Back
Top Bottom