Mkulima wa Kuku
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,270
- 532
Leo asubuhi jamaa yangu alikuwa amekuja kuchukua gari yake akielekea Zimbabwe. Alipofika kwenye kituo kimoja km 20-30 hivi kabla hajafika Tunduma mpakani askari wa Tanzania wakamsimamisha na kumtuhumu kuwa yeye ni polisi amekuja kufanya upelelezi kwa nchi na kuwa hawatamuachia mpaka awape pesa. Akawa hakubaliani na jambo hilo akaonyesha vitambulisho vyake na pasport yake inayosema yeye ni Mchungaji lakini wakamng'ang'ania kwa saa moja mpaka akawapa 10,000/= ndipo walipomuachia.
Nimewasiliana naye akasema akifika Zimbabwe atafungua jalada ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya jambo hilo.
Hii ni aibu kwa Mwema, Rais na nchi kwa ujumla kudai fedha ndogondogo za aibu.
Naomba kuwasilisha.