Aibu ya watangazaji na wazungumzaji katika Media

jellyFish

JF-Expert Member
Mar 6, 2013
316
127
Nashangazwa na watangazaji wa radio na televisheni na wazungumzaji wanao hojiwa au kuwa katika mazungumzo mubashara katika vyombo vya habari kwa kuboronga katika kutumia lugha ya Kiswahili.

Neno linalokosewa sana na wengi wa wazungumzaji na watangazaji ni neno NYIMBO na WIMBO. Mtu haoni ukakasi kusema ile "nyimbo" yangu badala ya ule "wimbo" wangu. Yaani mtu anashindwa kujua wingi wa wimbo na umoja wa nyimbo. Ingekuwa mtu anakosea hivi katika lugha ya kiingereza mfano mtu angetamka ===introducing a "songs" --- Ndindindi of lady JD===. angeshambuliwa kwa kuitwa kilaza na kejeli nyingi.

Chakushangaza, watangazaji wa TV na redio ndio wanaongoza kukosea matumizi ya neno "wimbo" na "nyimbo" mbaya zaidi hata watangazaji na wazungumzaji mbalimbali wa media ambao asili yao ni mwambao wa pwani na wengine wanatoka Zanzibar nao pia wanashindwa kulitumia neno hili kifasaha.

BADILIKENI HAMWONI AIBU KUKOSEA LUGHA YA ASILI YENU? WATANGAZAJI WA NJE WA KISWAHILI WATAJIFUNZA WAPI KUONGEA KISWAHILI MWANANA.
 
Nashangazwa na watangazaji wa radio na televisheni na wazungumzaji wanao hojiwa au kuwa katika mazungumzo mubashara katika vyombo vya habari kwa kuboronga katika kutumia lugha ya Kiswahili. Neno linalokosewa sana na wengi wa wazungumzaji na watangazaji ni neno NYIMBO na WIMBO. Mtu haoni ukakasi kusema ile "nyimbo" yangu badala ya ule "wimbo" wangu. Yaani mtu anashindwa kujua wingi wa wimbo na umoja wa nyimbo.
Ingekuwa mtu anakosea hivi ktk lugha ya kiingereza mfano mtu angetamka ===introducing a "songs" --- Ndindindi of lady JD===. angeshambuliwa kwa kuitwa ****** na kejeli nyingi.
Chakushangaza, watangazaji wa TV na redio ndio wanaongoza kukosea matumizi ya neno "wimbo" na "nyimbo" mbaya zaidi hata watangazaji na wazungumzaji mbalimbali wa media ambao asili yao ni mwambao wa pwani na wengine wanatoka Zanzibar nao pia wanashindwa kulitumia neno hili kifasaha.

BADILIKENI HAMWONI AIBU KUKOSEA LUGHA YA ASILI YENU? WATANGAZAJI WA NJE WA KISWAHILI WATAJIFUNZA WAPI KUONGEA KISWAHILI MWANANA.
Hawa watangazaji zero kabisa
 
Back
Top Bottom