Aina gani ya nyanya inafaa kulima msimu wa masika?

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,227
2,197
Nyanya ni zao ambalo hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu msimu wa mvua nyingi na msimu wa baridi kali. Hali hiyo husababisha bei ya nyanya kupanda sana kipindi hicho na wale wanaobahatika kuwa na nyanya vipindi hivyo huuza kwa bei nzuri.

Naomba kujua ni aina gani ya nyanya inayofanya vizuri msimu wa masika, najua changamoto za kilimo cha nyanya ila nataka nicheze na misimu ili kutega soko.

Naomba kuwasilisha wandugu.
 
Mbegu inayofaa kulima kipindi cha mvua Ni mbegu ambayo imetengenezwa kuhimili sehemu kubwa ya misuko suko na changamoto na magonjwa mengi yanayokithiri kipindi cha mvua.

Ukiwa na lengo la kuzalisha mbegu hizi jitahidi kwenye makadirio yako wakati wa kuzalisha matunda uwe ni kipindi cha mvua, simply sababu zenyewe nyingi hua hazina uwezo wa kuhimili changamoto za kipindi cha jua.

Zipo mbegu nyingi tuu zinazoweza kulimwa kipindi cha mvua na zikafanya vizuri, miongoni mwa hizo ni Gamhar f1, Imara f1, Ansal f1, TO 135, DRD, Firenze, Rambo, Eden na shanty.

Uchaguzi wa mbegu pia unaendana na ukanda uliopo ili kupunguza hasara zinazotokana na mazingira.
Wazoefu watarekebisha penye makosa hapo
 
Asante, naendelea kusubiri michango mingine zaidi.
 
Nadhani machaguzi ya mbegu yanategemea na unapolima mkuu, mimi nimelima imara f1 pande za Ruaha Mbuyuni, dawa za ukungu zipo ni huduma tu unatoboa
 
Vp mzee matokeo yake. Ulipanda ekari ngap na ulivuna creti ngap
Uliza changamoto Kwanza ukisha zijua fuatilia mavuno, jamaa alikwambia kapiga 22m kwa ekari utakurupuka hata kwa kukopa halafu unakutana na kantangaze anakupa uja wepesi na unazaa sifuri ogopa sana, nakushauri uzijue changamoto kabla ya kujua mavuno.
 
Mbegu inayofaa kulima kipindi cha mvua Ni mbegu ambayo imetengenezwa kuhimili sehemu kubwa ya misuko suko na changamoto na magonjwa mengi yanayokithiri kipindi cha mvua.

Ukiwa na lengo la kuzalisha mbegu hizi jitahidi kwenye makadirio yako wakati wa kuzalisha matunda uwe ni kipindi cha mvua, simply sababu zenyewe nyingi hua hazina uwezo wa kuhimili changamoto za kipindi cha jua.

Zipo mbegu nyingi tuu zinazoweza kulimwa kipindi cha mvua na zikafanya vizuri, miongoni mwa hizo ni Gamhar f1, Imara f1, Ansal f1, TO 135, DRD, Firenze, Rambo, Eden na shanty.

Uchaguzi wa mbegu pia unaendana na ukanda uliopo ili kupunguza hasara zinazotokana na mazingira.
Wazoefu watarekebisha penye makosa hapo
Vp Bei ya hzo mbegu bora za Nyanya
 
Nasikia tengeru hybrid inastahimili sana magonjwa bei yake ipoje?

Pia ukitaka kulima masika hakikisha una mtaji wa kutosha
 
Nadhani machaguzi ya mbegu yanategemea na unapolima mkuu, mimi nimelima imara f1 pande za Ruaha Mbuyuni, dawa za ukungu zipo ni huduma tu unatoboa
Kaka naitaji kulima VIP uwezekano wa kupata shamba hapo ruaha mbuyun na bei zake
 
Back
Top Bottom