Uchaguzi 2020 Aidah Kenani (CHADEMA) wa Nkasi Kaskazini amuangusha bwana Ally Kessy (CCM)

Maeneo mengine, wasimamizi aidha wamepewa maelekezo au wamekuwa na hofu ya kutumbuliwa, wameishia kudhulumu ushindi wa wagombea.

Yaliyotokea yanaenda kuleta chuki ya muda mrefu katika jamii.
Wananchi ngazi za majimbo na kata na vijiji wanajua ni mgombea gani anakubalika.

Viongozi wa Tume wapo Dar na Dodoma lakini wasimamizi ngazi za chini ni watumishi wa Serikali, wengi ni wateuliwa na ni makada wa chama na wasaidizi wa ngazi za kata na vijiji walikuwa wanapewa maelekezo bila viongozi wa Tume ya Uchaguzi(Taifa) kufahamu kuwa ngazi za chini wasimamizi hawapo huru katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa uchaguzi.

Kinachofuata ni maisha ya kinafiki, chuki na visasi dhidi viongozi na wananchi.
Ukweli watu wengi hawajajitokeza kupiga kura alafu wanalalamika CCM kushinda jamani kura moja ina impact sana.
 
Mkiwa na kiongozi mkuu mnafiki na zao la shetani, waongozwa wote mtajuta. Sahizi kuna watu wanafurahia lakini waja wakati ambao wanaofurahia watajuta kuliko wanaoumia leo.

Nchi ipo katika laana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu. ..watu wanafurahia Ila hakika tutakuja kulia na kusaga meno wote hapo baadae.
 
Huyu mkurugenzi hajipendi mkuu alitoa maelekezo haya ' yaani nikuteue mimi mshahara nikupe .imi gari mimi alafu kwenye uchaguzi ukamtangaze wa upinzani. Ndio kilichotendeka hata tahira wameona
 
Hawakusahau wameanza kujistukia.
Wamepanga kumtoa kafara huyu mwenye mdomo mchafu mzee ili izime hali hii kuonesha kuwa unaona huyu mtu maarufu kwetu lakini kashindwa kwa kura alfu 1 ni mambo ya kitoto sana huko kwingine ni mwendo wa 80% ujinga mtupu. sitopiga kura tena maisha yangu yote mpaka siku nione kweli kura yangu ina maana kwa sasa upuuzi tu.
 
Namuombea huyu dada apewe usirikiano na CHADEMA, laa sivyo atakuwa na wakati mgumu sana bungeni. Kutimiza majukumu yake ya kibunge na kufuata matakwa/masharti ya Chama.

Ushirikiano wa kufanyaje? kumsindikiza bungeni au? ilipaswa asiende hata mmoja
 
Na hiyo ndio sample ya uchaguzi wa ukweli ikiwa katika ngome yao ya Nkwasi wamepoteza wataweza vipi kulinda au kushinda kwenye ngome za wapinzani. haingii akilini mimi nachukulia hiyo ndio hali halisi kilichotokea kwa huyo mzee ni kama kusema CCM wameshidwa Dodoma lakini wameshinda Pemba.
 
Back
Top Bottom