Aida Khenan: Kama sikususia Uchaguzi siwezi kususia matokeo, CHADEMA iliniteua nikashinde na siyo kushiriki Uchaguzi

Swala la kushiriki au kususa uchaguzi ni suala la chama husika na sio suala la mgombea mwenyewe binafsi.

Kama Chama husika kikisusia matokeo ya uchaguzi, mgombea hana hoja wala mantiki ya kuyapokea hayo matokeo. Kwanini? Nafasi ya ugombea kwenye uchaguzi hapa Tanzania ni mali ya chama husika na sio mtu anayegombea.
 
No, she's right. Aligombea ili ashinde, na ameshinda, kwanini akatae ushindi? Na ametoa ushauri mzuri kuwa chama kifuate utaratibu wa kudai haki katika yale maeneo yenye dosari. Zifunguliwe kesi za uchaguzi kwa kutumia ushahidi uliopo. Wakifungua kesi majimbo yote, na zikathibitishwa mahakamani, itasaidia pia kama uthibitisho wa dosari kwenye uchaguzi wa rais japo hauhojiwi mahakamani.
Upande wa Rais mimi naona Hauna shida sana mana Rais ni mtu mmoja tu anayechaguliwa na kwa vypvyote ni lazima mmoja ashinde na kwa sheria na katiba ya Tanzania aliyepo madarakani anagombea akiwa na kamalaka yote. Anaweka nguvu zote za kidola kumrudisha madarakani bila kuulizwa na mtu hivyo hawezi kushindwa kamwe labda kwa uwezo wa Mungu.

Tatizo lipo kwa wabunge na madiwani kama kweli itathibitika kuwa kuna Wakurugenzi walioharibu uchaguzi kutangaza walioshindwa na kuwaacha walioshinda kwa kweli hao sitawaombea mema kwa Mungu na kwa wanadamu. Hao ni bora wakaonja joto la jiwe na wasione wema wa kutenda uovu.

Hao walibainika inanidi washitakiwe kwa uhujumu Uchumi mana wamelisababishia Taifa hasara kubwa sana . Lakini pia ni vyema wananchi wakagawana mali zao walizopata kwa rushwa na uhalifu wa uchaguzi ili iwe fundisho kwa wale viongozi na wajumbe wengine wa Tume wanaoneemeka kwa machozi ya wengine.
 
Pamoja na kuwa umechaguliwa na wananchi lakini chama ndicho kilichokutambulisha kwa wananchi, chama ndicho kilichokuteua chama ndicho kilichokudhamini, na chama ndicho kilicho kupigia kampeni, kwenda kinyume na chama ni kujiondoa mwenyewe kwenye chama.

Cecil Mwambe aliyekuwa mbunge wa Ndanda alitaka kujifanya ni mkubwa kuliko chama lkn akajikuta ameishia kuwa mbunge wa Spika, mifano ni mingi lkn uchaguzi ni wako kusuka au kunyoa. Una safari ndefu kwenye siasa kama umeamua kuwa mbunge wa mahakama endelea na harakati zako, mjumbe huwa hauawi.
 
Pamoja na kuwa umechaguliwa na wananchi lakini chama ndicho kilichokutambulisha kwa wananchi, chama ndicho kilichokuteua chama ndicho kilichokudhamini, na chama ndicho kilicho kupigia kampeni, kwenda kinyume na chama ni kujiondoa mwenyewe kwenye chama.

Cecil Mwambe aliyekuwa mbunge wa Ndanda alitaka kujifanya ni mkubwa kuliko chama lkn akajikuta ameishia kuwa mbunge wa Spika, mifano ni mingi lkn uchaguzi ni wako kusuka au kunyoa. Una safari ndefu kwenye siasa kama umeamua kuwa mbunge wa mahakama endelea na harakati zako, mjumbe huwa hauawi.
Mbowe na Lema wa angekuwa wameshinda angeenda bungeni kama kawa

Wanambania dada wa tu bure.
 
Mama hamia CCM Kama unataka ubunge. CDM hakiitaji mwakilishi. Unga juhudi mkono. Ili mkaendelee na vikao vya CCM dodoma badala ya bunge
Huu ni ukatili mkubwa wao ingetokea wameshinda wasingeenda?

Huyu Dada ni wakupewa moyo sana.

MAENDELEO HAYANA VYAMA ILA MAENDELEO YA KWELI UTAYAPATA CCM
 
Pamoja na kuwa umechaguliwa na wananchi lakini chama ndicho kilichokutambulisha kwa wananchi, chama ndicho kilichokuteua chama ndicho kilichokudhamini, na chama ndicho kilicho kupigia kampeni, kwenda kinyume na chama ni kujiondoa mwenyewe kwenye chama...
Uzuri wenu tanapa huwa mnaongea kwa kufuata mapigo ya makalio yenu na wala si vikao,na hata kama ni maamuzi ya vikao,Mbowe anabadili gia angani na hakuna wa kumpinga.

Hivi mbowe akiteuliwa na Rais kuingia bungeni na akakubali kwenda kuwa KuB mtawaambia nini watu?au mtarejea zile kauli zenu za kwenye siasa hakuna adui wa kudumu,Mbowe ana busara,blah blah.
 
Mbunge si muwakilishi wa wananchi tu.

Ni muwakilishi wa wananchi kwa tiketi ya chama.

Hivyo, leo CHADEMA kama chama wakiamua kususia bunge, na huyu Mbunge akang'ang'ania kwenda bungeni, na CHADEMA wakamvua uanachama, kisheria atakosa uwezo wa kuwakilisha hao wananchi wake.

Not that we follow the law so much in Tanzania.

Hivyo, amalize tofauti zake na wenzake wa CHADEMA ndani ya chama.
Huyu ndiye Kiranga niliyemfahamu wakati najiunga JF. (free thinker)
 
Hizo ndio akili za maCCM.
Ngoja nikupe shule hapa.
Hakuna mgombea aliyegombea ili kushindwa. Hivyo hoja ya kugombea ili ushinde haina mantiki hapa...
Ametoa ushauri mzuri lakini. Hata katika chaguzi zilizopita kulikuwa na dosari nyingi, na kuna majimbo ambayo upinzani ulishinda licha ya dosari hizo.

Hakuna mantiki ya kupoteza muda kulalamikia dosari za uchaguzi mahali ambapo chama kimeshinda licha ya dosari hizo. Nguvu inapaswa kuelekezwa pale ambapo dosari zimeleta madhara kwa maana ya kupoteza.

Sawa, chama kifanye kinavyotaka lakini ushauri wa mbunge ni mzuri.
 
Upande wa Rais mimi naona Hauna shida sana mana Rais ni mtu mmoja tu anayechaguliwa na kwa vypvyote ni lazima mmoja ashinde na kwa sheria na katiba ya Tanzania aliyepo madarakani anagombea akiwa na kamalaka yote. Anaweka nguvu zote za kidola kumrudisha madarakani bila kuulizwa na mtu hivyo hawezi kushindwa kamwe labda kwa uwezo wa Mungu....
Kwenye ubunge wafungue kesi tu. Kwa ujumla mahakama zimekuwa zikitenda haki katika hizi kesi za uchaguzi. Na mahakamani ndipo penye fursa ya kuweka ukweli wote hadharani, for the record. Watumie fursa hii.
 
Huyu nae ni wa kuhurumia tu! Ipo siku atakuja juta maana miaka 5 si mingi. Magu si mtu na hana rafiki bali anakutumia pale tu anapokuhitaji.

Awaulize Mbatia na Lipumba .

Aendelee na ubunge wake na afanye yote lakini kamwe asinyee kambi.
Kweli chadema kumejaa watu wa kushangaza, kwahiyo unataka nawewe huyu dada asiende bungeni?

Kisa Mbowe,Lema,Msigwa,Sugu,heche wamekosa ubunge? You're completely prejudice!!
 
Huyu nae ni wa kuhurumia tu! Ipo siku atakuja juta maana miaka 5 si mingi. Magu si mtu na hana rafiki bali anakutumia pale tu anapokuhitaji.

Awaulize Mbatia na Lipumba .

Aendelee na ubunge wake na afanye yote lakini kamwe asinyee kambi.
Huwezi jua mzee, jamaa wa visasi anaweza akamuona tena, siumechk shonza kwenye viti maalum
 
Hizo ndio akili za maCCM.
Ngoja nikupe shule hapa.
Hakuna mgombea aliyegombea ili kushindwa. Hivyo hoja ya kugombea ili ushinde haina mantiki hapa. Pili kama yeye aligombea na kushinda haina maana kuwa uchaguzi katika jimbo lake ulikuwa huru na haki...
Kama hoja ni kutokuwa na uchaguzi huru na wa haki basi hata 2015 hakukuwa na uchaguzi huru na wa haki,lakini mbona hakukuwa na haya mambo? Miaka yote upinzani umekuwa ukishiriki chaguzi hizihizi zisizo huru na haki,cha tofauti safari hii ni hao akina Mbowe na wenzie kuguswa moja kwa moja na huu uchaguzi usio huru na haki ambao wamekuwa wakiushiriki miaka yote huku wakitambua kuwa sio uchaguzi wa haki,ila labda pengine wakati huo nafasi zao za ubunge zilikuwa hazijaguswa wakawa wanaona kawaida tu hawakuona ulazima wa kugomea matokeo kwa kuziacha nafasi zao za ubunge.
 
Kweli chadema kumejaa watu wa kushangaza, kwahiyo unataka nawewe huyu dada asiende bungeni?

Kisa Mbowe,Lema,Msigwa,Sugu,heche wamekosa ubunge? You're completely prejudice!!
Mimi nashangaa wakati miaka yote wamekuwa wakilalamika kwa kutokuwa na uchaguzi huru na wa haki ila hatukuona hao akina Lema,Mbowe,Lissu n.k wakigoma kwenda bungeni ijapokuwa hizo chaguzi zote hazikuwa huru na haki.

Mimi ndio maana huwa naulizaga kuwa hawa wanaojiita wapinzani ni kwamba wanapinga nini?maana hawana msimamo.
 
Mlimteua wa nini kama hankutaka aingie bungeni?

Kwanza ubunge kapata kwa gharama na juhudi zake binafsi, kumbuka hakuna mgombea ubunge aliyesaidiwa pesa na makao makuu, wote waliambiwa wajitegemee katika kampeni.

Bunge limlinde dhidi ya udikteta na ubinafsi wa viongozi wa CHADEMA.

Kuna mahali CHADEMA waliweka hoja mufilisi kuwa ni mpenzi wa mbunge mmoja wa CCM, sasa kwani hilo ni kosa? Watu wa vyama tofauti hawaruhusiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi? Mbona Jesca Kishoa na Kafulila wana mahusiano au Zitto na yule mtoto wa kiongozi wa CCM ( Amina) ni wapenzi hadi kuzaa mtoto? Kwa nini iwe nongwa kwa mbunge huyo wa CHADEMA?

Kama tume imeweza kumlinda na kumpa ubunge
Bunge ltawezaje kushindwa kumlinda ashukuru jimbo lake walikuwa wawili tu
 
Back
Top Bottom