Aibu yetu: Karne ya 21 bado unaamini maendeleo ni imani pasipo kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa na nidhamu ya pesa na muda

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
484
541
Karne ya 21 bado unaamini maendeleo ni imani pasipo kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa na nidhamu ya pesa na muda.

Aibu yako! Matokeo ya kutafasiri maendeleo kama imani utaishia kuchinja albino, kuchanjwa chale makalioni, kulala makaburini, kuvaa hirizi kiunoni, kujisaidia haja kubwa kwenye sufuria la kupikia wageni, kuzini na vikongwe, kulala chini ya kitanda na wakati una kitanda kizuri, kunywa mkojo wa mbwa kila unapopata kiu na wakati Mungu kakupa maji safi bure, kuwafanya watoto wako mazezeta na wakati wewe wazazi wako walikulea vizuri, kuzaa na vichaa na wakati una mke mzuri na kila aina ya uchafu kisa, eti upate utajiri.

Aibu yako! Acha kuchekesha wagonjwa, maendeleo hayaji kwa bahati nasibu, ingekuwa ni hivyo basi kila mtu angekuwa tajiri Tanzania.

Karne ya 21 bado watawala wetu mnaamini umaskini utaondoka kwa semina elekezi. Unajua haya nayo ni maajabu! Afisa wa serikali na usomi wako wote unasafiri kwa gari na dereva wa serikali kuwahi semina elekezi pale Dar katika hoteli ya kifahari kumsikiliza mtaalamu kutoka Marekali na Ulaya Magharibi akupe mbinu za kupambana na umaskini. Mtaalamu mwenyewe kaufahamu umaskini wetu kupitia vitabu.

Ajabu sana! Aliyesema ignorance doesn’t kill but it makes you sweat a lot hajakosea. Njia sahihi ya kupambana na umaskini ni kwa kumtumia expert wa umaskni mwenyewe ambaye ni maskini alisema Hernando de Soto mwandishi wa, “The Mistery of Capital.”
 
Karne ya 21 tunachukua hatua baada ya maafa kutokea! Aibu yetu. Mwaka 2015 ajali iliyotokea Mafinga kutokana na barabara mbovu ilinihuzunisha sana. Kontena kutoka kwenye lori lilidondokea basi na kuua karibu abiria wote. Mashuhuda wanasema walisikia vilio vya watu chini ya kontena lakini hakuwa na uwezo wa kuwasaidia. Abiria hao walilia sana lakini hakuna aliyeweza kunyanyua kontena la futi arobaini lililowafunika. Karne ya 21 hatuna teknolojia ya kuweza kuokoa majeruhi kwa haraka, mpaka wanakufa tunawaona. Inahuzunisha. Vilio vyao vilizimika kwa mauti. Baadaye serikali yote ikahamia Mafinga na rambirambi kibao zilizosindikizwa na maneno ya,

“Walale mahali pema peponi.” Ni aibu kuelekeza nguvu kubwa kwenye maafa badala ya kutibu vyanzo vya maafa. Ni aibu kuonyesha utu baada ya maafa kutokea. Aliwahi kuimba Charles Jangalason, “Mgonjwa anaugua, anapelekwa Muhimbili kwa kibaiskeli, ndugu hawana habari. Lakini anapokufa, ndugu wanajitokeza kwa mbwembwe kibao na kujisemea, ‘Huyu ni mtu wetu, mwili wake lazima usafirishwe kwa ndege.” Eti ni mtu wao. Walikuwa wapi kipindi anaumwa? Serikali ulikuwa wapi wakati watu wa Mafinga wakikupigia kelele kuhusu ubovu wa barabara yao? Leo sasa tumepoteza ndugu zetu. Damu ya marehemu na machozi ya ndugu wa marehemu na viwe juu yenu enyi watawala dhalimu mnaotanguliza matumbo yenu mbele badala ya nchi. Aibu yenu.
 
Karne ya 21 bado unaamini maendeleo ni imani pasipo kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuwa na nidhamu ya pesa na muda.

Aibu yako! Matokeo ya kutafasiri maendeleo kama imani utaishia kuchinja albino, kuchanjwa chale makalioni, kulala makaburini, kuvaa hirizi kiunoni, kujisaidia haja kubwa kwenye sufuria la kupikia wageni, kuzini na vikongwe, kulala chini ya kitanda na wakati una kitanda kizuri, kunywa mkojo wa mbwa kila unapopata kiu na wakati Mungu kakupa maji safi bure, kuwafanya watoto wako mazezeta na wakati wewe wazazi wako walikulea vizuri, kuzaa na vichaa na wakati una mke mzuri na kila aina ya uchafu kisa, eti upate utajiri. Aibu yako! Acha kuchekesha wagonjwa, maendeleo hayaji kwa bahati nasibu, ingekuwa ni hivyo basi kila mtu angekuwa tajiri Tanzania.

Karne ya 21 bado watawala wetu mnaamini umaskini utaondoka kwa semina elekezi. Unajua haya nayo ni maajabu! Afisa wa serikali na usomi wako wote unasafiri kwa gari na dereva wa serikali kuwahi semina elekezi pale Dar katika hoteli ya kifahari kumsikiliza mtaalamu kutoka Marekali na Ulaya Magharibi akupe mbinu za kupambana na umaskini. Mtaalamu mwenyewe kaufahamu umaskini wetu kupitia vitabu.

Ajabu sana! Aliyesema ignorance doesn’t kill but it makes you sweat a lot hajakosea. Njia sahihi ya kupambana na umaskini ni kwa kumtumia expert wa umaskni mwenyewe ambaye ni maskini alisema Hernando de Soto mwandishi wa, “The Mistery of Capital.”
Ahsante sana kaka watanzania wanafikiri et maendeleo ni miujiza wanafikiri wakikaa tu ndege zitakuja zenyewe wanaamin zikinunuliwa kwa pesa zetu hazitaleta faida wanaamini ukibana matumizi kujenga nchi kwa uzalendo ni unyanyasaji na uwizi wanaamin zaidi kuongoza kwa kuelekezana tu kwa upole wanaamin ukiwa mkali basi sio jadi yao hawajazoea mwizi anaambiwa tu kwa upole kaka au dada usiiibe nakuomba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom