Aibu: Watuhumiwa watatu kesi ya Mbowe wadai kuteswa na Polisi ili wakubali kuandika maelezo ya uongo

Kwa hi
Usijifanye mjuaji kwenye mambo ambayo una ujinga wote. Wawe na majeraha wasiwe nayo, wanaruhusiwa kuyakataa maelezo waliyoyatoa Polisi alimradi kama huko Polisi kulikuwa na mazingira ya kuwalazimisha kama vile mateso, vitisho, au masumbufu kama yale ya kuwaweka kwenye sero za Polisi kwa muda usiojulikana.
Kwa ujinga wako unadhani kukataa maelezo uliyoandika police kunaweza kukunasua kwenye kukutwa na makosa?
Hiyo huwa ni namna ya kurukaruka tu kama maharage kwenye sufulia lakini lazima yaive.
 
Kwa hi

Kwa ujinga wako unadhani kukataa maelezo uliyoandika police kunaweza kukunasua kwenye kukutwa na makosa?
Hiyo huwa ni namna ya kurukaruka tu kama maharage kwenye sufulia lakini lazima yaive.
Toa mifano kama mtu mwerevu. Hili siyo jukwaa la vioja. Inaonekana mawazo yako mwisho wake ni kwenye chakula tu.

Always think and argue intelligently.

Hoja ya msingi hapo ni kuwa maelezo yaliyotolewa kwenye mazingira ya kulazimishwa, hayana uzito wowote katika ushahidi.

Polisi wangekuwa na akili japo kidogo, walistahili kuhakikisha maelezo ya hao mashahidi yanatolewa mbele ya mlinzi wa amani na wakili wao.
 
Polisi wengi wajingawajinga......wanauwezo mkubwa wa nguvu, huku wakiwa na uwezo mdogo wa akili (reasoning)!!!
Uko sahihi KABISA.
Tangu nji hii ipate Uhuru nijuavo mimi Kazi ya UPOLISI ILIKUWA NI CHAHUO LA MWISHO kabisa kwa watu ambao walikuwa hawana uwezo darasani!!!
Hivo polisi wengi ni aidha Form 4 failures au Division "0"......!!
Ndiyo maana hata wakti wa uhakiki wa vyeti fake Mwenda zake hakugusa majeshi yote...!!!
Hivo mie sishangia Mzee Zero na Maafande wake kwa MADUDU wanayewafanyia CHADEMA na mwenyekiti wake lakini pia hata Watz wengi wasio na hatia.....!!!!
 
ukizingatia hawa walinzi walikuwa x- military, watakuwa wameteswa sana.. nakumbuka story ya Mdude kuteswa hadi kukojoa damu aisee !! ni dhambi kubwa mno - no wonder familia nyingi za mapolice huwa hazina amani na mafanikio maishani sababu ya kujitafutia laana kama hizi kwa koo zao.
 
Kwa hi

Kwa ujinga wako unadhani kukataa maelezo uliyoandika police kunaweza kukunasua kwenye kukutwa na makosa?
Hiyo huwa ni namna ya kurukaruka tu kama maharage kwenye sufulia lakini lazima yaive.
Acha ujinga wewe!
Maelezo uliyoandika Polisi haiwezi kuwa ndiyo ushahidi pekee wa mtu kutiwa hatiani. Mtuhumiwa anaweza kulazimishwa kuandika kuwa ameaua@ gun point lakini USHAHIDI CONCRETE ukathibitisha kinyume chake.
Kwa hiyo ushahidi wa IGP Zero na Ole Subayi(Sabaya) au Ole na ngai hautakuwa ushahidi wa mwisho. There's a lot to be revealed in this case about Tanzania Police Force pre-planned and cooked evidences! Time gonna tell.
 
Watuhumiwa hao watatu walioshitakiwa pamoja na Mbowe Wameiomba Mahakama kutoyatambua maelezo waliyoyaandika Polisi kwa vile waliyaandika kwa shinikizo la vipigo na mateso, hayakuwa maelezo ya kweli , bali waliyaandika ili wasiuawe kwa mateso .

Ombi hilo limetolewa Mahakamani na washitakiwa hao watatu , waliodai kwamba walilazimishwa kuandika maelezo ya uongo kibabe na kwa mateso makubwa mno , Polisi walitesa watuhumiwa hao kinyama ili kulazimisha kwamba walitumwa na Mbowe kufanya ugaidi kwa lengo la kuhalalisha Tuhuma dhidi ya Freeman Mbowe zilizopangwa kishamba ili kuwafurahisha watawala

Washitakiwa hao wamedai kwamba ili kujinusuru na mateso makubwa ya kinyama na ya kudhalilisha walipokuwa mikononi mwa Polisi , walilazimika kuandika MAELEZO YA UONGO WALIYOYATAKA POLISI ili kuokoa uhai wao
Mahakama ina uwezo wa kuyaondoka maelezo ya awali ya washtakiwa kama watajirishidha kwamba walitenswa mno ili wakubali kuandika na kurekodiwa na hao mapolice. Hili halitakuwa jambo jipya.
 
Tutajuaje kama wao hao hao ndiyo wanaocheza mchezo wa kujikosha?

Swali la kujiuliza ni je wakiwa mikoni mwa Polisi waliteswa au hawakuteswa?? Hii kesi itafungua mengi sana tusiyoyajua, mfano jana nilikuwa nafuatilia 'Space' ya Maria Wakili Fatma Karume akasema nchi yetu mpaka leo imekataa kusaini mikataba ya kimataifa inalinda haki za mahabusu ili wasiteswe wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola kama polisi Magereza. Sasa jambo hili kama ni kweli maana mimi siyo mwanasheria, limenishangaza sana sanaa, kwa nini sisi nchi tunayosifika kwa amani na utulivu (uvumilifu???) tukatae kusaini mikataba ya kimataifa ya kuwalinda watu wetu wasiteswa na mapolisi wapenda rushwa au wasiojua wajibu wao?? why??? Sote tunakumbuka alichosema Mdude nyagali mateso aliyoyapata akiwa mikononi mwa vyombo vyetu, sasa je wanakataa makusudi ili waendeleze utesaji??
 
Lakini mahakama hizi hizi ndio tulizisifia pale zilipoondoa kesi za mbowe, mdude n.k, na zilipomshughulikia Sabaya pia

Kama wakati huo tuliziita huru, iweje sasa tusiziite hivyo?
Haimaanishi zikikosea zisisemwe eti kwasababu zimewahi kuamua sawasawa kesi moja katika 100000
 
This is low!! Hizi legal arguments hapa siyo mahali pake. Yaache hukohuko mahakamani. Ndiyo utawala wa kusheria unavyotaka. Chadema mnakwama wapi? Sasa unataka tufanye nini sisi hapa JF. Una uhakika walilazimishwa au la? Kesi hii itapangiwa jaji ambaye atajua uongo na ukweli ni upi. Kwa kuleta humu tujadili details za masuala yaliyo mahakamani ni kuonesha how fatuous you are . Please give us a break

Kwanza hii ni public forum na pili kila mtu anaingia humu kwa bundle lake na kwa wakati wake na kusoma au ku share anachoona ili kujieleimisha, kupashana habari, na ku share experinces mbalimbali. Wewe hakuna aliyekulazimisha kuufungua huu uzi na kuusoma, sasa kwa nini unapangia watu humu as if umewanunulia bando ??? Who do you think you are?? acheni hizi mentaliti za kipuuzi puuzi....Mbona kesi ya Sabaya inaripotiwa daily tena mpaka details zote zilizojiri mahakamani?? So ni uppuzi kusema eti hizi legal arguments hapa si mahala pake!!! mahala pake ni wapi chooni kwako au??? Unataka kusema watanzania wenye interest na wanachama na mashabiki wa Mbowe/CHADEMA wote nchi nzima waende mahakamani?? Mwisho nikukumbshe tuu kwamba Mahakama ni public ofisi na kiuhalisia kesi huwa zinatakiwa kuendeshwa wazi kabisa ili wananchi wafuatilie na wajifunze. Ndiyo Maana wenzetu wenye mifumo mizuri kama Kenye, Afrika Kusini etc kesi zenye interest kubwa kwa umma inakuwa live kwenye TV na vyombo mbalimbali vya habari, nyie kwa vile mmezoea kuminywa hata pale unapotaka kupiga chafya au kujikuna ndiyo mnakuja hapa na hizi porojo zenu za Karume kenge.
 
ukizingatia hawa walinzi walikuwa x- military, watakuwa wameteswa sana.. nakumbuka story ya Mdude kuteswa hadi kukojoa damu aisee !! ni dhambi kubwa mno - no wonder familia nyingi za mapolice huwa hazina amani na mafanikio maishani sababu ya kujitafutia laana kama hizi kwa koo zao.
Kila ubaya utalipwa
 
Tutajuaje kama wao hao hao ndiyo wanaocheza mchezo wa kujikosha?
Kama hawakuwa na wanasheria kusimamia haki zao nyakati za kuandika maelezo husika, basi madai yao yana uzito; ni sahihi.
 
Acha ujinga wewe!
Maelezo uliyoandika Polisi haiwezi kuwa ndiyo ushahidi pekee wa mtu kutiwa hatiani. Mtuhumiwa anaweza kulazimishwa kuandika kuwa ameaua@ gun point lakini USHAHIDI CONCRETE ukathibitisha kinyume chake.
Kwa hiyo ushahidi wa IGP Zero na Ole Subayi(Sabaya) au Ole na ngai hautakuwa ushahidi wa mwisho. There's a lot to be revealed in this case about Tanzania Police Force pre-planned and cooked evidences! Time gonna tell.
Kwa hiyo unachofurahia hapa ni nini kwamba wamekataa ushahidi walioandika police au ?
Subili kesi iishe ndo mtajua kama walilazimishwa police au wanarukaruka tu kam maharage.
Ni sawa na mwanasheria wenu kusema atawaita sabaya na siro kama mashahidi kisha nyie mnatembea mnanengua viuno wakati hizo ni mbwemnwe tu ili ale peaa yenu.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom