Aibu ya Udom hii hapa!!!

Konzogwe

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
435
225
Sikutegemea chuo kipya na kinachojijengea umaarufu kama hiki kikose maji. Hebu tazama, mtu unaenda ****** unakutana na kinyesi cha jana! Mtu kaenda na kikopo cha maji lita moja na baada ya kujisafisha yeye anaondoka.Ndiyo, atawezaje ku-flash uchafu kwa maji mengi wakati hata hayo kidogo kayahangaikia kuyapata? Hata kampuni inayohusika na usafi itapata wapi maji? Asubuhi utashangaa msomi wa masters akirandaranda bila kujua atapata wapi nusu ndoo akaoge.

Inauma sana! Leo nimezunguka nusu saa bila kupata walau tone la maji, nikaamua kwenda cafeteria kwa wapishi maana wanayo matanki, nao wakanifukuza lakini mkuu wao akanionea huruma akaniita kanipa robo ndoo (lt 5) na akasisitiza nisipite njia nilokuja nayo ili wahusika wasinione.

Inauma sana! Mliopita Universities hebu pigeni picha muone maisha haya.Kama nikawaida au la! Sijui aliye responsible ni nani abebe hii kashfa!
Inauma sana. Naomba aliye karibu na mhusika amwambie kabla hatujaanza kuvunjiana heshima.
 
Johnsecond

JF-Expert Member
May 4, 2010
1,076
0
Achana nao hao vijana wooote ni CCM, hawajui kugoma wala kuomba haki zao. Hata ikichukua week mbili huwezi waona wakipiga kelele maana wamechoka walikuwa kwenye kampeni. Hivyo achana nao hao hata wakikosa mwezi mzima
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Achana nao hao vijana wooote ni CCM, hawajui kugoma wala kuomba haki zao. Hata ikichukua week mbili huwezi waona wakipiga kelele maana wamechoka walikuwa kwenye kampeni. Hivyo achana nao hao hata wakikosa mwezi mzima
Poleni sana vijana, bahati mbaya kampeni zimeishapita sijui nani atawasikiliza.... Kale kaBoss kafupi kanaitwa Mlacha kana nyonya mavi lake huwa kanalikodisha kwa chuo, labda mkaambie kaje kuwaletea maji kupitia hilo nyonya mavi. Jifunzieni kugoma ktk hii issue msiogope kukiangusha chama chenu cha mapinduzi, jifunzeni ushupavu wa vijana wa vyuo vingine ambao wakiletewa za kuleta wanagoma. Hivi ile milioni moja mliyomchangia JK kuchukua fomu si ingewasaidia kununua maji????
 
Lenana

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
421
225
watoto wamebanwa na makada wa ccm si unajua tena vyuo vyetu vikuu na baadhi ya taasisi muhimu zinaongozwa na makada na isitoshe serikali za wanafunzi zilishatiwa mfukoni na hao makada husika vijana jitambueni sio lazima muwategemee hawa mafisadi haki inadaiwa haiombwi chonde chonde au wengi wenu hamna qualificatins stahili so mnawazo mkifukuzwa hamtapata chuo tena amkeeni wajameni acheni ufala etii!
 
Konzogwe

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
435
225
Haaa! Lenana! Ufala tena! Infact I escaped a Lion and I meet the Bear! Kwa heli.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,147
2,000
Wewe mwenzetu wa wapi? Haya mambo hata UDSM huwa yapo hivyo hivyo. Watu tulikuwa tunanunua uhai ya lita kumi siku hizo kwa ajili ya kuoga. Suala la cho.o.ni hilo ilikuwa ni kesi nyingine. Ukiingia mabwenini, unapoanza kupanda ngazi tu, unakutana na harufu ya ch.o.oni imetapakaa kila mahali.

Hiyo ilikuwa ni hali ya kawaida na tulikuwa tunaweza kukaa hivyo kwa wiki nzima, ndipo waanze kutuletea maji kwenye magari (tankers). Na hayo ukiyachelewa imekula kwako. Kwa hiyo sikutarajia kwamba UDOM iwe unique sana wakati ipo ndani ya system ileile ambayo ni ya kifisadi. Gangamala, hiyo ndo shule ya bongo. Unashangaa nini?

Halafu ukimaliza hapo ukapewa ukatibu mkuu wa wizara ya elimu unaanza kuwafanyia hayohayo watakaokuwa wanasoma hapo wakati huo. Hiyo ndiyo tabia halisi ya mtz. Akiwa kwenye shida kelele kweli, akipewa nafasi ya utendaji, anafanya yaleyale aliyokuwa anawapigia kielel wenzie.
 
Ally Msangi

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
608
250
maji hilo ni tatizo la vyuo vikuu vya serikali, na hivi UDOM mpo porini hata maji ya kununua yanakuwa tabu tupu aisee poleni sana bt ndio siasa hizo, na mpo karibu na mahali ambapo hao wanao tetea haki zenu wapo sasa inakuwaje msi toe malalamiko yenu kwa uongozi husika
 
AcinonyxJubatus

Senior Member
Nov 3, 2010
125
170
Mimi pia nimepitia adha hiyo nikiwa kama mwanafunzi wa masters hapo UDOM. kwa kweli ukiwa ndani ya hicho chuo utasikitika hata kwa nini wanasiasa wanajisumbua kukisifia kwamba wana bonge la chuo. upuuzi mtupu. viry poor plan iliyokua implemented na mchina. Campus ya social ndio usiseme. mifumo ya maji taka imeharibika. population ikiwa high campus yote inanuka kwa sababu maji taka yamefurika kila mahali. huyo jamaa aliyetambulishwa hapo juu kama kaboss kafupi, ni mfupi kweli mpaka akili. ana nyodo utathani yeye tuu ndio msomi nchi hee, ni mwehu fulani hivi anayejigamba kuletwa UDOM na mhishimiwa Dacta mkuu wa nji. UDOM isikieni tuu huko nje, sisi tulioko humu ndani ndio tunajua ubovu wa kuanzia watendaji, majengo ya kichina, huduma mbaya za chakula, aaghhhh:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry: let me stop there before I abuse someone some more.
 
LoyalTzCitizen

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,178
2,000
Inanikumbusha nilipokuwa high school pale Mazengo Boys High School Dodoma! maji yalikuwa ni ishue! huuuuh! nilikuwa nateseka sana na typhoid, halafu kule beech(toilets) ndio hakufai kabisa! tuliishi kama wanyama pori! anyway, what an adventure that was! Bigggg up Mazengo Boys n Msalato gyals everywhere!!:smile-big:
 
Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
1,500
Jamani si ndio nyie UDOM mliomsifia JK sasa nini tena. Hebu nyamazeni bana mnanikera alaaaaa
 
Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
3,441
2,000
Sikutegemea chuo kipya na kinachojijengea umaarufu kama hiki kikose maji. Hebu tazama, mtu unaenda ****** unakutana na kinyesi cha jana! Mtu kaenda na kikopo cha maji lita moja na baada ya kujisafisha yeye anaondoka.Ndiyo, atawezaje ku-flash uchafu kwa maji mengi wakati hata hayo kidogo kayahangaikia kuyapata? Hata kampuni inayohusika na usafi itapata wapi maji? Asubuhi utashangaa msomi wa masters akirandaranda bila kujua atapata wapi nusu ndoo akaoge.

Inauma sana! Leo nimezunguka nusu saa bila kupata walau tone la maji, nikaamua kwenda cafeteria kwa wapishi maana wanayo matanki, nao wakanifukuza lakini mkuu wao akanionea huruma akaniita kanipa robo ndoo (lt 5) na akasisitiza nisipite njia nilokuja nayo ili wahusika wasinione.

Inauma sana! Mliopita Universities hebu pigeni picha muone maisha haya.Kama nikawaida au la! Sijui aliye responsible ni nani abebe hii kashfa!
Inauma sana. Naomba aliye karibu na mhusika amwambie kabla hatujaanza kuvunjiana heshima.

Yaani hata maji ya kutawaza, Soma Signature below!!
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,707
2,000
Hiyo ndio hasara ya kufanya mipango kwa haraka haraka bila kuifikira kwa kina ilimradi inakidhi matakwa ya kisiasa!! Hivyo hivyo international Airport itajengwa Bagamoyo kwa kutumia mabilioni ya shilingi halafu hakutakuwa na ndege hata moja ya kutua hapo!! It will be another white elephant!!Lakini kwa vile Rais kaahidi basi lazima kiwanja kijengwe hata kama watu watakosa dawa hospitalini.
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,523
2,000
Hii ndo shida kubwa katika public utilities na necha ya dom si mwaijua, nadhani watapaswa kufanya kazi ya ziada vinginevyo magonjwa njenje. Lakini wasijali najua wengi ni wanachama wa ccm so let them wait forever in vain kupata maji ya ziwa Victoria!
 
mtuwawatu

Senior Member
Oct 30, 2007
105
195
Kumbe hizi sifa tunazisikia ni fiksi tupu, uchakachaji mpaka plans, kweli tz imeisha
 
Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,146
2,000
:nono: Wacha muipate. si nyinyi ndiyo mlizunguka nchi nzima kusainisha fomu?
 
gaby

Member
Nov 14, 2010
17
0
Sikutegemea chuo kipya na kinachojijengea umaarufu kama hiki kikose maji. Hebu tazama, mtu unaenda ****** unakutana na kinyesi cha jana! Mtu kaenda na kikopo cha maji lita moja na baada ya kujisafisha yeye anaondoka.Ndiyo, atawezaje ku-flash uchafu kwa maji mengi wakati hata hayo kidogo kayahangaikia kuyapata? Hata kampuni inayohusika na usafi itapata wapi maji? Asubuhi utashangaa msomi wa masters akirandaranda bila kujua atapata wapi nusu ndoo akaoge.

Inauma sana! Leo nimezunguka nusu saa bila kupata walau tone la maji, nikaamua kwenda cafeteria kwa wapishi maana wanayo matanki, nao wakanifukuza lakini mkuu wao akanionea huruma akaniita kanipa robo ndoo (lt 5) na akasisitiza nisipite njia nilokuja nayo ili wahusika wasinione.

Inauma sana! Mliopita Universities hebu pigeni picha muone maisha haya.Kama nikawaida au la! Sijui aliye responsible ni nani abebe hii kashfa!
Inauma sana. Naomba aliye karibu na mhusika amwambie kabla hatujaanza kuvunjiana heshima.

Hicho chuo hakina tofauti na hizi sek za kata
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
53,857
2,000
nyie si ndio naskia mlichanga hela ya JK kuchukua fomu za kugombea? Mlidhani wote ni ma-riziwani nini,, na bado mafisadi wako bussy sa ivi wanarudisha hela yao ya kampeni. Vaeni makofia yenu na tshirt zenu mlizopewa na ccmafisaid kaeni chini na kujiliwaza.
 
suamakona

Member
Oct 31, 2010
13
0
Ni kweli kila mtu ana yake ya kusema lakini ifahamike kuwa no body is perfect lazima kutakuwa na mapungufu tu. Hayo ya UDOM yanayoonekana kuwa ni kero ni kasoro ambazo hatuwezi kuzikataa halafu si UDOM pekee. Mwanzo mgumu hasa unapokamia game jamani.
Na nyie wana-UDOM mnaokidis chuo mmeniangusha kuona mnajifanya mnajua kukosoa hayo mapungufu ambayo mnaona wazi kuwa hayavumiliki. SWALI NI KUWA MMEFANYA NINI JUU YA HILO? Acheni unafki ficheni ujinga msifiche busara.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom