Aichoma Moto Nyumba Yake Baada ya Mkewe Kukataa Kumpikia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aichoma Moto Nyumba Yake Baada ya Mkewe Kukataa Kumpikia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jul 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Monday, July 27, 2009 5:46 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Australia amehukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kuichoma moto nyumba yake huku mkewe na watoto wake wakiwa ndani baada ya mkewe kukataa kumpikia lanchi. Akiwa na hasira kwanini mkewe hataki kumpikia chakula cha mchana Rajah Theiveneraeas, 54, mkazi wa Melbourne nchini Australia alimwaga petrol kwenye ngazi za nyumba yake na kuiwasha moto nyumba yake huku mkewe na watoto wake wakiwa ndani.

  Mkewe Vasangha na binti zake Amviga, 21, na Anoja, 16, iliwabidi wapitie madirishani kusalimisha maisha yao.

  Mkewe na watoto wake waliunguzwa vibaya na moto huo katika harakati za kuokoa maisha yao.

  Mahakama iliambiwa kuwa Rajah alikuwa amelewa sana siku ya tukio hilo na alikuwa kwenye mzozo na binti yake mkubwa akimtaka binti yake huyo ampe heshima zake.

  Akisomewa hukumu yake Jaji wa mahakama hiyo alisema kuwa kitendo cha Rajah kilikuwa ni cha hatari, kisichojali utu na chenye nia ya kufanya uharibifu.

  Rajah alihukumiwa kwenda jela miaka minne na atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu kabla ya kuingizwa kwenye kundi la watu ambao wanaweza kusamehewa vifungo vyao.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2636542&&Cat=2
   
Loading...