Aida Khenani: Nilipewa laana nyumbani kisa CHADEMA. Nitamkumbuka Hayati Magufuli kwa uthubutu wake

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
6,178
3,142
Mbunge pekee CHADEMA wa kuchaguliwa, Aida Khenani(Nkasi Kaskazini) akihojiwa na Clouds Media amefunguka yafuatayo.

Kwa bahati mbaya mama yangu hajui kabisa siasa anapenda sana kusali muda wote, mashangazi zangu ni CCM waliobobea, walikuwa wakinitolea laana, ili kulinda ndoto yangu nilihama nyumbani.

Jambo ambalo nitamkumbuka Hayati John Magufuli ni uthubutu wake haijalishi hicho kitu kitakuwa na athari kiasi gani lakini aliamini hayo yote yanawezekana kurekebishika, natamani na Mama Rais Samia Suluhu Hassan awe na uthubutu.

Khenani.JPG
 
Umesema kweli, hiyo ndio legacy aliyotuachia Magu. Viongozi wengi watamuiga katika hilo.

Na kubwa zaidi katika hayo ni kuteuwa watu wasiokuwa katika chama kwa muda mrefu au hawakuwa katika ngazi yeyote ya uongozi. Hili ni muhimu sana na naliona kwa Rais Samia SH vile vile. Uchaguzi wa makamo wa Raisi P.

Mpango ni mfano tosha, ndio maana hakuna aliyehisi kuwa mpango angeteuliwa kuwa makamo wa Rais. Majina kama Nchimbi and the company yalitawala, lakini mama kaachana na yote hayo.
 
Rais Samia asije akamwamini Mbowe ni muongo muongo sana, aliangushwa na konyagi nyumbani kwa hawara Joyce Mkuya alafu akalitangazia taifa eti amepigwa na wasiojulikana.
Usisahau yeye na wenzake walivyojipiga bomu Arusha wakati wa Kikwete na kusingizia serikali.
 
Kinuju,
Hawa ndio zao, wanacheza mapichapicha yao alafu unaskia wanaanza kuuliza polic flani yukowapi.

Usanii mtupu.
 
Wabunge wakiwachiwa huru kumbe wana hekima na busara, kina mijitu huwa haina akili ikianza ujinga hao wabunge akili zao zinapotea kabisa
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom