Aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
mwanamme.jpg

Aina Kumi Za Waume Ambao Wake Zao Wanakereka Kuwa Nao*

Kila ndoa inachangamoto zake na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa *kuvumiliana* katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamu ambazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona *nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;*

*(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband);* Hii ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

*(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband);* Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

* (3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband);*Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya msingi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.

*(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband);* Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

*(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband);* Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.

*(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband);* Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhaifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.

*(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband);* Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.

*(8) Mume Mtalii (Visiting Husband);* Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

*(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband);* Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.

*(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband);* Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

*Hiyo nji baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo ?na kama ni mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako.*
 
View attachment 442079

Hahaha hao wote ni chadema, ndiyo maana chadema wanaongoza kwa kuachwa na Wanawake Tanzania!
 
We Dada huwa unawashwa nini ubongoni mbona akili ndogo hivi?kiherehere tu na ROHO mbaya... Ulivo na chuki epuka kuonyesha ujinga wako huu hadharani labda kama hii tabia yako ya kitoto unaifanyia huku tu jf Ila kama hadi nyumbani kwenu uko hivi basi Wazazi wako wana mzigo Sana.. Mpuu zi... Husomi Maada ukaelewa.. Mambo ya siasa yamekuathiri na Sasa unakuwa unapagawa.. Utadata ukweli nakueleza
 
Mbona hakuna Maelezo kwa Mwanaume asiweza Mchezo? Sifa zote nzuri uwe nazo lakin Kama huwezi Msuguano Utakuwa kidume cha namna gani?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom