mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,075
- 4,111
Mimi sijahama CHADEMA na wala sitegemei kuhama, mimi ni Mbunge mteule kwa hiyo nitawatumikia Wananchi kwa imani ambayo waliniamini, labda chama changu kitakavyoamua kama itakuwa vinginevyo basi itafahamika.
"Niliahidi kutokusaliti chama changu na kwa maana hiyo siwezi kuwasaliti wananchi walionipa heshima, utaratibu unaoendelea kwa chama changu cha CHADEMA wanaweza kuendelea nao kwa sababu sheria inawaruhusu.
Lakini kwenye jimbo langu pamoja na wananchi wangu na viongozi, tumeona hakuna sababu ya mimi kugomea kuapishwa kwa sababu chama kiliniamini nigombee na naamini kiliniteua nikashinde na siyo kushiriki uchaguzi.
Ni vigumu sana kurudi kwa wananchi kuwaambia nasusia matokeo, kama sikususia uchaguzi siwezi kususia matokeo, lakini maeneo ambayo wanafikiri kuna dosari waendelee kufuata utaratibu wa kisheria na haki itatendeka.