Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,441
- 7,780
Leo mbunge pekee wa kuchaguliwa kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia jimbo la Nkasi Kaskazini amefanya mahojiano na mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya DW, Deo Makomba na mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo.
MWANDISHI: Unajisikia vipi hasa kuwa mmoja wa wabunge walioweza kushinda katika moja ya chama cha upinzani?
AIDA KHENAN: Moja, ninajisikia furaha kuwa mbunge wa kuchaguliwa kwenye jimbo langu ambalo ni kwa mara ya kwanza kupata mbunge mwanamke lakini mbunge wa kwanza wa upinzani kwenye mkoa wetu wa Rukwa. Lakini ninajisikia vibaya pia kuwepo peke yangu ndani ya Bunge kwa sababu nilikuwa mbunge wa viti maalum, nilikuwa na wabunge waliokuwa wamenitangulia na wabunge wengine ambao niliendelea kujifunza kutoka kwao na nilitamani niendelee kujifunza kutoka kwao.
MWANDISHI (DW): Uchaguzi haukuwa huru na haki, upande wako umeuonaje?
AIDA KHENAN: Upande wa jimbo langu nimetangazwa, kwenye maeneo mengine imekuwa tofauti, kwa kuwa chama kimeamua kwenda mahakama, kiendelee na huo mchakato. Haki ilitendeka au kutotendeka hiyo tafsiri itaenda kutolewa na mahakama.