AIBU: Wachungaji KKKT wampinga Dk Shoo

Kitendo cha KKKT kufanya uchaguz kama zile za SSM ..kumtafuta mbu.nge wa kuwakilisha jimbo ni chanzo kizuri mno cha migogoro katika kanisa hili watu hutoa hadi rushwa ili achaguliwe ...
 
KKKT mnakopi na kupesti migogoro kutoka Anglikana. Anglikana ndio baba wa migogoro kwa makanisa yote duniani.

Wametulia kwa muda subiri waliamshe dude.
umesahau moravian kwa kina anayejiita askofu wa chadema mwamakula (asiye hata na kanisa wala waumini wa maana), kuna kikanisa pale kimara kila wakati polisi huwa wanaenda kuamulia ugomvi waumini na wachungaji wameshikana mashati wanapigana ngumi. kila mtu mbabe kuanzia waumini, wazee wa kanisa hadi wachungaji.
 
Kitendo cha KKKT kufanya uchaguz kama zile za SSM ..kumtafuta mbu.nge wa kuwakilisha jimbo ni chanzo kizuri mno cha migogoro katika kanisa hili watu hutoa hadi rushwa ili achaguliwe ...
Hakuna rushwa ili awe Askofu,mchakato wake sikama unavyochukulia.
Pili hakuna kugombea.
Kwani huyo Mwaikali ni msafwa?.
Akiwa msaidizi alichemka.
Wakadhani amebadilika akiwa ya mfumo.Sasa anawakimbiza hadi anahamisha kiti cha kikuhani wakati hakukiweka mimbarani.Moja ya watu waliopaswa kuwa wanyenyekevu kihuduma ni huyu.Sasa kafungua mafaili yote
 
umesahau moravian kwa kina anayejiita askofu wa chadema mwamakula (asiye hata na kanisa wala waumini wa maana), kuna kikanisa pale kimara kila wakati polisi huwa wanaenda kuamulia ugomvi waumini na wachungaji wameshikana mashati wanapigana ngumi. kila mtu mbabe kuanzia waumini, wazee wa kanisa hadi wachungaji.
Moravian angalau kidogo. Anglikana ndio baba lao.
 
Nina washikaj zangu wanne Ni wachungaji wa Lutheran.
Kila wkend Kuanzia ijumaa hua tunakula bia mwanzo mwisho na wanapenda bebez Ni hatari .
Jumapili tupo church
 
Suluhisho la migogoro ya madhehebu ni kugawanyika tu. Kkkt inashindwa nini kugawanyika vipandevipande kama wale wengine waliogawanyika mpaka wakatokea wenye ministry a.k.a mitume na manabii, na wanajaza watu kwenye ministry zao kwa amani na maisha yanaendelea
 
Muundo wa utawala ni yeye Mwaikali kakiuka.
Jibu ni;
Jina la Dayosisi KKKT-KONDE.
Makao makuu TUKUYU.
Kiti cha kiuaskofu- TUKUYU CATHEDRAL.
Umiliki wa kiwanja cha Makao makuu-Tukuyu.
Umiliki wa kilipo kiti cha Uaskofu ni ni Tukuyu.

Anaposimikwa alikabidhiwa hiyo katiba inayomwelekeza makao yalipo,akapewa na HATI MAALUM.

Ni hekima tu kaitumia mkuu wa kanisa kusema hivi.
"KITI CHA UASKOFU WA MWAIKALI KIRUDI TUKUYU"
Maana yake kama hataki anatakiwa kujiuzuru au kubaki mbeya mjini kusiko na
KITI CHA UASKOFU usiokuwa na hati.
KITI CHA UASKOFU wa hati maalumu wa Mwaikali kipo TUKUYU.
Kauli ya mkuu wa kanisa asipoitii waumini wanahaki yakumshitaki kwa uhaini.Pia amekosa sifa yakuwa mdhamini wa Dayosisi..
Inakuwaje mtu anakiuka utaratibu ili hali kuna utaratibu wa kumahuglikia
 
Mambo mengine ni kushangaza sana inakuwaje Kanisa lenye waumini wengi kujiendesha kama klabu ya pombe hukuna maelewano ni vurugu, tamaa ya mali hakuna uungu hapo.

Siku chache baada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Dk Fredrick Shoo kuagiza kiti cha Askofu Dk Edward Mwaikali kurejeshwa Dayosisi ya Konde Tukuyu, wachungaji wa majimbo matano kati ya saba wamepinga maagizo hayo.

Novemba 16, Dk Shoo alifanya ziara mkoani hapa kufuatia mgogoro wa kanisa hilo baada ya waumini kumtuhumu Askofu Dk Mwaikali kuhamishia mali za kanisa na kuzipeleka makao makuu ya Konde jijini Mbeya.

Katika kikao kilichofanyika Tukuyu, kikiwahusisha viongozi wa Serikali, akiwamo Kamanda wa Polisi Mkoa, Urlich Matei na Msajili wa jumuiya za dini kilicholenga kumaliza mgogoro huo, Dk Shoo aliagiza hadi kufikia Novemba 22 kiti cha Askofu kirejeshwe Dayosisi ya Tukuyu, ambapo wachungaji wameweka ngumu wakidai hawakufurahishwa na vitendo vya kiongozi huyo.

Wakizungumza jana jijini hapa kwenye kikao kilichohusisha wachungaji 67 kutoka majimbo matano kati ya saba, walisema hawakubaliani na uamuzi ya Dk Shoo kwa kuwa amelifedhehesha kanisa na viongozi wao.

Nyibuko Mwambola, mchungaji wa jimbo la Mbeya Mashariki alisema hawakubaliani na ubabe, uonevu na unyanyasaji aliofanyiwa Askofu Mwaikali.

Alisema hawakutarajia vyombo vya dola vitumike kuwalazimisha viongozi wa Dayosisi kufika kituo cha Polisi ili kukutana nao kwa mazungumzo badala ya kutumika kwa ofisi ya Dayosisi.

Agosti 22, 2021 waumini wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde Tukuyu walifanya vurugu wakipinga Askofu Mwaikali kuhamisha mali za kanisa hilo kuzipeleka makao makuu ya Ruanda Mbeya hadi Jeshi la Polisi lilipoingilia kati.
Hah hah Askofu Shoo alidhani KKKT Dayosisi ya Konde ni sawa na Chadema kule Kilimanjaro, sasa nyumba yake mwenyewe inateketea kwa kukosa maarifa,askofu Shoo wakati mwingi anatumia na kupoteza muda kuongelea na kukashifu uongozi wa serikali kwa kuwa ana mahaba na mchaga mwenzake, na anasahau majukumu yake hadi anadhauriwa na waumini wake, nadhani angetumia busara kutatua hilo tatizo la Dayosisi ya Konde kwani kama alikuwa hajui sasa ndio atajua Wanyakyusa ni watu wabishi na wenye msimamo wakisema HAPANA basi jua ni HAPANA ,hawapepesi macho wala kumwangalia sijui huyu ni nani, Wanyakyusa ni masikini jeuri wakiamua ,wameamua.
 
Haki KKKT wanaongoza kwa mihogoro ya hapa na pale jamani, huku kwetu washapiganaga na fyombo fya Dola fikaja.

Nasadiki kwa kanisa moja Katoliki Takatifu la Mitume, Naungama na ubatizo mmoja wa maondoleo ya Dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu na uzima wa milele ijayo!.


Sent from
 
Hiyo ilikua polite reminder tu kwamba ukinyooshea mtu kidole kimoja kuna vidole 3 vinakunyookea wewe. Tusijihesabie haki. Wote tumeoza, ni wadhambi. Na dhehebu halimpeleki mtu mbinguni bali matendo yake. Good night Princess
Hamna noma nmekusoma Kuhani
 
Back
Top Bottom