Aibu yetu ama aibu yao? Kwanini watanzania wanadanganyika kirahisi hivi?

Mheikungu

JF-Expert Member
Oct 15, 2018
214
448
HILI HAPANA.

Kilichotokea leo uwanja wa Taifa sio haki, sio heshima kwa wajasiriamali. Yapaswa Serikali kutoa kauli kuhusu hili lililotokea.

Wajasiriamali wameujaza uwanja wa Taifa leo baada ya kutangaziwa kuwa kutakuwa na mikopo kuanzia 500,000/-

Watu wamedamka asubuhi, wamepigilia suti za maana. Kufika kule hakuna cha mkopo wala nini badala yake ni tamasha la dini. Sio haki kabisa hii.

Waliowaongopea wadanganyika wawajibishwe haraka
 
siyo wale wanajiita wakorea kweli maana huku kwetu kinyerezi kila siku wanadanganya watu eti wanakuja kugawa hela na watu wanaenda kweli
 
Ambatanisha kapicha kidogo mkuu.
 
siyo wale wanajiita wakorea kweli maana huku kwetu kinyerezi kila siku wanadanganya watu eti wanakuja kugawa hela na watu wanaenda kweli
Wanaweza kuwa hao. Kuna jamaa yangu ameenda,amenipigia simu analaani hataaare
 
Kuna mambo yanasikitisha sana...

Hawa viongozi wanaoratibu haya mambo ipo siku yatawafika mabaya sana...

Cc: mahondaw
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom