AIDS DAY: LUKUVI atwikwa zigo la Ukimwi SHINYANGA

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
AIDS Day Shinyanga

Awali ilitarajiwa kuwa JK kama mgeni rasmi, baadaye kidogo akakabidhiwa Mtaalam wa Nyuklia nae kama akatolea nje hivi kisha akakabidhiwi Pinda naye sijui kakumbwa na masahibu gani sasa ni Lukuvi.

Naomba nisitie chumvi zaidi ya kujiuliza hizi siasa za Tanzania na mapambano dhidi ya matatizo yanayomzunguka mtanzania.

Hatusikii wakiahirisha na kukacha shughuli za kufungua mahoteli.

Takwimu kuhusu Ukimwi kwa sasa zinatisha baada ya kuwa ugonjwa huu ni kama umezoeleka huku taasisi zilizokuwa zinafaidika na mabilioni ya wahisani zikikumbwa na baridi baada ya fuko la fedha kujali zaidi ushoga kwa madai kuwa vita ya ukimwi sasa inaeleweka vema na kwamba kila mmoja anajua nini la kufanya kujilinda na maambukizi mapya.

My TAKE:
Ukimwi ni kama umezoeleka na hakika hakuna hata anayeuogopa tena, kama kuna aliyeko huko kambarage atupe detil kwa wanayojiri...Nimeona kama Star TV wapo Live japo wamepotea ghafla sijui symbion itakuwa imewatenda au kitu gani.

ADIOS
My take:
 
mkuu kama kawaida yao
issue haina maana kwao na kwa watanzania
halafu hakuna ulaji sana na kimataifa haina tena deal maana mshiko kila siku unapungua
 
suala la ukimwi kuzoeleka lisichukuliwe kwa mtizamo hasi pekee, UKIMWI ukizoleleka watu wagonjwa hawatanyanyapaliwa, watu wengi watajitokeza kupiwa na watakaogundulika watapewa dawa ambazo zinapunguza maambukizi -mtu anliyeanza kunywa dawa uwezekeno wake wa kuambukiza unakuwa mdogo zaidi kuliko mwathirika ambaye hajaaanza. Hayo yote yanatokana na kupungua kwa nyanyapaa
 
Back
Top Bottom