Aina 15 ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na kuweka mwili sawa

dr_seifu

New Member
Dec 20, 2021
1
10
Aina 15 ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume,na kuweka mwili sawa.

1.Tende.

Katika kila gram (100) ndani ya tende kuna virutubisho kwa asilimia kama ifuatavyo.

Chuma (iron). 5.50ppm.

wanga (cabohydrate) 78.8%.

Nishati (energy) 317kcal.

Hamirojo (protin)2.5%.

Mafuta (fat).0.4%.

Kamba kamba (fiber)4%.

Madini 2.1%.

Unyevu nyevu (moisture)15.3%.

Fructose 27%.

Grucose (Sukari) 35%.

Faida nyingine za tende.

1.Huongeza damu ukichanganya na maziwa

2.Husaidia kuzalisha manii kwa wingi

3.Huongeza nguvu za kiume.

4.Huzidisha hamu ya tendo la ndoa.

2.Zabibu.

Huongeza sana nguvu za kiume,
wengi hupenda kuyaita "viagra"kwa sababu ya ufanyaji kazi mwilini. husaidia mzunguko wa damu,pia huondoa cholesterol

3.Chocolate.

Husaidia kuongeza stamina,kwa sababu ina viambato vya phenylethylamine na Alkaloid

Phenylethylamine.
hupelekea kujisikia vizuri.

Alkaloid.
Huongeza stamina wakati wa tendo la ndoa.

4.Ndizi.

Ni chanzo kikubwa cha vitamini B,ambacho ni muhimu katika tendo la ndoa,ina kimeng'enyo cha bromelan ambacho huongeza Ashk wakati wa tendo la ndoa.pia huongeza stamina.

5.Tangawizi.

Husisimua sana mzunguko wa damu.tangawizi imekuwa ikitumika sana katika maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.

6.Tunda la komamanga.

Ni aina ya matunda yenye rangi nyekundu na muonekeno kama apple.husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea uwezo na hamasa wakati wa tendo la ndoa na kupoke hisia kwa urahisi.

7.Mtini.

Ni matunda yenye kiwango kikubwa sana cha amino asid,ambayo ni kiungo kikubwa cha Kuzalisha homoni mwilini.

8.Karanga.

NI Chanzo kikubwa sana cha kurekebisha Protini mwilini,pia husaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu,na kusaidia kuzalisha homoni ambayo ni muhimu kwa tendo la ndoa.

9.Asali.

Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu za kiume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kutibu uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji kwa wanandoa. Tumia vijiko 2 asubuhi na 2 jioni.

10.Kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu kina Allicin, kiambato kinachosaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu.Pia Hupunguza tatizo la damu kuganda katika mishipa ya damu

11.Samaki aina ya pweza na chaza.

Hutoa madini aina ya zink ambayo huzalisha vichocheo vinavyoleta msisimko kwa wanandoa.

12.Ugali wa dona.

Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya na kuongeza nguvu za kiume.

Ongeza nguvu za kiume kwa kula ugali wa dona kila siku.

13.Maji.

Maji huchukua karibu asilimia (70%) katika mwili wa binadamu.

Ambapo;

Mifupa ina karibu asilimia (25%) ya maji.

Damu ina karibu asilimia(85%) ya maji.

NB.Damu ndio husababisha uume kusimama.

Misuli ya mwili ina karibu(75%) ya maji.

Ubongo una karibu asilimia(85%) ya maji.

Kunywa maji kila siku kabla ya kusikia kiu,Ikiwa mwili utakosa maji utajikopa maji toka katika ubongo,na wewe utapatwa na ‘kichwa kizito’ au kichwa kuuma ambacho kinaweza kupelekea maumivu ya kichwa.

unywaji wa maji kwa wingi hutusaidia kuweka sawa mzunguko wa damu pia huongeza akili na uwezo wa kufikili.

Kwa matumizi bora ya maji kunywa walau glass 8 kwa siku, na kunywa glass 1 ,kila unapoenda kulala.

14.Tikiti maji.

Lina vitamin A ambayo huondoa sumu mwilini,vitamini C huboresha kinga,hukinga uharibifu wa seli,husaida ubongo kufanya kazi vema,husafisha damu,na kukinga shinikizo la damu,

Hutibu nguvu za kiume ukila na mbegu zake.

15.Mbegu za maboga.

Huondoa msongo wa mawazo, Hutibu matatizo ya ngiri ,huondoa cholestrol,Zina madini ya zink ambayo ni muhimu kwa Mwanaume,zinaongeza wingi wa mbegu za kiume (sperm count), ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona kazi yake.

images%20(2).jpg
 
Vinatumika kwa pamoja au unachagua kadhaa au kimoja unadili nacho?
 
Sema gym ni msaada mkubwa sana. Kula vizuri na pia nenda gym ukafanye mazoezi ya kutosha na sio kubeba machuma tu. Mimi toka mwaka Jana mwishoni nimeanza kwenda gym nguvu za kiume zimeimarika sana
 
Wavulana wa dar mnaitwa huku

Mkoani jembe linatosha sana kuongeza nguvu zote unazozijua wewe
 
Back
Top Bottom