Aina hii ya ndege uchunguzi wa kitaalam kuhusu "performance" ya ndege unahitajika.

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana JF.

Ni takriban miezi mitano tu imepita tangu kutokea ajali mbaya ya ndege ya shirika la LION AIR la Indonesia, aina ya BOEING 737 MAX 8. Jana Jumapili tarehe 10/03/2019 inatokea ajali nyingine ya shirika la ndege la Ethiopia ambayo inauwa takribani aburia 157 wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, nayo ni aina ile ile ya ndege katika mazingira yale yale.

Ninasema ni mazingira yale yale si kwa maana ya maeneo yale yale ya ajali zinapotokea bali mazingira ya urukaji wa ndege (take off).

Ndege ya shirika la LION AIR ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka na kudondoka baharini. Kwa taarifa za uchunguzi wa ajali za ndege, chanzo cha ajali ya ndege hiyo ni kutokana na ndege kujiingiza (engage) kwenye mfumo wa ndege kujiongoza yenyewe (autopilot), nose down na kumshinda pilot kuitoa kwenye mfumo huo (autopilot disengage). Matokeo yake ndege ilipiga mbizi baharini. Taarifa ya awali ya ajali hiyo ilivyosema kuwa ndege hiyo ya LION AIR ilidondoka baharini kwa kasi ikiwa nose down nilihisi ni makosa ya rubani kuwa alipanda kwa kasi kubwa sana kiasi cha ndege kupoteza kani mnyanyuo (lift force) kutokana na ke-exceed angle of attack, hivyo ndege kupoteza nguvu (stall) navrubani akafanya dive manuevre ili kuirudisha jatika hali yake. Nilihisi kuwa hali hiyo ndiyo iliyomfanya rubani ashuke kwa kasi kichwa chini baharini.

Baada ya taarifa ya uchungu kutoka na kuonekana ni kuingia autopilot tena nosedown na kushindikana kutolewa, nilianza kuwa na wasiwasi wa "controlability" ya ndege aina hii ya ndege. Ajali ya ndege ya ETHIOPIA AIRLINE ikiwa ni aina ile ile ya BOEING 737 MAX 8, katika mazingira yale yale ya kupanda (ascending), na taarifa za mwanzo zinasema rubani alituma taarifa ya kutaka kurudi uwanjani kutokana na kushindwa kui-control ndege. Inanipa wasiwasi kuhusu controlability ya ndege hii hasa wakati wa kupanda kuitafuta cruising level.

Uchunguzi ufanyike katika aina hii ya ndege kama zina tatizo la kiufundi lifahamike zisiendelee kupoteza watu kwa sababu ajali ya ndege majeruhi huwa ni ndara sana, mara nyingi ni "no survivors".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi barafu na wewe ni ndugu moja yuko wapi mwenzio siku hizi,,? Au kule kuongea sana kuhusu shilika letu mfufuka kulimpoteza,,!!
Mambo ni mengi ila muda ni mchache,,
 
TAA wazuie ndege aina ya Boeing 737 Max 8 kutua kwenye viwanja vyetu mpaka uchunguzi wa chanzo cha ajali utakapokamilika. Bahati nzuti ET wamezi-ground zote za aina hii.
 
kweli kabisa mkuu nimesoma report ya ndege ya LION AIR na nimepitia report ya ndege hii ya ETHIOPIA

zote zilipoteza control zikiwa bado kwenye kutafuta Altitude

na kwenye kesi kama hyo ni ngumu sana kupona ukicheki ilipotea kwenye radar ikiwa kwenye speed ya 400 knots. sasa hapo jumlisha na uzito wa ndege yenyewe na tani za mafuta (AVGAS) Ilizonazo kwenye fuel tanks ni ngumu kupona kama ikidondoka

kutakuwa na tatizo la kiufundi kwenye hizi boeing 737 max 8 hasa kwenye eneo la kutafuta cruisingH altitude
Screenshot_20190312-100110.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni jukum la wamiliki husika wa ndege. Tukisema tuzuie basi biashars nyingi zitasimama.
Mpaka uchunguz umalizike huko ethiopia kujua nn tatizo.
TAA wazuie ndege aina ya Boeing 737 Max 8 kutua kwenye viwanja vyetu mpaka uchunguzi wa chanzo cha ajali utakapokamilika. Bahati nzuti ET wamezi-ground zote za aina hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF.

Ni takriban miezi mitano tu imepita tangu kutokea ajali mbaya ya ndege ya shirika la LION AIR la Indonesia, aina ya BOEING 737 MAX 8. Jana Jumapili tarehe 10/03/2019 inatokea ajali nyingine ya shirika la ndege la Ethiopia ambayo inauwa takribani aburia 157 wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo, nayo ni aina ile ile ya ndege katika mazingira yale yale.

Ninasema ni mazingira yale yale si kwa maana ya maeneo yale yale ya ajali zinapotokea bali mazingira ya urukaji wa ndege (take off).

Ndege ya shirika la LION AIR ilipata ajali muda mfupi baada ya kuruka na kudondoka baharini. Kwa taarifa za uchunguzi wa ajali za ndege, chanzo cha ajali ya ndege hiyo ni kutokana na ndege kujiingiza (engage) kwenye mfumo wa ndege kujiongoza yenyewe (autopilot), nose down na kumshinda pilot kuitoa kwenye mfumo huo (autopilot disengage). Matokeo yake ndege ilipiga mbizi baharini. Taarifa ya awali ya ajali hiyo ilivyosema kuwa ndege hiyo ya LION AIR ilidondoka baharini kwa kasi ikiwa nose down nilihisi ni makosa ya rubani kuwa alipanda kwa kasi kubwa sana kiasi cha ndege kupoteza kani mnyanyuo (lift force) kutokana na ke-exceed angle of attack, hivyo ndege kupoteza nguvu (stall) navrubani akafanya dive manuevre ili kuirudisha jatika hali yake. Nilihisi kuwa hali hiyo ndiyo iliyomfanya rubani ashuke kwa kasi kichwa chini baharini.

Baada ya taarifa ya uchungu kutoka na kuonekana ni kuingia autopilot tena nosedown na kushindikana kutolewa, nilianza kuwa na wasiwasi wa "controlability" ya ndege aina hii ya ndege. Ajali ya ndege ya ETHIOPIA AIRLINE ikiwa ni aina ile ile ya BOEING 737 MAX 8, katika mazingira yale yale ya kupanda (ascending), na taarifa za mwanzo zinasema rubani alituma taarifa ya kutaka kurudi uwanjani kutokana na kushindwa kui-control ndege. Inanipa wasiwasi kuhusu controlability ya ndege hii hasa wakati wa kupanda kuitafuta cruising level.

Uchunguzi ufanyike katika aina hii ya ndege kama zina tatizo la kiufundi lifahamike zisiendelee kupoteza watu kwa sababu ajali ya ndege majeruhi huwa ni ndara sana, mara nyingi ni "no survivors".

Sent using Jamii Forums mobile app

Swali fikirishi rubani anawekaje ndege kwenye autopilot katika muda mfupi kama huo hata stability ya ndege angani haijawa achieved ,yaa ndani ya dakika 12. Tu
 
Sio mtaalamu sana wa ndege lakini from engineering point of view na ulichokiandika inaonekana kuna tatizo la balancing during take-off kwa maana ya nose-up hapa ndio kwenye root cause of the problem halafu ndio unapata engagement ya autopilot.
Sijui during take-off, max and min angle ni ipi lakini inaonekana kama wakati wa take-off zinakwenda beyond max angle na controller ikisense ndio unapata auto pilot and will only disengage once no problem lakini if the problems still there bado controller haiwezi kukuruhusu kudisengage hiyo auto-pilot.. NI MAWAZO YANGU TU YA KIFUNDI.
 
Swali ninalojiuliza kila mara pale inapoelekea kutokea ajali kama hiyo, ni vipi abilia wana_react na huchukua action gani kuelekea tukio la ajali au wakijua ndiyo mwisho wa uhai wao?
 
Huo ubavu utoke wapi
TAA wazuie ndege aina ya Boeing 737 Max 8 kutua kwenye viwanja vyetu mpaka uchunguzi wa chanzo cha ajali utakapokamilika. Bahati nzuti ET wamezi-ground zote za aina hii.

Vrou van samaria give me bit of water to drink
 
Swali fikirishi rubani anawekaje ndege kwenye autopilot katika muda mfupi kama huo hata stability ya ndege angani haijawa achieved ,yaa ndani ya dakika 12. Tu

No sio rubani anayeweka auto-pilot, inajiweka yenyewe halafu inagoma kutoka pale rubani anapojaribu kuitoa... Hivi ni vitu vya kawaida kwenye technical issue's hasa pale conroller inapokuwa imsense kitu fulani... Maengineer wa Boeing inapaswa wakae wafanye troubleshooting na analysis ya hizi ajali ili watatue tatizo something wrong there.
 
yaani jukumu unawaaachia wenye ndege? ngoja siku ikidondoka Kariakoo ndio utajua nilikuwa namaanisha nini
Hakuna lolote. Kisa imedondoka kwingine tuzuie sis as if zinatuhusu.
Yes wenye ndege na walio tengeneza ndio watakuwa responsible na ndege yao.
Hatuwez kuzuia ndege zingine sababu hiyo.

Hakuna kiwanja cha ndege duniani kimefanya hiyo kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brooo naona upo vizuri kwenye interlocking devices. Unachokisema ni kweli. Welcome to engeering world.

Once ndege iki experince abnomal situation asumption ni kwamba Rubani ameshindwa kuicontrol for a variety of reasons,

Kwa sababu ndege ni intelligent basi ina ji engage kwenyw autopilot ili ijiendeshe according to her intelligence.

Once rubani atakapofight na yeye afanye yake anakuta ndege inajiokoa yenyewe na yeye anashindwa kurudisha kwenye manual pilot na mwisho wa siku ndege inashindwa mwishowake inadondoka pua chini.

NB: autopilot ni nzuri sana na katika maeneo mengi imefanya kazi wakati rubani hayupo active. Huenda ni hijacking, ulevi, or any unsafe activity done. Lakini inabidi kuwepo na namna ya ku dis engange autopilot instrumentation ili rubani afanye maamuzi yake katika kuondokana ajali zisizo za lazima.
Sio mtaalamu sana wa ndege lakini from engineering point of view na ulichokiandika inaonekana kuna tatizo la balancing during take-off kwa maana ya nose-up hapa ndio kwenye root cause of the problem halafu ndio unapata engagement ya autopilot.
Sijui during take-off, max and min angle ni ipi lakini inaonekana kama wakati wa take-off zinakwenda beyond max angle na controller ikisense ndio unapata auto pilot and will only disengage once no problem lakini if the problems still there bado controller haiwezi kukuruhusu kudisengage hiyo auto-pilot.. NI MAWAZO YANGU TU YA KIFUNDI.

Vrou van samaria give me bit of water to drink
 
Swali fikirishi rubani anawekaje ndege kwenye autopilot katika muda mfupi kama huo hata stability ya ndege angani haijawa achieved ,yaa ndani ya dakika 12. Tu
Soma kwa umakini usione raha kukosoa unaweza kujikosoa mwenyewe.... Sijaona mahali rubani aliweka auto pilot Bali nimeona sehemu ruban ameshindwa kuitoa kwenye uwo mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali fikirishi rubani anawekaje ndege kwenye autopilot katika muda mfupi kama huo hata stability ya ndege angani haijawa achieved ,yaa ndani ya dakika 12. Tu
Elewa maelezo rudi kasome tena, umeambiwa ilivyokuwa inanyanyuka kutafuta cruising level hata bado aijapata stability maaana wamesema ni dk 6 tu toka inyanyuke ndio ikapoteza direction ,na tatizo ili Autopilot ji Engage yenyewe sio rubani alifanya hvyo ni yenyewe bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom