Aina, madhumuni na lengo la takwimu za covid tunazodaiwa na WHO si kama unazojua. Ni za 'testing, testing, testing preventive strategy'

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,952
4,326
Kumekuwa na mihemuko ya baadhi ya wanajamii hasa wanasiasa za upinzani, wakitaka kupewa takwimu za ugonjwa wa covid 19. WHO nao wamekuwa wanadai takwimu. Ukweli ni kuwa takwimu wanazozitaka hawa baadhi ya wanajamii wazozitaka na malengo yao ni tofauti kabisa na zile WHO wanazozitaka.

1. Hawa baadhi ya wanajamii takwimu wanazozitaka ni za Watanzania wapewe taarifa kila siku ya idadi ya wagonjwa wa corona kwenye kila mkoa na wilaya zetu. Haieleweki wakishapewa hizo taarifa sijui itasaidia kipi kwani ugonjwa huu hautegemei kuondoka leo wala kesho kama ilivyokuwa kwa UKIMWI. It is here to stay for many years to come (endemic).

Isitoshe ikupata dadi ya watu wanaoumwa ugonjwa covid kila siku haiwezekani kuipata unless kila siku uwapime watanzania wote kipimo cha covid (PCR) kwani 80% ya wagonjwa wa covid hawana dalili na 15% wana dalili za mafua ya kawaida tu. Hawa wasio na dalili na wale wenye mafua ya kawaida takwimu zao huwezi kuzipata kwani wala huwa hawaendi kutibiwa hospitalini na hata wakienda hawapimwi virusi vya covid.

Ni asilimia 5% tu ya wenyebcovid ndiyo wanakuwa wagonjwa (wa SARS aka acute respiratory syndrome aka changangamoto la upumuaji) ambao ndyo huhitaji matibabu ambayo kwa mazingira yetu ni kiasi fulani tu ndiyo hufika kwenye vituo vyetu vya afya (zahanati, health centres na hospitali). Kiasi kingine kikubwa tu hujitibia majumbani au kwa waganga wa jadi ambao huwezi kupata taarifa zao.

Sasa hawa baadhi ya wanajamii wenzetu wanaotaka kujua idadi ya kila siku ya wagonjwa wa covid nchini kwetu, ni wagonjwa wapi hao? Ni hao wachache (less than 5%) wanaofanikiwa kufika kwenye vituo vyetu vya tiba wakiwa na SARS (Changamoto la upumuaji) iliyosababishwa na virusi vya corona (CoV-2) ambao kuujua lazima uwe umefanyiwa kipimo cha RT- PCR (reverse transcription polymerase reaction) ambayo gharama yake ni TSh 150,000/ ? Hii ndiyo takwimu jamaa hawa wanaishupalia iwe inatolewa kila siku? Eti itasaidia watu kuvaa barako, kujifukuzia na kuzingatia masharti mengine ya tahadhari. Eti wala haitawataharukisha. Sasa hata kama ndivyo kwa nini uwape taarifa ya takwimu ambazo si za kweli kuhusiana na ukubwa wa tatizo hilo kama lipo?

2. Takwimu wanazotaka WHO ni tofauti kabisa na hizo za baadhi ya wanajamii wetu. Takwimu zinazotakiwa na WHO ni za utekelezaji wa mpango wa kuwatambua haraka iwezekanavyo wale wote walio na virusi vya CoV-2 na kuwatenga (isolate/quaranteen) hadi pale virusi hivyo vitakapoondoka kwenye miili yao (si chini ya siku 14). Mpango huu unataka maelfu kwa maelfu ( hsa malaki) ya watanzania kila siku wafanyiwe vipimo vya virusi hivi yaani PCR kwa kuchonolewa ndani za mapua yao hadi mdomoni mara kwa mara.

Walengwa zaidi ni wale walio kwenye maeneo yenye uwezekano wa kuwa na virusi hivi (hot spots), waliokutana na wenye virusi hivi (contact tracing), watoa huduma za afya, waalimu, polisi na watumishi wengine wote wanaokutana na public mara kwa mara. Mpango huu unaitwa kiepidemiolojia 'Test, test,test epidemic control strategy'. Mkakati wa aina hii hufaa tu kwenye hatua za mwanzo kabisa wa mlipuko na si baada ya mlipuko kuenea sehemu kuwa. Ni takwimu za survilence.

Wanaopimwa kwa kawaida hawana ugonjwa ila wanaweza kuwa na virusi. Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu ni zoonotic (wa wanyama). The natural host ya virusi hivi ni wild animals and birds including bats. Intermediate hosts include domestic animals and chicken. Ndiyo maana si ajabu wanyama na ndege hawa ku test positive


Kwa bahati mbaya WHO imekuwa ikiwahesabu wote waliopatikana na virusi kuwa ni wagonjwa (Cases) wakati ni 5% tu kati yao ndiyo wagonjwa. Hivyo jinsi unavyopima wengi ndiyo unaonekama una wagonjwa wengi na WHO imekuwa ikishinikiza nchi zipime watu wengi sana kila siku.

Hivyo utaona kuwa si rahisi kukusanya hizo takwimu wanazotaka hao WHO ikizingatiwa sisi mambo ya lockdown na isolation ya watu ambao si wagonjwa tulisha achana nayo. Isitoshe hizo gharama za kupima watu ambao si wagonjwa ni upotevu wa pesa. Na ukweli ni kuwa hata hizo nchi zinazotoa takwimu hizo kwa WHO, nyingi ni za uongo na za kubumba. Wananchi wengi hawakubali kuchokonolewa pua zao ili hali si wagonjwa. Ni udanganyifu mtupu. Sisi ni wasema ukweli, hatuwezi kupeleka takwimu za uwongo uwongo.

3. Prevalence na incidence rates:
Kuenea kwa ugonjwa kwenye jamii hupimwa kwa kufanya a prevalence (kuenea) study of a randomized non biased represantative sample of the population of the community at a point in time (eg a paricular date) or over a specified time period (eg a certain month). Hii ndiyo itakupa takwimu halisi ya ukubwa wa tatizo kwenye jamii. Itakupa ni propotion gani kwenye jamii ina hilo tatizo kipindi hicho. Prevalence inajumlisha existing and new cases at that time. Incidence ni kwa new cases only.

4. Takwimu za hospitali kamwe haziwezi kukupa picha ya ukubwa au udogo wa tatizo kwenye jamii. Kwanza si wote wenye tatizo wanakwenda hospitali na wanaokwenda kwenye hospitali siyo wote wanatoka kwenye hiyo jamii.

5. Idadi pekee (namba) haina maana. Kinachotazamwa ni proportion ya sample population. Kwa mfano ukisema Mkoa wa Singida leo una wagonjwa 10 wa covid 19 na mkoa wa Mwanza una wagonjwa 20 haimaanishi kuwa mkoa wa Mwanza ndiyo umeathirika zaidi ya mkoa wa Singida. Kama population ya Mwanza ni watu million 5 wakati ule wa Singida una watu million moja, basi mkoa wa Singida ndiyo umeathrika zaidi. Bahati mbaya hata takwimu za WHO ambazo zimekuwa zikitolewa ni zile za idadi tu, zile za uwiano zinamezewa kwa makusudi.
 
Naona umeandika kwa kukariri vitabu vinasemaje.Rudi ukasome kwa kuelewa principle za epidemic of a new disease.
 
As long as huna isolation centers, hakuna lockdown na mipaka ipo wazi kabisa ambapo every Tom, Dick & Harry wanaingia tu bila kuulizwa cheti cha covid19, hakuna maana yoyote kupima na kutangaza data. Ukishawapima watu tena ambao wamejipeleka wenyewe unawaweka wapi?

Suala la test test test & announce linakwenda sambamba na maandalizi thabiti ya vitu vingine. Tanzania "tunakwepa" kupima na kutangaza maana swali la pili baada ya kusema una positive cases say 300 per day litakuwa "hawa carriers umewaweka wapi ili kuhakikisha hawaambukizi wengine"? Swali la tatu litakua "umeshafanya contact tracing na kuwakamata wale wooote waliocontact na hawa wagonjwa ndani ya siku 10 zilizopita"? swali la nne litakuwa vipi wale wageni walioingia nchini bila kuonyesha hali zao za afya kwa kuwa hukuwaomba vyeti?
 
Back
Top Bottom