Aina 50 ya Online Business Platforms unazoweza anzisha Tanzania na uka-Dominate Soko

==> Anzisha Mitandao kama Uber, Tala, Airbnb, Amazon, Zidisha, Makazi, Jumia, Brightermonday...Upate Kuwa na Competitive Edge na Utoboe Kiufanisi Zaidi
------------------------------------------

1. Platform kuu kuuza mazao nchi nzima = hapa naamaisha kuwepo kwa platform ambayo wauzaji nchi nzima wanaweza uza mazao yao kwa haraka na uhakika. Mteja anaweza tafuta mazao fulani kulungana na specification kama kiasi, aina, bei, eneo, quality na kuagiza moja kwa moja mtandaoni na yakaja alipo.

Unajua sehemu kubwa ya Watanzania ni wakulima.

Sasa hapa ili uchomoke vyema ni lazima u-disrupt soko ambapo itabidi madalali uwaingilie nafasi yao kwa were kuweka system ambayo mkulima au wakala anauza mazao moja kwa moja kwa mnunuzi was mwisho; sababu wale madalali hawatakuwepo basi mtaweza uza mazao yenu kwa gharama bafuu zaidi na ktk quality nzuri. Sasa mteja ndio kila kitu: wateja wengi kama mahoteli na mashule watapenda kununua kwenu sababu mnakuwa na bidhaa original na yenye bei nafuu zaidi.

Usiogope kufanya disruption ktk soko maana usipofanya wewe basi wengine watafanya na wewe utakuwa mhanga. Disruption inaboresha soko kwa mteja. Hapa pia utasaidia wakulima wengi kunufaika na mazao yao. Wenzetu Wakenya wana kitu kama hiki.

2. Touring platform - hapa patamu. Kuna vivutio vingi haapa Tz lkn wengi hawajaweza kuviona. Sasa platform yako inakuwa imejikita kutangaza vivutio vya ndani na nje ya nchi; lkn pia kuandaa safari kuwapeleka watu maeneo hayo ya utalii. Hapa kuna kuwa na swala la usafiri, malazi, vyakula, michezo, campsites na vivutio. Sasa labda trip ya wiki ijayo inagharimu Tshs. 150k kwa mtu mmoja halafu ukawa umepata watu 75 na ktk kila mtu faida yako ni 45k hivyo kwa watu 75 unakuwa umetengeneza 3.375M faida.

Sasa ukawa very ambitios ukawa unaorganise tours za kutosha nchi nzima na ukawa na ubia na wadau mbalimbali wa utalii, basi utakuwa habari njema sana kwa tuor lovers. Watu wanaoenda honey moon itakuwa kwao rahisi kufanya kazi nawe. Hapa mteja anaingia ktk platform kisha anachagua kivutio na tarehe kisha anachagua huduma za ziada atakazohitaji then anafanya malipo kuweka booking ya tours. Siku ya tarehe mnaanza tour yenu kwa usalama na burudani kwa wateja wako. Unaorganise vyema mpaka wale wateja wawaite marafiki zao kwako.

3. Online Tuition - hii idea ni nzuri. Wanafunzi wengi wanapenda tuition, hata wazazi pia. Sasa unakuwa umejitoa vizuri na unaingia ubia nawalimu mbalimbali kuandaa notes za maandishi na video za topiki mbalimbali halafu wanafunzi wanakuwa wanaweza kuzisoma, kufundoshwa, kuuliza maswali, kufanya mazoezi…

Hapa mwanafunzi kwanza inabidi awe mwanachama kwanza wa Tuition hiyo labda 10,000 kwa mwezi halafu then anakuwa huru kusoma chochote ambacho kipo ktk mtandoa huo. Sasa mfano wanaosoma PCM unaweza kuta kwa mwezi akalipia 30,000 kwa jili ya tuition, sasa kama atalipia 10,000 kwa vyote basi utawavuta wengi. Lkn hapa unapaswa kuhakikisha unakuwa na nondo adimu. Solution za kutosha. Mpo active muda wote.

4. Duka la kuuzia pembejeo za kilimo = ni ngumu kutafuta dawa au mashine eneo ulipo kwa kuzunguka mji mzima. Na mashine nyingine ni adimu au usizifahamu kama zipo. Kuwepo kwa duka kama hili kutarahisisha mteja kupata pembejeo anayotafuta kwa unafuu, akagundua pembejeo muhimu nyingine, urahisi wa kutafuta, uhakika wa ubora

5. Platform ya kukopeshana mtaji wa kilimo - hii concept ni nzuri sana; inahitajika kuwepo kwa sehemu ambayo wakulima wanaweza kopa mtaji kuweza kulima aua kufuga. Mkopo uwe wa haraka na riba ndogo. So wewe kama mkopeshaji/mwekezaji unaingia ktk platform na unawekeza/kopesha fedha zako kwa watu kadhaa unaowataka.

Hapa mkopeshaji anaweza kuwa na 100,000 na akakopesha watu 10 kila mmoja 10,000 ili kuweza ku-dicersfy risk; mfumo huu tunauuona India ktk micro-lending paltforms na zinasaidia. Inafanana na Tala ila inakuwa na wakopeshaji wengi na wakopaji wengi. Pia wakopeshaji wanapata sehemu ya kuwekeza pesa zao na kupata faida ktk kilimo kwa masharti nafuu

6. Duka la kuuzia pure natural food - nani anapenda kula bidhaa zenye madawa? Kama atajitokeza mtu mmoja akajitoa kuhakikisha anakuwa na eDuka lenye bidhaa ambazo zina very less chemical, basi wapo watu wengi ambao watakuwa wanapenda kuagioza bidhaa hizi kwajili ya chakula natural. Hapa waweza anzisha ktk wilaya aua mji wako na ukatengeneza pesa nzuri

7. Food lovers platform - hii inakuwa ni platform nyingine online ambapo muuzaji unakuwa na vyakula na mapishi aina mbalimbali ya kusuprise watu. Unakuwa na wapishi wako wazuri halafu labda kila Jumapili unakuwa unatoa pishi jipya na kisha unawapelekea wateja wako. Utaratibu unakuwa hivi, wateja wanajiunga uanchama labda kwa mwezi Tsh. 30,000/= halafu kila wiki unakuwa unatafuta pishi adimu surprize kisha unawapelekea wateja wako wale ambao wamejiunga uanachama. Sasa kama ktk 30,000 unapata faida ya 10,000 kwa mwezi na pia unakuwa na wateja 300 wa kuanzia mtandaoni basi unakuwa na 3M

8. Duka la kuuza vifaa vya jikoni - nilishangaa siku moja nimeenda kariakoo na kukuta vifaa vya kutengenezea maua ya keki kwa ku mould na silicon. Nilikuwa sijuia kama vipo vitu kama hivyo. Sasa kwanini wewe usianzishe duka ambalo linakuwa na vifaa vilivyo sheheni adimu na vizuri na wateja wakawa wanaagiza toka mikoa yote TZ

9. platform maalumu ya kukodisha mashamba - unajua kuna watu wengi wanapenda kulima lkn kikwazo kimoja wapo ni wapi atapata shamba. Lkn pia mikoani na vijijini kuna watu wengi wanamaeneo na wangeweza kukodisha mashamba yao na kuwasaidia wngine. Hii inawezekana na wewe unayependa kuanzisha basi unapaswa uwe very smart rule breaker person ili ufanikishe hii idea maana inahitaji process na innovation nzuri

10. Platform ya kulima pamoja - najua unafahamu uber na concept yake ni ECONOMIC SHARING. Sasa kwanini tusiwe na platform ya kilimo ambayo mtu anayetaka kulima na amepungukiwa labda mtaji, shamba, pembejeo, utaalamu aweze kutafuta co-sharer ili waweze fanya PAMOJA? So kama nina banda la kuku 1000 na sina mtaji basi natafuta mtu aliye na uweze wa kuweka vifaranga hao 1000 na kisha akiuza mayai basi kuna kuwa na makubaliano ya kugawana faida. Hii ni concept nzuri sana; Economic sharing kwa sasa ndio inashika kasi sana duniani hadi ulaya serikali zinafanya utafiti namna ya kuitumia kurahisisha mambo ktk jamii

11. Uber ya kusafirisha mazao kwa pamoja - unajua kuna wakulima mikoani ambao wangependa kusafirisha mazao toka Mbeya na kuja Dar lkn wanakosa mtaji wa kutosha? Unaweza kuwa na agretive platform ambayo inakutanisha wakulima wanaotaka kusafirisha mazao tarehe fulani kuja sehemu fulani kisha wakajumuika na kupata usafiri wa pamoja kwa gharama nafuu na kuleta Dar.

12. Fast food eRestaurant - waweza anzisha ktk mji wako popote TZ platform ya mgahawa mtandaoni ambapo mteja anaweza agiza chakula fulani na wewe ukampelekea eneo lake ndani ya muda mfupi

13. Duka la kuuza mbao mtandaoni - unajua kuwa ubao wa Tshs.4000/= Dar, ukienda Mafinga ni Tshs. 2000/=. Kama mtu unaweza kuorganise haya mambo basi waweza anzisha duka lililojikita ktk mbao na miti na ukawasaidia watu kupata bidhaa hizo kwa unafuu na wakati. Labda badala ya 4000 wewe ukawauzia 3500 na mzigo anaagiza moja kwa moja mtandaoni na analetewa alipo. Unajua mbao ndizo zinazogharimu sana ktk ujenzi?

14. Duka la kuuza vifaa vya ujenzi - upo Mbeya au Mpwapwa? Waweza anzisha duka la kuuza vifaa vya ujenzi eneo lako. Waweza ruhusu watu wawe wanalipia kidogo kidogo vifaa na akikamilisha malipo ndani ya muda huo then anapelekewa mzigo wake; maana ujenzi wengi wanalipa kidogo kidogo na kwa njia ya mtandao malipo hayo ya installments ni rahisi na mteja anaweza anza lipia kuanzia Tshs. 500/=

15. Duka la kuuza furniture TZ nzima - Waundaji wnegi wa fanicha labda wanapatikana Dar. Lkn kuna watu mikoani ambao wanapenda vitu vizuri zaidi. Waweza anzisha duka ambalo linaweza wakutanisha wauuzaji fanicha na wateja. Mteja akawa na uwanja mpana wa kuchagua fanicha anazotanka yeye na kwa bei yenye ushindani na kisha akaagizaaletewe. Pia wawezakuwa na fanicha nzuri kutoka nje.

16. Duka la kuuza fanicha used - Nani anapenda kununua kitu kwa bei kubwa? Kama kuna uwezekano wa kupata kitanda cha 500,000 kwa bei ya 250,000 basi wapo watu wengi ambao watapenda kununua ktk eDuka lako. Wewe hapa unafungua duka ambao mtu akiwa na fanicha used basi anaziuza mtandoani na mteja akinunua basi mzigo unapelekwa kwa mteja. Utakacho fikiria kigumu na maswali yako kichani kwmaba itakuwaje itakuwaje hapa yote yanawezekana na by the way watu wapo ambao wanafanya haya

17. Platform ya kukutanisha mafundi na wateja - hapa unachokuwa nacho ni platform ambapo kuna kuwa na mafundi ambao wamejiandikisha humo kwa fani zao na level zao. Unakuwa na kazi ya ku-MATCH fundi na machaguzi ya mteja. Sasa hapa lazima mteja apate fundi mzuri mwenye uhakika na ambaye ataweza mfanyia kazi yake vyema. Hapa mteja atachagua fundi na kufanya malipo mtandaoni kisha fundi ataenda kumfanyia kazi mteja. Ni kama Taskrabbit ya USA

18. Platform ya kuuzia viwanja mtandaoni - kwa TZ bado hakujawa na platform moja ya uhakika ambayo unaweza tafuta viwanja ktk uwanja wa kutosha na machaguzi ya mteja unayotaka. Nyingi zipo shallow na sometimes viwanja vinavyouzwa havina uhakika sana. So waweza anzisha platform kama hii ambayo itaweza ondoa gharama za kijinga za madalali lkn pia iwe ya uhakika kwa mteja kununua. Hapa waweza amua kujikita TZ nzima au ktk eneo lako ulipo tuu

19. Platform ya kukodisha nyumba - wanasema ukiwa Dar kupata Makazi ni kazi Kuliko kupata Kazi. Yaani swala la kupata nyumba ni ngumu sana. Wengi wana nyumba za kupangisha ila wanakosa wateja. Na wateja pia hawajui wapi wanaweza pata nyumba hizo za kupangisha na zinazoendana na bei zao na eneo wanalotaka. Embu tengeneza platform kama hii ambayo inaweza saidia watu na wewe umake money nzuri. Waweza anzisha na ikawa inajumuisha nyumba zote Tanzania nzima

20. Platform ya kuwekeza ktk ujenzi - Unajua ujenzi ni gharama na pia wengi wanapenda kuweka pesa zao ktk rela estate sababu ya uhakika na low risks. Sasa kwa TZ hamna platform ambayo watu wanaweza wekeza hela zao kidogo kidogo ktk real estate kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia mtandao. Admins na timu yake wanatafuta na kutengeneza projects za kuwekeza kujenga na kupangisha au kuuza, wanaanda kila procedures; kisha investors wanakuja kutafuta sehemu wanazopenda kuwekeza na kisha wana-deposit pesa zao popote walipo moja kwa moja mtandaoni. Waweza jikita kufanya projects kubwa za maghorofa au ndogo ndogo za nyumba za kupangisha mtaani. Hakuna fursa ya kuwekeza Dodoma mpya?

21. Duka la chochote unachotafuta - hapa unakuwa kama Alibaba au Amazon. Unaanzisha duka la kuuza bidhaa zote ambazo mteja anaweza hitaji. Unahitaji kuwa na stock ya kutosha. Hapa unaweza ingia partnership na wauza mbalimbali na waweza wanauza bidhaa zao humo. Mteja akiingia humo anaagiza chochote anachotaka

22. Jamiiforum new version - Jamiiforums hii tunayotumia ni nzuri sana hadi pia mimi hapa ninaitumia kupost uzi wangu huu. Lkn kuna mambo unaweza boresha ktk forum hii na uka-make money nzuri. Kikubwa ufahamu kuanzisha social network ni work kubwa maana kutengeneza network effect ni kitu hard ila kinawezekana. Social Networks zinaanza kidogo na kukua so kuna muda utahitajika.

Waweza anzisha JF ambayo ipo ktk version ya kitofauti zaidi mfano: inakuwa imejikita zaidi ktk qulity ya contents yaani thread zisizo na maana zinaondolewa; Jf ambayo imejikita kwa niche fulani ya watu labda JF ya mkoani kwako; Jf inayohusu mambo ya kina mama; JF ambayo yenyewe ni ya maswali na majibu (QnA) kama Quora; JF ya Afya zaidi na ina module nyingi za afya kama calculators za afya; Anzisha JF ya makabila mbalimbali ambapo forums zinakuwa ni makabila mbalimbali;…

Okey wewe pia waweza boresha swala la matangazo yakawa ktk mfumo wa kama FB ambapo mtu yeyote anaweza achilia Tangazo lake kwa kuanzia Tsh.5000/= na kwakuwa una watumiaji wengi kwa siku ukipata matangazo 1000 ya 5000 hiyo ni 5M kwa siku.

Pia waweza anzisha JF iliyojikita zaidi ktk Consultations yaani hapa nazungumzia kwamba foruma yako labda imejikita ktk 'Afya ya Mama na Mtoto' na unakuwa na madaktari kadhaa wazuri wa afya hizo ambapo wamama wanakuwa wanauliza maswali na majibu kupata kutoka kwa wataalamu wazuri ya ukweli na mama anajiunga uanchama kwa labda 1000 kwa mwezi ili apata ushauri wa haraka. Waweza angalia sekta nyingine kwa idea hii kama kilimo, ujenzi, biashara…

Anzisha JF ambayo unakuwa unakodisha Forums kwa watu wengine na makampuni ambao wanataka kutoa semina kwa watu wao kwa malipo. Yaani hapa unakodisha Forum kwa mwalimu fulani ambaye anataka kufundisha ujasiriamali, afya, kilimo… kwa wanafunzi wake; mwanafunzi analipia pesa kiasi ili aweze ku-access forum kujifunza. Zipo WhatsApp na Fb groups lkn zinachangamoto ya limit ya watu, ngumu kupokea malipo… Ingia FB uone wengi wanavyopata tabu kufundishia wanafunzi WhatsApp

23. TZ Online University - hapa nazungumzia kitu simple lkn kikubwa pia. Wewe binafsi unaweza anzisha platform ambayo mtu yeyote anaweza fundisha kitu fulani ambacho anadhani watu watakihitaji kukifahamu na kukijua. So mtu yeyote anaweza fundisha topiki labda: 'namna ya kufuga kanga wa mayai kwa taratibu za kitaalamu' au 'jifunze namna ya kufanya biashara ya Forex na ufanikiwe' au 'Jifunze namna ya kusimamia biashara zako vizuri na uweze kuongeza faida yako' au 'jifunze kuandika scrpit za muvi za kitanzania' au 'namna ya kuwa mwanasiasa ambaye unakubalika ktk jamii yako'… yaani ni multi-sector school. So inakuwa local univerisyty.

Msomaji anachagua na kutafuta somo ambalo angependa kujifunza, anafanya malipo hapohapo mtandaoni kisha ndio anaruhusiwa kujifunza. So ukiwa na topiki tofauti tofauti kama 5000 kutoka kwa waandishi kadhaa na ukapata wateja kama 100,000 kwa mwaka basi mtakuwa na effect kubwa Tz na pia mkatengeneza pesa nzuri

24. Online Secondary Schools Practicals - hapa ni idea nyingine nzuri. Kama umesoma sayansi utajua namna ambavyo wanafunzi wanavyohitaji kufaulu practicals. Ila kuna shule kadhaa zinakuwa na upungufu wa wataalamu au vifaa. Sasa anzisha platform ambayo mnaandika vizuri na kufundisha practicals. Hapa mna-rekodi video kabisa za practicals vizuri kabisa na kwa utaalamu ili mwanafunzi aweze kuelewa.

Halafu kwa gharama ndogo tuu mwanafunzi anajiunga ktk platform yenu na anaweza jifunza practical zote anazohitaji. Labda ada kama ni 5000 kwa mwezi na ukawa na wanafundi 10,000 hiyo ni 50M kwa mwezi. Hapa kwa yule ambaye hana maabara anaweza ingia ubia na shule fulani kuweza kutumia maabara yao na pia kuingia ubia na walimu kadhaa. Au kama ni vijana active basi mnaji-organise nyie wenyewe na kufanya kazi kwa bidii mpaka mtoboe. Mtakuwa wakipekee TZ

25. Online Pastpapers - hapa ni idea nzuri nyingine kama unavyojua namna ulivyokuwa unasoma ulikuwa unapenda sana pastpapers. Sasa hapa unakuwa na solved pastpapers za masomo yote ambayo mwanafunzi atahitaji. Na hapa concept nzuri ni mwanafunzi kujiunga unachama ili aweze ku-access pastpapers na majibu yake. Kama una jumla ya mitihani 1000 na majibu yake ikiwemo Necta za kuanzia miaka ya 1980 na majibu yake. So kikubwa ni kutafuta pastpapers na solutions zake.

26. Product review site - hii ni platform muhimu ambayo kazi yake ni kuchambua bidhaa mbali mbali ambazo makampuni mbalimbali yanauza. Bidhaa zinachambuliwa kiundani ktk pros na cons. Sasa hapa waweza chagua kujikita kwenye sekta fulani kama vipodozi au magari au vyakula au muziki au movie. Pia hapa waweza pia ukawa unauza bidhaa hizi kwa wateja na wasomaji wako maana utakuwa umewashawishi kuhusu bidhaa hizo. Kikubwa inabidi bidhaa zako ziwe ziwe na uchambuzi unaovutia

27. Wholeseller to retailer supplier - this is big idea ambayo niliiona kwa rafiki yangu kama opttunity kwake maana yeye anapata wateja toka vijijini ambapo anakuwa anauza kwa jumla, sasa yeye wateja wake wanatoka huko na kuja mjini kununua bidhaa. Sasa nikajiuliza kwanini hawa wateja wasiwe wana-order mtandaoni bidhaa wanazohitaji kisha yeye anawapelekea hukohuko kijijini? Au kila wiki anakuwa na safari ya kupeleka huko vijijini? Hapa hawa retailers watafurahi maana watapunguziwa complications za nauli na kusafiri. Hapa kama muuzaji waweza chagua location fulani kisha wewe ndio uwe unawapelekea bidhaa hizo.

28. China to Tanzania supplier - unajua kuna wauzaji wengi Tanzania wanapenda kununua bidhaa toka China, Sasa wewe kama mfanyabiashara wa mtandaoni unaweza anzisha platfrom ambayo hawa wauzaji watakuwa wanaagiza bidhaa toka china na wanaletewa moja kwa moja mpaka dukani kwake. Yaani swala la mteja kusafiri, kushughulikia Tax na bandarini na kila kitu wewe unamsaidia. Yeye kazi yake iwe kuagiza bidhaa na kulipia tuuu. Hapa utapiga pesa ndefu kama utakuwa umejitoa kuhakikisha platform inakuwa super

29. Kariakoo to Mikoani supplier - hapa unajua kuna watu wengi sana wa mkoani ambao wanapenda kununua vitu toka Dar. Sasa hawajamaa wanatumia nauli kubwa na hela ya gesti kulala Dar just kuchukua mzigo. Wengine hawajui vyema Kariakoo ilivyo mwisho wa siku wanapigwa na kudhulumiwa. Sasa akatokea mtu mbunifu aliyejitoa akaweza aggregate bidhaa nyingi za kutosha toka Maduka ya Kariakoo ambazo kila mtu atazitaka na kisha watu wa mikoani wakawa wanaagiza moja kwa moja mtandaoni na wanapelekewa moja kwa moja mpaka dukani kwao. Yaani hapa utawawewezesha hata watu wanaotaka kufunga mzigo wa 100K kuagiza toka Dar bila kujali hela yao ndogo. Hapa wauzaji wengi watakupenda kwasababu hata kwa hela ndogo anaweza pata mzigo. Nilitoa mfano juu kuwa FB watu wanaipenda sababu unaweza weka tangazo hata la ~dola 1, lkn huwezi kwenda ITV ukatangaziwa tangazo la 2500/=

30. Platform ya usafirishaji mizigo toka Dar kwenda Mikoani - Najua kuna watu wengi ambao wanapenda kusafirisha mizigo yao toka Dar kwenda mikoani na vice versa. Sasa wasafirishaji wapo ila hawafahamiki sana. Wewe unaweza jikita kuwezesha watu wenye mizogo kusafirisha kwa gharama nafuu kwenda mikoani. Waweza chagua niche fulani labda vifaa vya ujenzi au mavazi au movies… kisha ukawa na platform ambayo mtu anaweka-order ya mzigo wake kusafirishwa then mnaufuata na kupeleka anakotaka

31. Platform ya kusupply kwenye magenge - hii ni idea nimekuwa nikiifikiria na kama wiki kadhaa niliona kuna wauzaji magenge wanakwenda Buguruni wananunua vyakula na kisha wanaacha mzigo kwa kirikuu then kesho mzigo wanakuletea ulipo kwa kutumia kirikuu yao. Nilimuuliza masswali kirikuu 'Mteja anaagiza bidhaa fulani kisha nyie ndio mnamletea?' akasema 'la hasha, Mteja just anakuja Buguruni kununua bidhaa then anatuachia sisi then tunampelekea alipo'. Sasa nikasema kwanini mteja asiwe just aliko anaagiza bidhaa moja kwa moja then nyie mnampelekea alipo? ; anyway hii ni fursa ambapo wewe unaweza ifanya kisomi na ukawa supplier wa magenge yaani wenye magenge wana-order mtandaoni halafu wanapelekewa moja kwa moja walip0.

Yaani hapa wewe huwi na mzigo bali unakuwa unaubia na wauzaji wa mashambani na walioko Buguruni then unakuwa na ubia pia na wenye Kirikuu ili wakusafirishie mzigo kwenda ambako wateja wameagiza. Unaweza ukawa na route kadhaa ambazo wewe umeziweka vyema na pia hakikisha Quality na Quantity ya bidhaa inakuwa ile ambayo mtaja ameagiza. Unajua watu wenye magenge wanapiga profit percentage kubwa kuliko duka la bidhaa? Ila wanapata changamoto ya mzigo kama usipouzika vyema unaweza lala maybe kuoza na kuharibika. Sasa kama wewe ni uhakika kufanya supply kila muda bila yeye kuchoma nauli basi watakupenda kwelikweli

32. Duka la kuuzia bidhaa za kijasiriamali - Siku hizi kuna wanawake na vijana wengi sana wanatengeneza bidhaa zao wenyewe. Embu fikiria mabatiki, mashati, nguo za kutalizi, sendozi, viatu… uje kwenye chakula kuna dagaa za kukaanga, bites, mango pickel, ubuyu, kashata, juice packed, karanga, nuts… Sasa hawa jamaa unaweza waweka katika platform moja ambapo wataweza uza kwa uhakika.

Mfano unaweza weka wajasiriamali wawe wanauza bidhaa zao kwa jumla halafu wauzaji wakawa wana-weka oda ya bidhaa kiasi fulani then wanapelekewa walipo. Inaweza ikawa jumla na rejareja. Sasa wapo watu wengi ambao wanappenda bidhaa za kijasiriamali maana zina aina fulani ya ladhaa na sifa adimu. Pia wapo watu wanopenda Made from Tanzania. Sasa hapa utakuwa umetengeneza platform yenye sifa na tija. Pia utakuwa umewasaidia wamama wengi kuwa na soko la Uhakika maana wao watahakikisha uzalishaji wa bidhaa unakuwa wa uhakika na bora zaidi kwa haraka maana soko wanalo toka ktk plaftrom yako. Do this guys.

33. Platform ya kuuza picha TZ - unajua watu wengi siku hizi wanahitaji picha kwajili ya matangazo na pia kuweka mitandaoni. Sasa kukiwa na platform ambayo waweza wawezesha artists mbalimbali wakawa wanuza picha zao nzuri kwa njia ya Downloading utakuwa umefanya kitu cha kipekee. Hapa utapaswa uangalie vyema soko na wateja wako ambao umewa-target

34. Platform ya any documents - hapa the idea ni kuwa na aggrgative platform ambayo people wana depposit documents mbalimbali za kutosha. Yaani idea any trending document watu wanaweza ipost hapo ktk platform. Documents za miaka ya nyuma, magazeti, mitihani, mikataba,…. So kama platfrom inakuwa inajumuisha documents za aina mbalimbali za Tz basi watu kibao watakuwa wanakuja ktk platform kutafuta documents fulani ambayo wanajua wataipata hapo.

Just imagine umeweza motivate watu waweza upload documents nyingi za kutosha ambazo toka sekta zote ambazo maybe zimefika kama 5M documents tofauti tofauti; so hiyo itakuwa Precious Repository ambapo watu watakuwa wanakuja kutafuta documents ambazo wanaitaji. Wewe waweza make money kwa kuweka uanachama kwa wanaotaka ku-access documents hizo . Labda kuaccess documents 0 - 10 kwa mwezi ni bure, 10 - 1000 kwa mwezi ni Tshs. 5000/=. Hapa utapata watu walio serous kulipia. Another version ya hii basi waweza amua kujikita kukusanya documents za fani fulani labda Law School au Walimu au Wanafunzi au Engineers au Magazeti ya miaka ya nyuma …

35. Used car eDuka - najua siku hizi kuna magari mengi ambayo watu hapa Tz wameyatumia na wanataka kuyauza. Sasa wewe mjasiriamali waweza jipanga kwa nguvu na uhakika ukawa unamiliki plafrom ya kuuzia magari mtandaoni. Yaani nikitaka kuuza gari au pikipiki au bajaji basi nakuja mtandaoni pako nachapicha vizuri gari hilo ninalotaka kuuza. So wateja watapenda kama wanapata uhakika wa kupata muuzaji kwa urahisi na wakawa na uwanja mpana wa kuitafuta gari wanalotaka kwa urahisi, kwa bei wanayotaka, aina, model… Sasa itapaswa ujenge TRUST ktk platform yako ili watu wawe na uhakika kwamba wakilipia bodaboda ya 700k basi watapelekewa walipo na itakuwa katika conditions zilezile zilizoaionishwa mtandaoni.

Hapa waweza tengeneza mawakala kila mtaa ambao wanaweza kukusaidia kukusanya bidhaa ambazo zinauzwa vizuri na kwa uhakika. Yaani ukiwa na platform hapa TZ ambapo mtu anaweza pata gari used la uhakika full legal la 3M, 5M au mtu anaweza pata bodaboda ya 400K, boxer ya uhakika ya 700k basi mtu wangu utapiga profit. Inakuwa clean platform iliyo professional ambapo mtu anaweza tafuta model na specifications anazotaka kwa uhakika. Duu tufanye kazi kwa bidii. Hapa unaweza ongezea kipengere cha mteja kulipa kwa awamu labda miezi 3 akianza na 50% halafu iliyobaki alipe ndani ya miezi 3 na akimaliza basi anapelekewa gari lake. Ni idea tuu

36. Platform ya kukodisha gari za harusi - hapa patamu. Harusi zinatumia bajeti kubwa kukodi magari. Sasa kupata gari ni mpaka uangalie kwa huyu na yule na yule. Why old system? Vijana wa sasa hapa changamkieni fursa kwa kuanzisha platfrom ambayo unakusanya magari yote ya harusi ya aina mbalimbali na specifications zao. Halafu mteja anaingia ktk platform anatafuta gari analotaka kulingana na specifications zake then anachagua anataka kukodi kuanzia lini mpaka lini kisha anafanya malipo mtandaoni then siku hiyo anayoitaka analipata. Sasa kama gari limekodiwa kwa 400K na wewe mwenye platform unapata commission ya 20% ambayo ni 80K na kwa mwezi ukafanikiwa kuwasaidia watu kukodi magari 200 basi utakuwa na revenue ya 16M. Inakuwa vipi ukapanuka mikoa yote?

37. Platform ya kukodi vifaa vya harusi - hapa wale watu wa urembo na ujasiriamali. Magauni, suti, viti, maturubai, viatu, kumbi, magari… platform yako inakuwa na lengo la kukodisha vitu hivi ktk ubora na uhakika na unafuu zaidi. Kwanini mtu anunue gauni la 800K wakati anaweza kuja ktk platform yako na akakuta magauni 100 tofauti tofauti ambayo anaweza chagua na kukodi kwa 150K pekee? Utapata wateja. Unafanya ubia na ma-saloon wakusaidie kupata wateja na inventory pia

38. Platform ya kuuza keki - simple idea but very realistic and powerfull. Hapa unakuwa na wapikaji kibao wa keki. Wanaposti kwa utaalamu vyema aina na staili mbalimbali za keki wanazoweza kumtengenezea ikiwemo specifications za kutosha kama recipes na kila kitu. Halafu mteja anaweza kuja na aka-order keki kwa mpishi fulani ili tarehe fulani aipate. Ni simple but itakuwa na hobbist wengi. Kama ikawa na keki mbalimbali kama 200 halafu mteja anachagua staili anayoipenda yeye kisha analipia then baada ya siku analetewa alipo ikiwa imefunashwa vyema kulingana na specifications alizochagua yeye mteja.

39. Platform ya kuuza maua na miti ya matunda - ni ngumu sana hapa TZ kutafuta ua fulani. Na mauza ni gharama. Sasa ukawa na utaalamu na hobby nzuri ya mauza then unaweza shirikiana na wakulima na wauzaji wengine ukaanzisha eDuka lenye maua kibao ambappo mteja anaorder na kupelekewa ikiwezekana na kapindiwa. Hapa kama utakwa umeweka smart biashara yako basi majumba mengi watakuwa wateja wako

40. Platform ya kuuza gadgets - unajua siku hizi wadada kwa wakaka kwa watu wazima wanapenda tech gadgets kama smrt whatch, earphones, games consoles, beauty gadgets, smart pens, smart miwani… waweza jikita kuagiza bidhaa hizi nje na ukawa unaziuza online TZ na mtu analipia na kupelekewa alipo. Waweza weka muda kuwa akiiagiza anasubiri wiki 2 mpaka itoke nje na ije hapa Tz.

41. Platform ya kuhire wadada wa kazi - Kwanini wadada wa kazi wasiwe wanafanya kazi masaa kadhaa kwa siku kadhaa? Sometimes hakuna ulazima wa kukaa na dada wa kazi. Unaweza anzisha platfrom ambapo mtu ana-hire mdada wa kazi kwa siku fulani na kwa masaa kadhaa kisha analipia pesa mtandaoni na then siku hiyo mdada ataenda kufanya kazi ambazo zimeainishwa ktk mtandao na mteja.

Hii inaweza saidia kuongeza ufanisi kwa wadada wa kazi maana watakuwa wanafanya kwa kujituma ili siku nyingine apate hiring. Hapa sasa lazima mtu aki-order basi anapata mdada ambaye yupo maeneo ya karibu nayeye ili kusave nauli. Lkn hii imekaa ktk economic sharing model hivyo waweza maximize utendaji wa kazi na hivyo kuwaongezea wadada mishahara mizuri na pia kupunguza gharama za kulipa kwa boss. Idea ngumu ila very possible. Na unaweza order dada ambaye anaweza fanya kazi fulani na mwenye vigezo fulani

42. eDuka la kuuza nguo tuu - nilipata tabu kutafuta jeans aina fulani niliyokuwa naitaka. Why pasiwe na specialized eduka ambapo mtu watafuta kitu utakacho? Unatafuta kadeti ya aina fulani size fulani kuliko kuanza kuzunguka Mwenge nzima.

43. eDuka la kuuza nguo za ndani - hapa pakubwa na penyewe. Nguo hizi zipo nyingi na staili na specifications mbalimbali. Ukiwa na aina 1000 za chupi za staili na specifications tofauti tofauti basi wapo wadau wengi wata-order

44. Gift ordering and sending Shop - wapo watu wanaopenda mpaka leo. Jamaa ana baby wake na anataka kumpa surprise basi aningia ktk eshop yako anachagua zawadi nzuri kadhaa ambazo anajua baby wake atafurahi sana. So anaweka address za mpokeaji wa zawadi, maneno ya kuandika ktk kikaratasi cha zawadi, ifungweje na lini iende (labda birthday yake) kisha anafanya malipo ya zawadi mtandaoni halafu siku hiyo zawadi inakuwa imefika kama surprize. Hapa utapata order nyingi sana za watu wakizepeleka zawadi ktk machuo :) . So kama mtu anahitaji zawadi basi hatakuwa tena anapenda kwenda kariakoo kutafuta duka la zawadi, ila atakuwa anaingiazawadi

45. Onlne Tshirt Printing shop - hapa kwa mtu anayetaka kuuza Tshirt printed basi unaweza tumia aina hii ya duka kuweza kuuza customized tshirt. Hapa mteja anachagua maneno na logo yake binafsi ya kuweka ktk Tshirt halafu anafanya malipo mtandaoni kisha anaandaliwa Tshirt hiyo then anapelekewa alipo. Unaweza badili Tshirt ikawa shuka, banners, vifungashio….

46. Platform ya kuuza biashara - unajua kuwa kuna watu wengi ambao hawapendi kuanzisha biashara toka mwanzo? Kuanzisha biashara ni kitu kigumu na kinahitaji akili na maarifa. Ukiweza pata biashara ambayo ipo tayari inafanya kazi na pia ina wateja tayari na inaiingiza faida na mtu anaiuza basi ni bora uinunue hiyo na kisha uiboreshe. Sasa waweza andaa platform ya kuuza biashara mbalimbali na watu waweza tafuta biashara wanayotaka then wazinunue

47. Platform ya kubadilishana mali kwa mali (Barter trade) - unajua swala la kupata pesa ni gumu kama ugumu ulivyo? Unaweza ukawa na mali lakini ukakosa pesa ya kufanya kitu fulani. Unaweza ukawa na gari lenye thamani ya 10M na unahitaji huduma fulani ya 10M lakini ukakosa sababu tuu huna cash money. Swala la kuwa na mali ni jingine na swala la kuwa na cash ni jingine. Kubadili mali kuwa cash mara nyingi ni mpaka uuze, sasa kuuza ni kazi ngumu! Basi anzisha platform ya kukutanisha watu kubadilishana bidhaa na bidhaa au huduma na huduma au bidhaa na huduma. Hapa wadau wanakuwa wanaposti na kukubaliana mbadilishano wa bidhaa hizo, hii itasaidia wengi maana hali ya uchumi inaweza changi pesa cash kuwa adimu lkn bado watu wanazo mali. Wewe mmliki waweza ukawa unachaji pesa kiasi fulani kumruhusu kuposti bidhaa au tangazo lake liweze onekana juu zaidi au kupata huduma za ziada kibiashara.

48. Mtandao wa kuchangiana matibabu - hapa concept ni cloud-source; yaani labda waweza jikita ktk mambo ya afya na ukawa unasaidia watu ambao wanahitaji mchango wa kifedha ili kufanyiwa opertions na kupata huduma ambazo labda ni ghali sana kugharamia mtu peke yake; Waweza ukawa unajikita kusaidia watoto wanoishi mtaani na wanahitaji huduma fulani kiuweza kujikimu na kupata msaada wa kimaisha. Unaweza tumia platform ya Cloud-funding ambapo posti ya mtu anayehitaji msaada inaandaliwa vyema na kuchapishwa kisha watu ambao wanakuwa wameguswa kumchangia mgonjwa wa upasuaji huo watachanga kiasi chochote ambao wameamua wao.

Labda mgonjwa anahitaji Tshs. 20M kusafiri kwenda India kupata matibabu lkn yeye hana, basi wakitokea watu 10,000 wakachanga kila mmoja Tshs. 2000 basi huyu mgonjwa anasaidiwa kiafya. Embu imagine ni watu wangapi ambao maybe wamefariki kwa kukosa huduma za ghali kama hizi? Lkn humu tuu JF tupo zaidi ya 500,000 ambapo labda nusu ya watu humu wakachanga 1000/= tuu inapatikana kama 250M ambazo zinaweza saidia wengi. So kwanini tusiunganishe nguvu ya pamoja kutatua matatizo kama haya kwa kutumia mtandao?

49. Mtandao wa ku-wekeza ktk idea za kibiashara - hii ni kitu muhimu sana ktk nchi yetu. Watu wengi wanshindwa kufanya mambo makubwa kwa sababu tuu ya kukosa capital ya kutosha. Sasa mdau mmoja mwenye deep conviction akajitoa kuanzisha mtandao ambao idea mbalimbali za kibiashara zinapostiwa kistaarabu na kiutaratibu wa kisomi vizuri halafu wale watu ambao wameipenda idea ya kibiashara hiyo wanaweza changi mtaji ili tuu idea hiyo ya kibiashara iweze kufanikiwa.

Sasa watu wanaochangia wanaweza pata zawadi just kidogo kwa kuchangia capital hiyo. Pia inawezekana labda kunakuwa na swala la kupeana share ktk biashara hiyo, nalo linawezekana. Wenzetu wazungu wanatumia platform kama hizi kuchangisha mabilioni ya fedha just kuwezesha wazo fulani zuri la biashara lifanikiwe. Hapa mara nyingi wachangiaji wa pesa hizi huwa wanakuwa hobbist wa hicho kitu (games, movie production, gadgets, restaurants food, Tv programme…)

50. eOffice ya ushauri kwa gharama nafuu kwa wakulima = hapa namaanisha kuwepo kwa sehemu ambayo wakulima wanaweza uliza maswali wataalamu na kujibiwa. Najua zipo forum za bure ila hazina ushauri ulio deep sababu ya kuwa wataalamu hawapo committed sabau hakuna malipo

51. Men/Ladies/kids subscription box - hii ni biashara nzuri sana sababu ukisha mpata mteja basi unakuwa na uhakika wa malipo yake kila baada ya muda fulani. Mteja anajiunga ktk club yenu mtandaoni ambapo akisha jiunga kila baada ya muda fulani anakuwa anapelekewa bidhaa fulani ambayo wewe kama admin unakuwa umeandaa muda huo. Sasa kwa mfano kwa Ladies: labda club ya urembo ya wanawake ambapo kila mwezi anapelekewa vipodozi adimu na vitu vingine vya urembo na ada ya kujiunga club hii inakuwa labda 15k kwa mwezi.

Au kwa wakaka inakuwa club ya wanaume ambapo kila mwezi wanakuwa wanapewa surprise ya vitu vya kiume kama gears, electronics, games, nguo, movies, books… Kwa watoto inaweza ikawa kila baada ya mwezi wanapelekewa majumbani mwao toys, games, books, food, movies… Concept hii unaweza iweka ktk sekta yeyote ile swala la kuhakikisha wateja wako wanakuwa excited na vitu utakavyokuwa unawapelekea.

Na pia ni lazima kuhakiksiha kuwa unafanya kitu ambacho kwa wateja wako ni kama hobby fulani. Sasa kama ktk 15K wanayolipia wewe unapata faida ya Tshs. 3000 na ukawa na club member kama 10,000 basi kila mwezi utakuwa unapata 30M. Kitu kingine cha kuhakikisha ni kwamba mtu akijiunga ktk club basi vitu atakavyopata viwe amepata ktk unafuuu zaidi kuliko akinunua yeye dukani. Waweza anaglia concept hii ktk vyakula, vitabu, underwear (kila mwezi anapelekewa chupi ya size yake), movies, exams…

52. Paid articles/news/notes - hii ni platform ambapo kunakuwa na makala adimu ambazo fiki unajua kuna watu ambao wanapenda kuzisoma. Zinaweza kuwa hadithi, ripoti, uchambuzi, notes, habari... lkn ili mtu aweze isome makala hiyo inapaswa ajiunge uanachama au alipie kiasi fulani kisha aweze ruhusiwa kusoma. Hakikisha kila mara unaongeza makla adimu na pia wateja wako hawachoki kuja kusoma makala zako.

==> Ushauri ni kwamba mjipange kama group lenu la MASTERMIND PEOPLE kisha mchague Idea mnayohitaji ku-execute vyema kisha muifanye kwa kujitoa
==> Kwa wale watakao hitaji kuandaliwa ONLINE BUSINESS PLATFORM hizi Pia
Waweza andaliwa kwa ada 10M (or Exchange with a Good Car [IST, RAV4 3 doors]) ikiwa na module zote zinazohitajika biashara kufanya kazi vyema mtandaoni (inventory, marketing, payment, customer service, shipping, multi-seller, referral marketing, social sharing, testimonial, forums, blogging, online advertising, user profiles, massaging system, social interaction, coupons, installment payment, delivery person, reviews and ratings, Question and Answers, membership system, support tickets, knowledge base, comparison system, customer wishlist, translation, users role levels, reward and incentives, subscription, discount, searching & filters, booking, preorder...) (+255-657-685-268 WhatsApp)
Unataka 10M kwa ajili ya kumfungulia mtu platfom? hapa ndo naamini kwamba ukiitwa kwenye fursa jua wewe ndio fursa yenyewe
 
Mkuu Safi sana Kwa ideas hizi

Ubarikiwe
 
Somo zuri ,,,,

Lkn kwa Tanzania hii bado ,!

Ni watu wangapi wana access ya mtandao ? Wanatumia simu janja ? Ni wachache, na walioko na simu janja wengi wao hawajui kuzitumia vyema ! Anajua kupiga, kupokea, kutuma msg tu!!!
 
Tozo mpya za Miamala zitumike kutengeneza Walipa Kodi kwa hiari
 
Niko online marketing mwaka wa 5 sasa, vingi ulivyoandika ni possible, challenge ni kufanya watu wakujue. JF hii ilianzishwa 2006 Leo ina members almost 5,000 licha ya umaarufu wake ikiwemo kesi za kina Melo wakitutetea. Ok. Kuna formula nayotumia ,ntakupa ya kupata wateja wengi bila kuwa na followers, subscribers Wala likes.
Hilo tatizo linatatuliwa na marketing.
 
Haya mambo yooooote yanawezakufanyika kwa platform moja yenye vipengere tofauti tofauti vya hizo biashara.

Mteja au mtoa huduma anaingia kule anapohusika tu.
Tunakoelekea tutalazimika kuendesha mambo kwa huu mfumo, hakuna namna. Teknolojia inabadili mfumo wa maisha na namna tunavyofanya kazi.

Hongera kwa bandiko zuri.
This is the future mkuu. Tazama pia freelancer sites kama upwork, fiverr na zinginezo zinavyorahisisha ufanisi wa kazi mbalimbali
 
Wakuu kuna fursa ya mtaji huku wa Tsh 50-200m huku. Deadline ni 31 Julai 2022

IMG-20220701-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom